Hongera Rais Magufuli kuipendezesha Ikulu yetu kuliko enzi za Nyerere, Ikulu iwe kivutio cha utalii, restrictions ziondolewe watalii wafurike

Itaingiza pesa nyingi kuliko hifadhi ya Burigi-Chato.
Ikulu ni mahali sensitive hauwezi kupafanya Zoo bila mipango. Usalama wa Mweshimiwa lazima uimarishwe, eneo la Ikulu ni dogo, kuruhusu watu kuingia na kutoka ni hatari kwa Raisi na uongozi mzima wa nchi

Wenzetu Marekani eneo la Ikulu ni kubwa na kwenye usalama wapo vizuri, kuliko sisi kwa asilimia kubwa

Kama kuna umuhimu wa kuifanya ikulu iwe na Zoo ya kutembelewa na wageni basi coverage ya ikulu iongezwe ili kuziya watu kuingia maeneo nyeti
 
Anzisha uzi wako uandike hayo maujinga ujinga yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi upeo wako umeishia hapo, sikulaumu.
Ungejitahidi kwenda mbele zaidi ungeona niliyoyaona mimi. Basi hata hapo kwa Bashite hujaelewa kitu!!??

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungeyaweka wazi na kutoa mtazamo wako siyo kusema niliyoyaona mimi...mimi nimechulua tafsiri nzima ya andiko wewe kama umeona mengine ambayo kwa jicho la kawaida hayaonekani hongera yako. Bashite ndio nani? kwenye andiko sijaona neno Bashite...
 

Na wewe kwenye hili kundi unaingia...unaonekana huwa hauelewi unakurupuka kuwasemea watu...toa maoni yako halafu pita na zako...
 
Sijakuelewa kwa hoja mbili,

1. Ofcurse ita make kuliko hata chato
2. Akae ikulu mpaka Mungu aamue

Nijajua uwezo wako wa kufikiri ni mkubwa sana, sina shaka kabisa kwamba unajua ulichomaanisha,nifumbue macho maana najua wewe ni mjanja mjanja, huenda kuna kitu unatafuta, Nanukuu " Mayala maana yake kwetu ni njaa" mwisho wa kunukuu
 
Dah ila wewe jamaa, Aisee JULIUS KAMBARAGE NYERERE ATABAKI KUWA JUU SANA, ANATEFUATA NI MKAPA THEN KIKWETE, THEN MWINYI WA MWISHO JEIPIEMU
Sent using Jamii Forums mobile app
 
JPM humuoni huyu mtu tu anayeitwa Mayalla umpe hata ukuu wa mkoa kwa jinsi anavyoleta kipele kwako mara kwa mara ukikune?
Kipele kinawasha sana!
Bandiko lako halistahili kabisa kuwepo. Jibu hoja iliyotolewa kwa kutoa maoni tofauti. Mchangiaji ametoa mawazo yake. Wewe, kwa kuwa tu hukubaliani na mawazo hayo, unaishia kusema anajipendekeza bila hata ya kukosoa hoja iliyotolewa kwa kutoa hoja tofauti. Hicho ni kiburi kisichokuwa na tija.
 
Binafsi nimeona jana, lakini sikufikiria mbali kama brother Pacal. Hapa ndipo wanasema ukubwa dawa, andiko la Pascal imekuwa dawa.

Ninaomba kuuliza jambo moja la ufahamu. Wapo wanyama niliwaona pale ambao wanamadhara kwa binadamu. Je, watatumia njia gani kuwahifadhi ili wasilete madhara kwa binadamu wanaoishi ikulu? Je, chakula cha hao wanyama ni nini? Hawatabadili tabia kutoka kwenye natural kuwa kwenye artificial?
 
Umesoma alichoandika Mzee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…