Hongera Rais Magufuli kuipendezesha Ikulu yetu kuliko enzi za Nyerere, Ikulu iwe kivutio cha utalii, restrictions ziondolewe watalii wafurike

Hongera Rais Magufuli kuipendezesha Ikulu yetu kuliko enzi za Nyerere, Ikulu iwe kivutio cha utalii, restrictions ziondolewe watalii wafurike

Unazungumziaje kuhusu Ile Nyumba ya Magogoni kuwa chafu kutokana na kinyesi Cha wale wanyama barabarani kila wakati, au ndo unapendekeza waajiri mtu kwa ajili ya kuzoa kinyesi barabarani kila sekunde ?
 
Hawa waandishi bhana kazi kweli kweli,

Anataka Rais atawale maisha yake yote kisa kaleta baadhi ya wanyama Ikulu, ha ha haah! Mbona hajaleta Simba?

Pili, huyu Rais si alisema kahamia Dodoma, sasa hapo Magogoni anafanya nini? Kwa nini hao wanyama asipeleke huko porini chamwino?

Tatu, unasema ameipendezesha ikulu kuliko enzi za Mwalimu, je kuna lipi jipya hapo zaidi ya akili za reverse tu, ni aibu sana mpaka sasa mambo mengi aliyafanya Nyerere, awamu hii ina igiza tu hakuna jipya wala ubunifu.

Nne, je kusifia sifia kusiko na mpango tatizo ni, USUKUMA au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bashite tena? Huyu anatakiwa apunguziwe majukumu, ashushwe na kuondolewa nafasi aliyonayo.
 
Nyie hamkuwepo enziza mwinyi!! Ilikuwa kichekesho... na ndie alieggawa wanyama waliokuwepo ikulu kwa wageni! Baada ya kuuza mbuga ya Loliondo kifisadi kwa waarabu!

Mwinyi ndie aliondoa Elimu bure iliyokuwa100%, matibabu bure yaliyokuwa 100%....na urojo mwingine! Barbarosa,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ikulu kuna nyasi za kutosha?au kuna shamba boys wa ikulu wa kulisha hao wanyama? Na hao wanyama wasijeharibu viwanja vya ikulu kama Mondi alivyovuruga uwanja wa Mbeya.
 
Pascal Mayalla,
Nimeishia hapo akae mpaka atakapomua, sasa akae kama nani kwa kuwa atachaguliwa mwingine, sasa hapo yeye atakuwa anafanya nini?au jengo hilo aachiwe Rais mwingine ajengewe ikulu ingine?

Unajuwa sijakuelewa P .
 
Back
Top Bottom