Hongera Nape Nnauye kwa kurudi kwenye nafasi ya Uwaziri

Kulipa kisasi ni haki ya Bw. Nape. Kama unabisha uliza mashekh.
 
Binafsi iliniuma sana Namna Nape alivyofanyiwa. Pia alivyokwenda kwa JPM kuomba Msamaha niliona huruma sababu nilidhani yeye ndiye ilistahili KUOMBWA MSAMAHA.

Kibinadaam tunasema Mama kamrejesha tena lakini Kiimani wengine tunaamini ni MUNGU kamuinua tena. Pia waliomnyanyasa ni funzo kwako.
 
Yule waziri anatoa macho macho anaitwaje?
Unamaanisha huyu?
IMG-20220108-WA0035.jpg
 
Nafikiri amepewa nafasi ajisafishe kwa mambo mawili, moja ni bunge live, pili ni bao la mkono.
Hahahahaaa!!! Atakumbuka basi? Wakishakalia zile ofisi unashindwa kuelewa wanakula maharage ya wapi. Mkapa alijuta kwamba kwa miaka 10 akiwa enzini, alisahau kabisa masuala ya kilimo (ambacho kimeajiri zaidi ya 75% ya watz)!
 
Ninapenda kutumia jukwaa hili kumpongeza waziri wa michezo Nape Nauye.

Hizi pongezi ni mahususi kwa Nape kwa sababu ni moja ya viongozi walioweza kusimamia haki na ukweli kwa kulipa gharama kubwa ya kupoteza nafasi yake ya Uwaziri.

Funzo: Viongozi mnaoteuliwa simamieni haki bila kujali kama nafasi zenu zitakuwa hatarini. Mungu pekee ndo mpaji.

Using'ang'ane kulinda nafasi yako kwa kuumizawengine. Haki itakuinua. Dhuluma itakushusha.

Nadhani unaweza kuona kuna aliepoteza nafasi na kuna aliepata nafasi. Wawili hawa tofauti yao mmoja alijaribu sana kulinda nafasi yake hata kama anayotenda ni chukizo kwa Mungu na kwa wanadamu.

Wa pili alilipa gharama na leo amelipwa. Tuwe watu wa haki.
Haki iko mbinguni tu
 
Na sherehe juu
 
Attachments

  • IMG_4721.MP4
    8.8 MB
Back
Top Bottom