Hongera kwa walioleta uzi wa Chumvi ya Mawe

Niushirikina tu Hakuna kitu kibaya kama kumshirikisha mwenyezi Mungu
Wacha wee......

2 Wafalme 2:21​

Elisha akaenda kwenye chemchemi ya maji, akatupa chumvi hiyo ndani na kusema, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nimeyafanya maji haya kuwa yenye kufaa; tangu sasa hayatasababisha vifo au kutoa mimba.”
 
Hakuna cha chumvi ya mawe wala nini hizo ni blaah blaah

Ungekuwa una akili kwa sasa ungefanya uchunguzi kuangalia ni nini kimeboresha biashara yako na kuongeza kipato chako ukomae humohumo na uboreshe zaidi
Kuna maisha huyajui ndugu tena huyajui kabisa unadhan maisha uliyo yajua wewe ndio yameishia hapo hapo ,kuwa mwepesi na kujifunza mambo usiyoyajua usidhani hayapo, chumvi ilitumika hata na mitume wa mungu wenyewe.
 
Weweee...
Utaanza kuloga sasa hivi..
 
Kuna maisha huyajui ndugu tena huyajui kabisa unadhan maisha uliyo yajua wewe ndio yameishia hapo hapo ,kuwa mwepesi na kujifunza mambo usiyoyajua usidhani hayapo, chumvi ilitumika hata na mitume wa mungu wenyewe.
Sio kwa imani ya chumvi ya mawe, Mitume waliitumia kwa kazi gani?
 
Imani potofu.
 
Hiyo chumvi mnayoongelea si ndo hiyo wanalishia ng'ombe majani.
 
Hatusemi chumvi ndio itakufanya uokote pesa.

Ila itaondoa nguvu hasi kwenye mambo na maisha Yako.

Elewa neno NGUVU HASI.
Lipeni ZAKA,

Nguvu hasi inaletwa na WIZI wa ZAKA, Mungu huruhusu nguvu hasi ikupate Ili ustuke, utubu na kumrudia.

Alipaye ZAKA harogeki, hapungukiwi, Hana mikosi Wala balaa, nk nk.

UBARIKIWE 🙏
 
Hakuna cha chumvi ya mawe wala nini hizo ni blaah blaah

Ungekuwa una akili kwa sasa ungefanya uchunguzi kuangalia ni nini kimeboresha biashara yako na kuongeza kipato chako ukomae humohumo na uboreshe zaidi
Ndio maana kuna msemo unasema "work hard" na kuna ule wa "work smart". Misemo yote inahimiza jitihada na uwajibikaji ila tofauti yake ni ufanisi na tija.

Unaweza ukafanya jitihada na kujitesa kutwa nzima ila matokeo sisimizi. Huu ni mfumo wa watu wanao work hard.

Ila kuna wale ambao wanatumia akili zaidi nguvu kiasi tu na kupata matokeo makubwa. Hawa ndio wanao work smart.

Kama una akili uta relate na comment yako uliotoa bila tafakari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…