Hongera Rais Magufuli kwa kulitatua tatizo sugu la mgao wa umeme nchini

Hongera Rais Magufuli kwa kulitatua tatizo sugu la mgao wa umeme nchini

UTAKUW AUPO KANDA PENDWA
Mm nipo huku Mlimani juu kabisa anakoishi aliyekuwa Mkrugenzi wa Tanesco Bw Mrema, eti alimgomea Msukuma kuwa nchii ni lazima kuwepo na Mgawo la sivyo tutajuta tutashtakiwa kumbe Harbinder Sigh na yule Mhaya anayetoka karibu na Magufuli wanatukomba mahela kwa kujitengenezea ulaji sasa wako wapi? mbona Mrema ni siku moja tu katumbuliwa? nani tena atakata umeme kwa siku?

HONGERA MAGUFULI, mm napata maji ya baridi Friji Computer TV nk havizimwi kwa 9,500 tu
 
What's so special alichofanya JPM kwenye umeme?!

Kwa wanaofuatilia wanafahamu mahali kama Dar moja ya changamoto kubwa ilikuwa miundombinu! Ni wakati Muhongo yupo waziri awamu ya 4 ndipo miundombinu iliboreshwa sehemu mbalimbali.

Aidha, ili kuondokana na kutegemea umeme wa maji kwa mabwawa ambayo yamejengwa tangu ukoloni na kuachana na matumizi ya mafuta, likajengwa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es salaam.

Baada ya kujengwa Bomba la Gesi, mitambo ambayo zamani ilikuwa inatumia mafuta ikaanza kutumia gesi, na wakati anaingia JPM tayari umeme ulishaanza kuzalishwa, na yeye akaongeza tu Kinyerezi III.

Hakuna mradi mkubwa hata mmoja ambao Magu ameuanzisha, no wonder anang'ang'ania Stiegler ili aache alama huko manake wakati Mkapa kajenga Ubungo Power Plant kwa kutumia Gesi ya Songosongo, JK akajenga Kinyerezi kwa kutumia gesi ya Mnazi Bay!

Nitajie Power Plant iliyojengwa na Magufuli!
 
Mgombea u-Rais alipokuwa anaomba kura mwak 2015 alitoa AHADI kuwa nitafanya haya na haya. Wapiga kura wakalinganisha kati ya yeye na mpinzani then wakampa yeye kura akashinda. Sasa anatekeleza yale aliyo YAAHIDI ambayo ni wajibu wake, SWALI, kwa nini nyie mnataka TUMSIFIE 24/7? isitoshe kila mradi anaoutekeleza anatumia kodi zetu sisi wenyewe, kwa nini mnakomaa mishipa KUMSIFIA?

Wanaotaka KUSIFIWA wana dalili zote za UDIKTETA na hivyo ndivyo alivyokuwa Adolf Hitler na Benito Mussolini
Miaka yote kodi zimekuwa zinalipwa. Ila mambo aliyoyafanya JPM yanastahili pongezi. Maana amejitoa, na kusema ukweli sio kumsifia mtu. Hayo ya Benito na Hitler ni mifano mfu.
 
What's so special alichofanya JPM kwenye umeme?!

Kwa wanaofuatilia wanafahamu mahali kama Dar moja ya changamoto kubwa ilikuwa miundombinu! Ni wakati Muhongo yupo waziri awamu ya 4 ndipo miundombinu iliboreshwa sehemu mbalimbali.

Aidha, ili kuondokana na kutegemea umeme wa maji kwa mabwawa ambayo yamejengwa tangu ukoloni na kuachana na matumizi ya mafuta, likajengwa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es salaam.

Baada ya kujengwa Bomba la Gesi, mitambo ambayo zamani ilikuwa inatumia mafuta ikaanza kutumia gesi, na wakati anaingia JPM tayari umeme ulishaanza kuzalishwa, na yeye akaongeza tu Kinyerezi III.

Hakuna mradi mkubwa hata mmoja ambao Magu ameuanzisha, no wonder anang'ang'ania Stiegler ili aache alama huko manake wakati Mkapa kajenga Ubungo Power Plant kwa kutumia Gesi ya Songosongo, JK akajenga Kinyerezi kwa kutumia gesi ya Mnazi Bay!

Nitajie Power Plant iliyojengwa na Magufuli!
Hata kabla ya mtambo wa gas pale ubungo na na mtambo wa kinyerezi .Hydropower stations zote zilikuwa na uwezo wa kuzalisha Megawatts zaidi ya 800, lakini zilipatikana kama megawatt 650.Mafisadi na wahuni wakaleta kisingizio cha ukame kuwa mabwawa hayatoshelezi. Ndio kukawa na mgao mkubwa sana ambao ulikuja kuzalisha Richmond,Dowans na Escrow. Kule kwenye Hydropower stations kulikuwa na hujuma ya kufungulia maji. Ili ionekane hayatoshi. Hilo limedhibitiwa. Kwa hiyo hoja sio kujenga plant bali ni namna gani waliokuwa wanahujumu wamedhibitiwa na sasa hakuna mgawo. Sio habari ya miundo mbinu ya Dar Mgao ulikuwa nchi nzima.kila mkoa.
 
Wewe uliyeandika hii habari upo wapi (Mkoa gani)?

Sent using Jamii Forums mobile app
Inaonekana ni Musukuma wa Chato akiwa na anayesifiwa alikokimbilia kukwepa kuambukizwa Covid-19 iliyoenea kila mtaa Dar. Maswali ya kijinga kutoka kwa mjinga yanaonyesha anatafuta uteuzi kwa kusifia kwtsha kwa mgao wa umeme sasa huku akiuliza maswali mengi ya kwa nini huko nyuma kulikuwa na mgao mara kwa mara. Pamoja na sifa hizo bado kuna maeneo mengi yana matatizo makubwa ya umeme. Kama kuna maeneo yasiyo na tatizo LA umeme, sifa ziende kwa watangulizi walioandaa miundombinu madhubuti ya umeme. Awamu hii ingoje sifa, posthumously, 2030+.
 
UMEME HAUKATIKI KABISA
kwani wewe upo Nchi gani, ulishawahi kuona magenerator yakinguruma Maduka yote mwezi mzima na Kidatu, mtera maji yamejaa?
ungeweza kushinda JF km leo simu full charge na computer hazizimwi tunashusha mavitu usiku kucha?
Hapo huna Shukrani kabisa kwa Magufuli, ulizia Nchi jirani zinavyolia na mgawo
Mm sitamsahau huyu jamaa nalipia kwa mwezi sh 9,500. @ mwezi na ninawasha kila kitu 24hr/7/30/mwaka nipo mwaka wa 4 sijazima
Hongereni huko kwenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo halikuwepo kipindi ya Nyerere, likatengemezwa kipind cha [Mkapa na JK] ft Lowassa likatatuliwa na Magufuli walewale unajitungia pepa halafu unasolve mwenyewe, halafu unajiita wewe kipanga!
 
chagu wa malunde,

"Kama hatutajenga utaratibu wa kuongozwa na sheria, Basi tutakuwa tumeruhusu kuongozwa kidikteta,Nia yangu haikuwa kujenga taifa la watu waoga,ukitaka kutawala nchi bila udikteta basi hakikisha unaongoza nchi kwa kufuata sheria'' Mwalimu Julius Nyerere
Nakumbuka maombi yetu wengi Chadema tuliomba sana tupate rais mkali sijui tumesahau?
 
Hata kabla ya mtambo wa gas pale ubungo na na mtamb[/URL]o wa kinyerezi .Hydropower stations zote zilikuwa na uwezo wa kuzalisha Megawatts zaidi ya 800, lakini zilipatikana kama megawatt 650.Mafisadi na wahuni wakaleta kisingizio cha ukame kuwa mabwawa hayatoshelezi.
TANESCO wenyewe wanasema 58.5% ambayo ni 796.34MW ya umeme unaozalishwa nchini unatokana na thermal gas and diesel.

Kabla hamjampa Magufuli sifa ambazo sio zake kama ilivyo kawaida yenu, nitajie thermal gas and diesel plants zilizoanzishwa na Magufuli Administration.

Aidha, 41.5% ya umeme unaozalishwa ambayo ni 561MW, huu unatokana na maji.

Mosi, wewe umezitoa wapi hizo 800MW ambazo Sterling Magufuli alipoingia tu madarakani, "akabomoa bomoa" kuta zilizokuwa zinazuia maji na matokeo yake umeme ukaanza kuwa wa kumwaga!!

Pili, kwavile post ya awali nimekuuliza unitajie power plants initiated and built by Magufuli administration lakini umeshindwa kutaja, ina maana alichofanya Magufuli kubwa zaidi ni kudhibiti the so-called waliokuwa wanazuia maji ambao hata nikikuuliza katika hilo zoezi ameokoa megawatts ngapi katu huwezi kuwa na jibu!!!

So, unataka kusema pongezi zote hizo ni kwa sababu aliweza kudhibiti waziba maji ambao hata nikikuuliza katika kudhibiti huko ameokoa MW ngapi, katu hutaweza kujibu!!!

Narudia, kazi kubwa kwenye umeme imefanywa na Mkapa pamoja na JK na sio Magufuli baada ya kufanikisha kutoa gas kutoka Lindi na Mtwara hadi Dar es salaam, na hapo ikawa ndio mwisho wa ku-rely heavily kwenye diesel kuendesha power plants kadhaa za Dar es salaam ambazo zimeingizwa kwenye national grid.

Kinyerezi peke yake inazalisha karibu 400MW kutokana na gas ya Mtwara ambayo bomba lilijengwa mwaka 2013. Pale Ubungo zinazalishwa takribani 230MW kutokana na gas kutoka Lindi!

Sasa pamoja na yote hayo, sifa apewe Magufuli ambae hajaanzisha plant yoyote ya uzalishaji wa umeme?! WHY?! Jibu ni very simple: Kwa mfuatiliaji anajua Magufuli kaanzisha miradi michache sana ambayo ipo successful.

Kutokana na hilo, Wafuasi wake wanalazimika kumsifia kwa vitu ambavyo hata hajafanya yeye, manake hata hizo flyovers za Dar es salaam, ukweli ni huu hapa kama unavyoelezwa na Wajapan wenyewe:-
Tanzania National Roads Agency (TANROADS) and Sumitomo Mitsui Construction Co.,Ltd. (SMCC) signed a contract on 15th October, 2015 concerning the project for Improvement of Tazara Intersection which will mark the construction of the first Flyover in Tanzania under the framework of the grant aid project supported by JICA
Na ukifuatilia, utakuat projects zote mbili, TAZARA na Ubungo, zilitokana na ombi la serikali la mwaka 2007, kwahiyo JPM kaja kujenga tu manake kila kitu kilishakamilika, including funding.
 
TANESCO wenyewe wanasema 58.5% ambayo ni 796.34MW ya umeme unaozalishwa nchini unatokana na thermal gas and diesel.

Kabla hamjampa Magufuli sifa ambazo sio zake kama ilivyo kawaida yenu, nitajie thermal gas and diesel plants zilizoanzishwa na Magufuli Administration.

Aidha, 41.5% ya umeme unaozalishwa ambayo ni 561MW, huu unatokana na maji.

Mosi, wewe umezitoa wapi hizo 800MW ambazo Sterling Magufuli alipoingia tu madarakani, "akabomoa bomoa" kuta zilizokuwa zinazuia maji na matokeo yake umeme ukaanza kuwa wa kumwaga!!

Pili, kwavile post ya awali nimekuuliza unitajie power plants initiated and built by Magufuli administration lakini umeshindwa kutaja, ina maana alichofanya Magufuli kubwa zaidi ni kudhibiti the so-called waliokuwa wanazuia maji ambao hata nikikuuliza katika hilo zoezi ameokoa megawatts ngapi katu huwezi kuwa na jibu!!!

So, unataka kusema pongezi zote hizo ni kwa sababu aliweza kudhibiti waziba maji ambao hata nikikuuliza katika kudhibiti huko ameokoa MW ngapi, katu hutaweza kujibu!!!

Narudia, kazi kubwa kwenye umeme imefanywa na Mkapa pamoja na JK na sio Magufuli baada ya kufanikisha kutoa gas kutoka Lindi na Mtwara hadi Dar es salaam, na hapo ikawa ndio mwisho wa ku-rely heavily kwenye diesel kuendesha power plants kadhaa za Dar es salaam ambazo zimeingizwa kwenye national grid.

Kinyerezi peke yake inazalisha karibu 400MW kutokana na gas ya Mtwara ambayo bomba lilijengwa mwaka 2013. Pale Ubungo zinazalishwa takribani 230MW kutokana na gas kutoka Lindi!

Sasa pamoja na yote hayo, sifa apewe Magufuli ambae hajaanzisha plant yoyote ya uzalishaji wa umeme?! WHY?! Jibu ni very simple: Kwa mfuatiliaji anajua Magufuli kaanzisha miradi michache sana ambayo ipo successful.

Kutokana na hilo, Wafuasi wake wanalazimika kumsifia kwa vitu ambavyo hata hajafanya yeye, manake hata hizo flyovers za Dar es salaam, ukweli ni huu hapa kama unavyoelezwa na Wajapan wenyewe:- Na ukifuatilia, utakuat projects zote mbili, TAZARA na Ubungo, zilitokana na ombi la serikali la mwaka 2007, kwahiyo JPM kaja kujenga tu manake kila kitu kilishakamilika, including funding.
Nafikiri unajibu kitu bila kujua hoja ni nini? Nimekuambia awali Tanesco walikuwa wanauwezo kuzalisha Megawatts tena sio mia nane ni zaidi ya mia nane. Ikafanyika hujuma zikawa zinapatikana kama 650 megawatts. Hapa ndio ikawa chanzo cha mgao na ufisadi mwingi. Hoja sio kujenga plant au kuanzisha. Hoja ni kudeal na hujuma mpaka akahahakikisha mgao unapotea. Kuhusu nani alianzisha wala halina tabu hii ni serikali ya Ccm na wanapokezana vijiti. Mimi hoja yangu sio nani alijenga plant. Hoja ni kudhibiti hujuma zilizosababisha kuwepo mgao wa umeme naomba uelewe. Hata JNHPP ilibuniwa wakati wa Mwl Nyerere lakini amekuja kujenga JPM. Labda unajibu hoja kwa kuangalia heading tu.
Na anae kufundisha kuandika anakudanganya. Mikoa ambayo haikuwa kwenye grid ya taifa ni michache sana ambayo ilikuwa inatumia jenereta. Haiwezi kufikisha megawati 796+.
Mimi nilikuwa nazungumzia uzalishaji wa umeme kabla ya Songas na Kinyerezi projects. Na hapo kulikuwa na uwezo wa kupata megawatss zaidi ya 800. Ila kuna mafisadi walifanya hujuma na leo wamezibitiwa.
 
Kuanzia mwaka 2006 mpaka rais magufuli anaingia madarakani nchi yetu ilikuwa mara kwa mara ikikumbwa na tatizo kubwa la mgao wa umeme. Tatizo ambalo kwa muda mrefu lilikuwa mwiba kwa taifa letu. Vinyozi,wenye saluni za kike, wenye mabaa mpaka wenye viwanda lilikuwa ni tatizo linalowaumiza.

Ulipoingia madarakani ulisema hili tatizo litakuwa kweli mwisho. Na kwa hakika sasa tumesahau. Maana kama umeme ukikatika ujue kuna hitilafu na matengenezo. Lakini sio mgao wa umeme eti kwa sababu umeme hautoshelezi.

Swali ambalo mimi nimejiuliza kichwani kwangu je kwa nini kipindi hicho kulikuwa na mgao wa umeme wa karibu siku tatu au wiki kwa baadhi ya mikoa ? Je ilikuwa ni dili za wauza jenereta? Na wewe ulipoingia ukazibana na sasa umeme unapatikana masaa 24!

Je zilikuwa deal za wajanja wachache kama akina Harbinder Seth na wenzake ili waweze kupata tenda za kuizuia umeme Tanesco na kisha kulipwa malipo ya capacity charges yanayoiumiza Tanesco. Ila wewe ulipoingia ukavunja na mkataba wa Tegeta Escrow.

Au ndio zilikuwa hujuma za watumishi wa Tanesco kwenye hydropower stations ambao walishirikiana na mafisadi ili kufungulia maji yapungue kwenye mabwawa ili umeme usizalishwe kama inavyohitajika. Ila wewe ulilishutukia hili na kuwatimua. Sasa mgao wa umeme sio hadithi tena.

Je, kama hali iko hivi Je JNHPP ikikamilika mambo yatakuwaje?

Jambo linalosikitisha pamoja na mambo mazuri unayoyafanya wafuasi wa Chadema na wanachama wao hawana uzalendo na kukushukuru kwa namna ulivyojitoa ili Tanzania iliyokuwa imepinda inyooke.

Ila nakupa pongezi kwa hili na kwa mantiki hii kura za urais Mungu akipenda utapata 99.5%.
Ndugu unaishi nchi gani hiyo isiyokuwa na mgao wa umeme. Wewe haata bunge husikilizi, hujasikia juzi mbunge mmoja akimwambia Waziri Kalemani aende Mtwara kimyakimya atampangishia gesti akae kwa siku tatu aone jinsi umeme unavyokatikakatika?. Huku kwetu toka ameingia Magufuli mgao umeongezeka mara 100. Yaani umeme unakatika sana mara kwa mara na hata wagonjwa wanafariki sana kwa kukosekana umeme. Hadi tunamkumbuka Kikwete. Kweli nchi hii si moja, watu wake si wamoja, uzoefu wao ni tofauti sana
 
Hapa nilipo umeme hakuna tokea asubuhi gongolamboto Mombasa majohe pugu yote kisarawe mpaka chanika inakuaje we we mpambe nukusi
 
Back
Top Bottom