Hongera sana, kama Ally Kamwe angechomwa sindano tu leo tusingekuwa naye

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Tukio la Ally Kamwe kuzimia limekuwa tukio la kusisimua sana kutokana na mkasa wenyewe kuwa mzito na kuepushwa matokeo ambayo yangekuwa ya huzuni.

Ally Kamwe alibeba vitu vizito siku ile. Kabla ya match alikuwa akihangaika sana na wazee ambao tunashukuru Ally Kamwe aliamua kujitoa mhanga tofauti na yule dogo Privadinho ambaye aliendekeza ubitozi sana.

Alipoelemewa na kuzimia haraka alikimbizwa hospitali, Mzee "Matata" alikuwa mmoja ya waliomsindikiza Hospital. Walipomchukua kumpeleka chumba cha wagonjwa wa haraka wa dharura. Mzee alisema "Msimchome sindano mwacheni apumzike" akawataka wauguzi watoke.

Ndipo akamtoa mizigo aliyokuwa amebebeshwa na hapo akarudiwa na fahamu na nguvu. Akawa mzima kabisa.

Hii ni pongezi kwake kwa kujitoa mhanga kipindi ambacho pengine wengi wangeingiwa woga. Wanayanga tunapaswa kumheshimu sana Ally Kamwe.
 
Kajamaa sijui walikabebesha majini mangapi dadadeki...
 
ni vitu gan hivyo vizito na alivibebea wapi akinani walimpa na kwa ajili ya nini
 
Kwahiyo bila huyo Mzee, Semaji la Vyura angeendelea kupoteza fahamu?

Watu wanajua kuji-risk maisha, itabidi wafanye mpango wamuongezee mshahara 😜🙌

Kuna mwaka nimesahau kidogo (wahenga wataweka tarakimu), kuna kipa alifia uwanjani kwa kuchanwa shingoni kwenye mshipa mkubwa...(nadhani ilikuwa Tanga ile)

Alikuwa kabeba mikoba na wakulungwa wakawa wanataka kafara lao, timu sijui haikutoa damu huko kwa wakulungwa...
 
Naskia kwanza walitaka wamwekee dripu.
Mzee akagoma kama kawaida

Ally Kamwe Yuko tayari kupoteza maisha kwa ajiri ya Yanga yake.

Ila huyo mnaye mwita Privadinyo hakubali ng'o.
Yupo kidigitali zaidi.
Ila Ally akiendelea na huo mchezo tutakuja kumpoteza mazima muda si mrefu.
 
Kuna mwaka nimesahau kidogo (wahenga wataweka tarakimu), kuna kipa alifia uwanjani kwa kuchanwa shingoni kwenye mshipa mkubwa...(nadhani ilikuwa Tanga ile)

Alikuwa kabeba mikoba na wakulungwa wakawa wanataka kafara lao, timu sijui haikutoa damu huko kwa wakulungwa...
Hiyo hatari Mkuu, na ukiwa mbeba mikoba ukihama timu unaweza hata kupotezwa kabisa yaani 🙌
 
Kwahy Ally Kamwe ni mtetezi wa wanyonge 😂
 
Back
Top Bottom