Hakuna lolote nyinyi ndio watu mbao mnateseka sana na maisha ya useja na mnatamani sana kuoa kuishi na mke
Ila changamoto mliyonayo inajulikana
Na sio yenu pekeyenu hiyo changamoto ni common kwa maisha haya ya sasa kwa kila mwanaume anayetafuta mwenza wa maisha
Maisha ya sasa kupata mwenza sahihi imekuwa mtihani mkubwa
ila chakushangaza wanaume wanawalalamikia wanawake uwongo/kuzingua pindi unapomuonesha nia ya kutaka kumuoa
Hali kadharika kwa wanawake pia kulalamika kuzinguliwa pindi tu aanapoonesha kukubali kuwa na mwanamme kwa hali yoyote ili kuingia nae ndoani
Yaan imekuwa tabu tupu vululuvululu
Kilichopo nyinyi mmekata tamaa kwa kutompata sahihi kwenu
Msitake kutuaminisha uwongo wakt COMMENT na THREAD zenu za nyuma zinajielezea tabu kwenu ipo wapi
Na sema hakuna asiyependa KUOA KUOLEWA tabu ni kumpata mtu sahihi wa kuingia NDOANI shida inaanzia hapo na ukiangakia umri unazidi kwenda aisee tabu tupu