Hongera Rais Magufuli kwa kulitatua tatizo sugu la mgao wa umeme nchini

Hongera Rais Magufuli kwa kulitatua tatizo sugu la mgao wa umeme nchini

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Kuanzia mwaka 2006 mpaka rais magufuli anaingia madarakani nchi yetu ilikuwa mara kwa mara ikikumbwa na tatizo kubwa la mgao wa umeme. Tatizo ambalo kwa muda mrefu lilikuwa mwiba kwa taifa letu. Vinyozi,wenye saluni za kike, wenye mabaa mpaka wenye viwanda lilikuwa ni tatizo linalowaumiza.

Ulipoingia madarakani ulisema hili tatizo litakuwa kweli mwisho. Na kwa hakika sasa tumesahau. Maana kama umeme ukikatika ujue kuna hitilafu na matengenezo. Lakini sio mgao wa umeme eti kwa sababu umeme hautoshelezi.

Swali ambalo mimi nimejiuliza kichwani kwangu je kwa nini kipindi hicho kulikuwa na mgao wa umeme wa karibu siku tatu au wiki kwa baadhi ya mikoa ? Je ilikuwa ni dili za wauza jenereta? Na wewe ulipoingia ukazibana na sasa umeme unapatikana masaa 24!

Je zilikuwa deal za wajanja wachache kama akina Harbinder Seth na wenzake ili waweze kupata tenda za kuizuia umeme Tanesco na kisha kulipwa malipo ya capacity charges yanayoiumiza Tanesco. Ila wewe ulipoingia ukavunja na mkataba wa Tegeta Escrow.

Au ndio zilikuwa hujuma za watumishi wa Tanesco kwenye hydropower stations ambao walishirikiana na mafisadi ili kufungulia maji yapungue kwenye mabwawa ili umeme usizalishwe kama inavyohitajika. Ila wewe ulilishutukia hili na kuwatimua. Sasa mgao wa umeme sio hadithi tena.

Je, kama hali iko hivi Je JNHPP ikikamilika mambo yatakuwaje?

Jambo linalosikitisha pamoja na mambo mazuri unayoyafanya wafuasi wa Chadema na wanachama wao hawana uzalendo na kukushukuru kwa namna ulivyojitoa ili Tanzania iliyokuwa imepinda inyooke.

Ila nakupa pongezi kwa hili na kwa mantiki hii kura za urais Mungu akipenda utapata 99.5%.
 
Kwa hili la umeme kweli wangalau amefanya vizuri, sio kwamba haukatiki kabisa, bali haukatiki muda mrefu kama zamani. Hao unaotaka wamshukuru sio wajibu wao kwani rais anafanya hilo kama wajibu wake maana analipwa mshahara. Ila hakuna anayemlaumu kwenye eneo hilo, maana umeme unapatikana kwa asilimia kubwa baada ya watu kuulipia. Kama unataka kumsifia msifie kwa muda wako. Itakuwa wendawazimu kumsifia mzazi aliyemlipia ada mtoto mpaka chuo kikuu huku akimlawiti.
 
tindo bila kuwa na political will hili jambo ni gumu. Lazima umpongeze JPM.
 
chagu wa malunde,

"Kama hatutajenga utaratibu wa kuongozwa na sheria, Basi tutakuwa tumeruhusu kuongozwa kidikteta,Nia yangu haikuwa kujenga taifa la watu waoga,ukitaka kutawala nchi bila udikteta basi hakikisha unaongoza nchi kwa kufuata sheria'' Mwalimu Julius Nyerere
 
Stuxnet kwani mzalendo namba moja anaendesha nchi kwa presidential decrees? Si anafuata sheria na katiba ya JMT
 
Mgombea u-Rais alipokuwa anaomba kura mwak 2015 alitoa AHADI kuwa nitafanya haya na haya. Wapiga kura wakalinganisha kati ya yeye na mpinzani then wakampa yeye kura akashinda. Sasa anatekeleza yale aliyo YAAHIDI ambayo ni wajibu wake, SWALI, kwa nini nyie mnataka TUMSIFIE 24/7? isitoshe kila mradi anaoutekeleza anatumia kodi zetu sisi wenyewe, kwa nini mnakomaa mishipa KUMSIFIA?

Wanaotaka KUSIFIWA wana dalili zote za UDIKTETA na hivyo ndivyo alivyokuwa Adolf Hitler na Benito Mussolini
 
Yaani kujibu hilo swali tu umeshindwa? Halafu unakuja na majumuisho hapa hakuna mgao?
Asante na nikutakie asubuhi njema.
UMEME HAUKATIKI KABISA

Kwani wewe upo Nchi gani, ulishawahi kuona magenerator yakinguruma Maduka yote mwezi mzima na Kidatu, mtera maji yamejaa? Ungeweza kushinda JF km leo simu full charge na computer hazizimwi tunashusha mavitu usiku kucha?
Hapo huna Shukrani kabisa kwa Magufuli, ulizia Nchi jirani zinavyolia na mgawo
Mm sitamsahau huyu jamaa nalipia kwa mwezi sh 9,500. @ mwezi na ninawasha kila kitu 24hr/7/30/mwaka nipo mwaka wa 4 sijazima
 
Stuxnet kwani mzalendo namba moja anaendesha nchi kwa presidential decrees? Si anafuata sheria na katiba ya JMT
Kwanza usimuite Mzalendo Na 1 unless unihakikishie kuwa BAKITA wametoa tafsiri nyingine ya neno Mzalendo. Hafuati katiba hata dakika moja. Ila anaifuata pale tu kama kuna vifungu/ ibara inamsaidia yeye kuimarisha UDIKTETA wake
 
UMEME HAUKATIKI KABISA
kwani wewe upo Nchi gani, ulishawahi kuona magenerator yakinguruma Maduka yote mwezi mzima na Kidatu, mtera maji yamejaa?
ungeweza kushinda JF km leo simu full charge na computer hazizimwi tunashusha mavitu usiku kucha?
Hapo huna Shukrani kabisa kwa Magufuli, ulizia Nchi jirani zinavyolia na mgawo
Mm sitamsahau huyu jamaa nalipia kwa mwezi sh 9,500. @ mwezi na ninawasha kila kitu 24hr/7/30/mwaka nipo mwaka wa 4 sijazima

UTAKUW AUPO KANDA PENDWA
 
Wewe upo wapi kwani? Unanukia harufu ya Chadema.
Unapoulizwa jibu si kila kitu mnaweka hayo mavyama yenu. Mkoa nilioko bado umeme ni tatizo, ni kama vile mgao upo ila taarifa hazitolewi tu mkuu. Najua unafanya kazi yako.
 
Mgombea u-Rais alipokuwa anaomba kura mwak 2015 alitoa AHADI kuwa nitafanya haya na haya. Wapiga kura wakalinganisha kati ya yeye na mpinzani then wakampa yeye kura akashinda. Sasa anatekeleza yale aliyo YAAHIDI ambayo ni wajibu wake, SWALI, kwa nini nyie mnataka TUMSIFIE 24/7? isitoshe kila mradi anaoutekeleza anatumia kodi zetu sisi wenyewe, kwa nini mnakomaa mishipa KUMSIFIA?

Wanaotaka KUSIFIWA wana dalili zote za UDIKTETA na hivyo ndivyo alivyokuwa Adolf Hitler na Benito Mussolini
Ni wangapi ambao wanaomba kura alafu wakishapata hawayatekelezi haya?
 
Unapoulizwa jibu si kila kitu mnaweka hayo mavyama yenu. Mkoa nilioko bado umeme ni tatizo, ni kama vile mgao upo ila taarifa hazitolewi tu mkuu. Najua unafanya kazi yako.
Mkoa gani? Maana siku hizi Jf ndio mahala pa kuibua madudu. Hata ukikatika bila taarifa watu wanafungua uzi.
 
Back
Top Bottom