Hongera Rais Samia kwa kuliponya Taifa dhidi ya siasa za chuki na roho mbaya

Hakuna roho mbaya iliyo kubwa kuliko kuhamasisha ufisadi katika Taifa.

Hakuna siasa za chuki kwa wananchi zilizo mbaya kuliko kuhamasisha ufisadi katika Taifa.

Samia ni fisadi anaehamasisha ufisadi katika Taifa,anapaswa kulaaniwa na kukataliwa na kila mwenye pumzi.
View attachment 2151190
Hahaaaa unaumia nini? Ndugu
1)Hela zenyewe tumepewa kwa masharti nafuu haijawahi tokea tangu tupate uhuru hata zikiliwa kuna shida gani? Tushafanya mambo mengi kwa muda mfupi na tutamaliza kero kabla ya 2025
2)Rasimali kama madini na vinginevyo hata vikibebwa wewe unaumia nini hata wanyama tu hawawezi kula wewe unaving'ang'ania vya nini?
Huu si ufisadi watu wale kutokana na urefu wa kamba zao ila tu wasivimbiwe
 
Alipigwa Mipasho Ndugai baada ya Kusema ambayo wengine hawakutaka kuyasikia...

Aliwekwa kando Lukuvi kwa kupewa kazi maalumu

Wengine walitupwa Malawi kwa kusema ndivyo sivyo...

Same Script, Different Cast....
 
Hahaaaa unaumia nini? Ndugu
1)Hela zenyewe tumepewa kwa masharti nafuu haijawahi tokea tangu tupate uhuru hata zikiliwa kuna shida gani? Tushafanya mambo mengi kwa muda mfupi na tutamaliza kero kabla ya 2025
2)Rasimali kama madini na vinginevyo hata vikibebwa wewe unaumia nini hata wanyama tu hawawezi kula wewe unaving'ang'ania vya nini?
Huu si ufisadi watu wale kutokana na urefu wa kamba zao ila tu wasivimbiwe
Ila waTz bwana, hizi akili za kijinga huwa mnazitoa wapi?
 
Mkifikia hatua ya Katiba Mpya unishtue
Alitumbuliwa Marehemu Mwele Malechela kwa kusimamia tu profession yake ikapelekea kutumbuliwa eti ateseke

Akatumbuliwa Rawrence Mafuru kwa kusema tu serikali kujiondoa kwenye mfumo wa benki binafsi kungeweka sekta ya fedha matatani. Ingawa aliondolewa Ila maneno yake yalitimia. Kwa miaka 3, 2016-2018 sekta ya mabenki ilitikisika sana.

Alitumbuliwa Mataragio wa TPDC kwa maneno tu ili Serikali ijiondoe kwenye sekta ya Gesi. Miradi mingi ikasimama kumbe tungewekeza kipindi kile leo tungekuwa tunaenda kuuza Gesi nje na kupata faida nyingi. Baadae akarudishwa na sekta ya Gesi ikawekwa kapuni.

Alitumbuliwa Nehemia Mchechu aliyekuwa na rekodi Nzuri ya utendaji kwenye sekta ya mabenki, akachafuliwa bila hata kupelekwa mahakamani kwa chuki tu kutokana na kuwa fundraiser mzuri wa kanisa la KKKT lililokuwa tofauti sana na mtawala yule.

Alitumbuliwa dada wa watu Kairuki pale NIC aliyekuwa akifanya vizuri kwenye uwekezaji kisa tu anaongea kiingereza na hakijui kiswahili kuvile matokeo yake uwekezaji ukashuka sana.

Akatumbuliwa Dk Ramadhani Dau kisa tu anaipenda dini yake na ameweka mpaka sehemu ya kuswali ofisini kwake jambo ambalo halina shida. Matokeo yake NSSF ikaanguka na sasa haieleweki imesimama au inakwenda!

Akatumbuliwa CAG Assad kisa tu naye anaipenda dini yake! Akadhalilishwa hadi kuitwa bungeni na puppet wa yule jamaa.

Akatumbuliwa DAS mmoja Kisarawe pale, kisa tu taarifa zilimfikia mzee kuwa anakula chakula ya Mzee aliyeiweka pale Kisarawe kimkakati.

Walipigwa risasi kina Lissu, walifungwa kina Sugu. Walishtakiwa kina Mchungaji msigwa na wakauwawa kina Ben Saanane.

Asante Samia maana naona unaliponya Taifa dhidi ya siasa hizi za chuki na roho mbaya!

Natarajia kuwaona Big Brains Charles Kimei, Ramadhani Dau wakiendesha taasis nyeti hivi Karibuni wakishirikiana na Big brains Wengine Kama Prof Luoga, Nehemia Kyando Mchechu katika kupeleka uchumi wetu mbele zaidi kwa kasi Kubwa na kutengeneza ajira nyingi na maisha mazuri kwa Watanzania.
 
Hivi hapa nani ni big brain ni hawa uliowaorodhesha hapa au ni aliewateua?

Nchi zetu siasa zitatuponza sana

Nadhani hapa ilitakiwa kusema hongera Big Brain Madam (BBM) kwa kuwachagua hawa
Nchi haiendeshwi na big brain mmoja isipokuwa kama ni Mungu.
 
Alitumbuliwa Marehemu Mwele Malechela kwa kusimamia tu profession yake ikapelekea kutumbuliwa eti ateseke

Akatumbuliwa Rawrence Mafuru kwa kusema tu serikali kujiondoa kwenye mfumo wa benki binafsi kungeweka sekta ya fedha matatani. Ingawa aliondolewa Ila maneno yake yalitimia. Kwa miaka 3, 2016-2018 sekta ya mabenki ilitikisika sana.

Alitumbuliwa Mataragio wa TPDC kwa maneno tu ili Serikali ijiondoe kwenye sekta ya Gesi. Miradi mingi ikasimama kumbe tungewekeza kipindi kile leo tungekuwa tunaenda kuuza Gesi nje na kupata faida nyingi. Baadae akarudishwa na sekta ya Gesi ikawekwa kapuni.

Alitumbuliwa Nehemia Mchechu aliyekuwa na rekodi Nzuri ya utendaji kwenye sekta ya mabenki, akachafuliwa bila hata kupelekwa mahakamani kwa chuki tu kutokana na kuwa fundraiser mzuri wa kanisa la KKKT lililokuwa tofauti sana na mtawala yule.

Alitumbuliwa dada wa watu Kairuki pale NIC aliyekuwa akifanya vizuri kwenye uwekezaji kisa tu anaongea kiingereza na hakijui kiswahili kuvile matokeo yake uwekezaji ukashuka sana.

Akatumbuliwa Dk Ramadhani Dau kisa tu anaipenda dini yake na ameweka mpaka sehemu ya kuswali ofisini kwake jambo ambalo halina shida. Matokeo yake NSSF ikaanguka na sasa haieleweki imesimama au inakwenda!

Akatumbuliwa CAG Assad kisa tu naye anaipenda dini yake! Akadhalilishwa hadi kuitwa bungeni na puppet wa yule jamaa.

Akatumbuliwa DAS mmoja Kisarawe pale, kisa tu taarifa zilimfikia mzee kuwa anakula chakula ya Mzee aliyeiweka pale Kisarawe kimkakati.

Walipigwa risasi kina Lissu, walifungwa kina Sugu. Walishtakiwa kina Mchungaji msigwa na wakauwawa kina Ben Saanane.

Asante Samia maana naona unaliponya Taifa dhidi ya siasa hizi za chuki na roho mbaya!

Natarajia kuwaona Big Brains Charles Kimei, Ramadhani Dau wakiendesha taasis nyeti hivi Karibuni wakishirikiana na Big brains Wengine Kama Prof Luoga, Nehemia Kyando Mchechu katika kupeleka uchumi wetu mbele zaidi kwa kasi Kubwa na kutengeneza ajira nyingi na maisha mazuri kwa Watanzania.
Bado na wewe kutumbuliwa. Huna mazuri yeyote na Mtanzania yeyote Kafiri tu ww
 
Wafuasi wa Magufuli wamefura kwa hasira...

Wanatamani siasa za kikabila na roho mbaya za kuuana, kufungana, kujitenga na dunia kama Wahutu, Tanzania iwe kama Burundi sijui ni kweli mungu wao alikuwa na asili ya huko
Wamechukia sana
 
Hivi huyo mchechu unamjua vizuri kweli na hasara aliyosababisha kipindi chake?
 
Back
Top Bottom