Hongera Mbowe umeshinda mchezo wa kisiasa

Upinzani na maridhiano hivi vyote ni mazigaombwe tu Kwa wananchi.

Ukweli ni kwamba Tanzania hatujawahi kuwa na chama chochote Cha upinzani, hivi tunavyoviona ni matawi ya ccm hata viongozi wake ccm ndiyo inaamua nani awe kiongozi.
 

Kukubali kutokubaliana ni sehemu ya mchezo:

Tathmini yakinifu uzinduzi wa mikutano ya siasa Mwanza:​


 
Naomba nichukue fursa hii kusema Hotuba ya jana ilikuwa ni kete ya mwisho na ya hatari katika game la kisiasa Chadema vs CCM+Serikali katika mechi iliyoanza tangu Mbowe atoke jela 4 March 2022. Mbowe ameshinda!
 
Kwanini asemi wameridhiana kwenye nini na nini?

Unataka kusema miezi yote walikuwa wanajadiliana kuhusu mikutano tu?
 

Kwa hiyo maridhiano ya CCM na Chadema na hizo siasa wanazoita za kistaarabu ndio zitawapeleka Chadema ikulu?
 
Ufunguzi ndio Mwenyekiti kufanya kazi za Sofia Mjema kuongelea CCM na serikali yake?
 
Vipi CDM wakisem tutoke Barabarani utatoka? Mna hulka za kike then mnasema maridhiano yataivuraga CDM, na CDM wakisema tuingie barabarani hamuonekani

Watu tuna vilema hapa vya kuingia barabarani, labda useme kingine. Kuna watu tulijitoa kuwapigania wakaishia kuunga juhudi, kisha wakahongwa vyeo hivyo hivyo kwa mlango wa uani. Sasa sijui unaongea nini boss.
 
Mleta mada ni vzr tukaweka akiba ya maneno hii nchi inachezewa sana na wanasiasa CCM wanatujua watanzania tulivyo na wanajua aina ya wanasiasa walewale wanaowafahamu na kwamba hawabadiliki na wanajua maeneo ya kuwachezesha wanasiasa wetu.Hii ni mapema sana kuweza kujua kilichomo kwenye mioyo yao,hivyo vikao walivyokaa na Rais hakuna ajuae undani wake.Muda ni rafiki mzuri sana tusubiri.
 
...... kupitia nyinyi tutapata Katiba Mpya bila kumwaga Damu bali kupitia njia hii nzuri ya Maridhiano.

Na Yericko Nyerere.
View attachment 2491265
Yericko, upo serious kweli? Unajua katiba mzuri ni ile inamnyang'anya madaraka Rais, inatoa haki ya matokeo ya kura ya urais yapelekwe mahakamani? Ni katiba inayotoa kibali Rais ashitakiwe akimaliza muda wake kwa makosa aloyatenda akiwa madarakani? Unajua vitu kama hivyo ni Yezu tu anaweza kusaini ili vimbane yeye? Zamani nilikuona wewe ni kichwa ila kwa andiko hili, mh!!!!
 
9 Mambo yote huwa ayapatikani kwa wakati mmoja, kama kuna juhudi hata kidogo za kutufikisha huko tusizibeze. Tuonyeshe sapoti. Sasa nyie mnaobeza mna taka nini? Njooni na suluhisho sio kubeza tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…