Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Alitumbuliwa Marehemu Mwele Malechela kwa kusimamia tu profession yake ikapelekea kutumbuliwa eti ateseke
Akatumbuliwa Rawrence Mafuru kwa kusema tu serikali kujiondoa kwenye mfumo wa benki binafsi kungeweka sekta ya fedha matatani. Ingawa aliondolewa Ila maneno yake yalitimia. Kwa miaka 3, 2016-2018 sekta ya mabenki ilitikisika sana.
Alitumbuliwa Mataragio wa TPDC kwa maneno tu ili Serikali ijiondoe kwenye sekta ya Gesi. Miradi mingi ikasimama kumbe tungewekeza kipindi kile leo tungekuwa tunaenda kuuza Gesi nje na kupata faida nyingi. Baadae akarudishwa na sekta ya Gesi ikawekwa kapuni.
Alitumbuliwa Nehemia Mchechu aliyekuwa na rekodi Nzuri ya utendaji kwenye sekta ya mabenki, akachafuliwa bila hata kupelekwa mahakamani kwa chuki tu kutokana na kuwa fundraiser mzuri wa kanisa la KKKT lililokuwa tofauti sana na mtawala yule.
Alitumbuliwa dada wa watu Kairuki pale NIC aliyekuwa akifanya vizuri kwenye uwekezaji kisa tu anaongea kiingereza na hakijui kiswahili kuvile matokeo yake uwekezaji ukashuka sana.
Akatumbuliwa Dk Ramadhani Dau kisa tu anaipenda dini yake na ameweka mpaka sehemu ya kuswali ofisini kwake jambo ambalo halina shida. Matokeo yake NSSF ikaanguka na sasa haieleweki imesimama au inakwenda!
Akatumbuliwa CAG Assad kisa tu naye anaipenda dini yake! Akadhalilishwa hadi kuitwa bungeni na puppet wa yule jamaa.
Akatumbuliwa DAS mmoja Kisarawe pale, kisa tu taarifa zilimfikia mzee kuwa anakula chakula ya Mzee aliyeiweka pale Kisarawe kimkakati.
Walipigwa risasi kina Lissu, walifungwa kina Sugu. Walishtakiwa kina Mchungaji msigwa na wakauwawa kina Ben Saanane.
Asante Samia maana naona unaliponya Taifa dhidi ya siasa hizi za chuki na roho mbaya!
Natarajia kuwaona Big Brains Charles Kimei, Ramadhani Dau wakiendesha taasis nyeti hivi Karibuni wakishirikiana na Big brains Wengine Kama Prof Luoga, Nehemia Kyando Mchechu katika kupeleka uchumi wetu mbele zaidi kwa kasi Kubwa na kutengeneza ajira nyingi na maisha mazuri kwa Watanzania.