Hongera sana homeboy kwa kumleta Flora (Mbasha) Henry nyumbani

Hongera sana homeboy kwa kumleta Flora (Mbasha) Henry nyumbani

Status
Not open for further replies.
Hii itakuwa ndoa ambayo itafungishwa na mkuu wa wilaya/mkoa au ni yake kimila, ndoa ya kanisani ni mara moja tu ktk maisha ya mkristo. Kwa uelewa wangu,sijui km mke/mme akifariki sheria za dini ya kikristo huwa zinasemaje.
Ngoja wataalamu waje watudadavulie... Anyway, hongereni kwa hatua nzuri mliyofikia maharusi watarajiwa.
Za kanisani huvunjwa kwa Uzinzi.
 
Safi sana kaka. Umesema lililo moyoni mwangu. Kijana namfahamu sana na katulia
Anaoa mke wa mtu lakin,
Mme wake ameteseka sana na huyu mwanamke, na isitoshe alikaribia kupotezwa kwa sbb ya huyu huyu mwanamke.
Kuzaa na mke wa mtu ni issue ambayo sio nyepesi, ki imani ni tatizo litakalosumbua katika familia yako kizazi mpaka kizazi.

Mmeshindwa kumshauri kuwa huyo mwanamke hawezi kudumu naye, kuwa anajitafutia laana.

Mungu atupe uzima ili tuweze kujifunza kupitia ndoa hii. Hii ndoa ikifanikiwa, litakuwa funzo kubwa kwa imani zetu, na ikifeli pia Itakuwa shule tosha kwetu sote.
 
Huna sababu ya kuwapongeza, wape pole maana moto hakika na wao. Hawawezi kuuepuka. Kuwa mkristo siyo jambo la kisipoti sipoti aisee.

Na kama Mbasha Emanuel anahamasisha ndoa badala ya kukemea jambo hili, naye moto ni halali yake.

Anyway, walete ushahidi wa maandiko.

Someni hapa kuhusu ndoa

11639145b26d759b3ac743c6675d3cba.jpg

4526e56724d94bc0d297568b83bb1fd7.jpg

Malizia na injili, maana wengine huwa hawaamini agano la kale

70de392e1e79eba6b422a3975df8d1d8.jpg
USIHUKUMU NA WE USIJE HUKUMIWA HUO MOTO HAUKUHUSU HIYO NI KAZI YA MUNGU MWENYEWE NGO ANAJUA
 
OK kumbe wote wanao omba michago hawana hela? Tuambie ni mwanasiasa yupi unaowafahamu wako vizuri financially hawakuchagiwa. Yes kijana ni mtu wa kijijini kwetu na ni mtu bright kiakili. Pesa inatafutwa na maisha hayana formula

Mwenye Pesa haombi mchango mkuu. Nani kakwambia wabunge wana hela?? Au sio hawa wakipigwa chini wanafulia mbaya?? Mkuu usione mtu anaendesha range ukadhani anahela, aaah wapi, wana hela ya kubadili mboga tu, ila Hawana PESA. Mkuu muonekano wa mtu usikudatishe.
 
Leta maandiko wacha upoyoyo. Nyie watu wa kolomije mna shida sana
Kolomije ndio wanaongoza nchi bado miaka 9 mbele, nimekujibu hivyo japo si muumini wa ukabila na ukanda lkn kwa watu wapuuzi kama wewe muda mwingine ukionyesha ustaarabu unaonekana dhaifu.
 
Hii itakuwa ndoa ambayo itafungishwa na mkuu wa wilaya/mkoa au ni yake kimila, ndoa ya kanisani ni mara moja tu ktk maisha ya mkristo. Kwa uelewa wangu,sijui km mke/mme akifariki sheria za dini ya kikristo huwa zinasemaje.
Ngoja wataalamu waje watudadavulie... Anyway, hongereni kwa hatua nzuri mliyofikia maharusi watarajiwa.
kama ndoa za mashoga mnaozesha mtashindwa hzo?
 
Hivi taratibu za dini ya kikristo zikoje juu ya hili???..Unaweza kumuacha mke wako wa ndoa na kuoa mwanamke mwingine?
Kwani hapo nani amemuacha mke wake akaoa mwingine?
 
Hivi taratibu za dini ya kikristo zikoje juu ya hili???..Unaweza kumuacha mke wako wa ndoa na kuoa mwanamke mwingine?
Ktk dini ya kikristo haiwezekani mpaka kifo kitakapo watenganisha. Pia kama hapakuwepo (hapakufanyika) na tendo la ndoa kati ya wana ndoa hao.
 
Ktk dini ya kikristo haiwezekani mpaka kifo kitakapo watenganisha. Pia kama hapakuwepo (hapakufanyika) na tendo la ndoa kati ya wana ndoa hao.
hivi mnavoshabikia hizo sheria za kanisa kwani zilitoka mbinguni? Mungu mwenyewe alivompa Musa sheria aliweka ya kuachana hata Yesu mwenyewe aliruhusu kuachana kwa uzinzi. hizo sheria za kanisa hazina mashiko zimewekwa na watu tu.
 
Soma biblia vizuri na uielewe.Mnapooana mnakuwa mwili mmoja na watu wawili. Sasa mwili mmoja unatengana vipi?! kilichofungwa hapa duniani na mbinguni kimefungwa pia.
 
Huwa sielewi katika wanawake wooote hawa waliojaa na wanatafuta waume wa kuwaowa hivi mtu hajaona mwanamke wa kuishi naye mpaka uchukuwe mke wa mtu?

Karma is really.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom