Hongera Nape Nnauye kwa kurudi kwenye nafasi ya Uwaziri

Hongera Nape Nnauye kwa kurudi kwenye nafasi ya Uwaziri

Kidenga

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2018
Posts
233
Reaction score
676
Ninapenda kutumia jukwaa hili kumpongeza waziri wa michezo Nape Nauye.

Hizi pongezi ni mahususi kwa Nape kwa sababu ni moja ya viongozi walioweza kusimamia haki na ukweli kwa kulipa gharama kubwa ya kupoteza nafasi yake ya Uwaziri.

Funzo: Viongozi mnaoteuliwa simamieni haki bila kujali kama nafasi zenu zitakuwa hatarini. Mungu pekee ndo mpaji.

Using'ang'ane kulinda nafasi yako kwa kuumizawengine. Haki itakuinua. Dhuluma itakushusha.

Nadhani unaweza kuona kuna aliepoteza nafasi na kuna aliepata nafasi. Wawili hawa tofauti yao mmoja alijaribu sana kulinda nafasi yake hata kama anayotenda ni chukizo kwa Mungu na kwa wanadamu.

Wa pili alilipa gharama na leo amelipwa. Tuwe watu wa haki.
 
Yule waziri anatoa macho macho anaitwaje?
 
Ha ha ha hawa si ndio walikuwa wanalilia kupewa fadhila hata ya barabara kuitwa kwa majina yao. Hongereni wahuni, mmeingia mitamboni
 
Well done my minister, bado upo kijana na pls tumia busara zako na usilipe visasi, fungua uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza bila woga na elewa vyombo vya habari ni moja ya kioo cha serikali na ikumbushe serikali kuhusu sheria ya public kupata habari.
 
Nape Ni waziri wa habari sio michezo mkuu. Waziri wa utamaduni na michezo ni mchengerwa.
 
Nikupongeze kwa kuaminiwa tena kwa mara ya pili na mhe Rais wa JMT na kukupa uwaziri.

Maisha yetu ndivyo yalivyo hapa duniani yanaenda mbele na kurudi nyuma. Ni imani yangu ulipokuwa nje ya uwaziri ulijifunza mambo mengi ambayo yatakuwa na tija kwa taifa letu. Hongera na Karibu sana.

Hata hivyo nitakiwa sijawatendea haki Mhe Hussein Bashe kwa kazi zako na mwisho kwa Mhe. Ridhiwani Kikwete. Kwa umri wenu mna mambo mengi ya kulitendea taifa letu.

Mwenyezi Mungu awatangulie ktk kutekeleza majukumu yenu.
 
Nafikiri amepewa nafasi ajisafishe kwa mambo mawili, moja ni bunge live, pili ni bao la mkono.
 
Nape atulie afanye kazi misimamo ambayo haina msingi inayokwenda kunyume na msimamo wa serikali ya awamu ya sita haitaleta picha nzuri,ni kweli anastahili hiyo nafasi kulingana na mwonekano wake kuwa na vitu vingi kichwani vyenye tija kwa taifa pili ana munkali wa kutosha wa kufanya kazi na kitu kingine asipende sana kuonekana kwa wapinzani kuwa yeye ni mtu wa haki sana yeye cha msingi afanye kazi kwa taratibu zinavyosema na kuishi kwa akili na mkuu wa nchi na watanzania basi kinyume na hapo ataona viongozi wake ni wabaya na hawatambui mchango wake.
 
Back
Top Bottom