Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Ni bora asingejibu tuu kama Majaliwa Jana. Maana majibu yake yameonyesha katiba anaisoma lakini haielewi.
Hajui hata ukomo wa madaraka yake, hapo ndio kauli ya Lema inapopata mashiko.
Lema ni kweli ana maono
 
Mie mwananchi wa kawaida hio katiba yenu itanisaidia kuingiza hela mfukoni?. Nimeangalia masikini wenzangu wa kenya baada ya kupata hio katiba mpya bado hawajawa matajiri.

Sasa maswali mwengine hayana tija...yanafurahisha wanasiasa tu
 
Hivi wakina Mbwambo na Karugendo walikuwepo au hawakuhudhulia? Hawa ndio naamini ni watu wanaoweza kushusha nondo bila woga!!!
 
Mbona Hakujibu la Kuzuia Mikutano Ila yakweke Peke yake? Au Pia yeye Ndiye Mtoa Fedha Kwa Mikutano ya Vyama vya siasa? Je Kubana Matumizi Pia Kunazingatia Badget ya Kumlinda Lipumba? MAGUFULI NI MNAFIKI FULANI HIVI!
 
Ni kweli ingawaje swali lake halikujibiwa kabisa..eti mayalla kwa kisukuma ni njaa,inahusiana vip na swali husika?or this is Mugabe of Tanzania …?
 
HIVI ANALIPA BUNGE NA MAHAKAMA HELA NANI?
 
Najua wengi hawatamtaja SAMI kutokana na kwamba aliuliza kwa KIDHUNGU na mkulu naye ili w/nchi wengi wasielewe alichokua anauliza akadakia usitafsiri kwa Kiswahili nimeshaelewa.Ila ndio MAN of THE MATCH ingekua ni SOKA
 
WanaJf wawili wameuliza Pascal na Manyerere but Pascal alikuwa smart na amejibiwa vizuri swali la mihimili mitatu!
JPM kalijibu swali la Pasco vizuri kwa kumuuliza ni kwa nini alialikwa Bungeni na kutoa hotuba yake ya kwanza pale mbele. Hapo ndipo linapoingia suala la head of state.
 
Ama kweli kipendacho moyo hula nyama mbichi! Hivi ni kweli kuwa Pascal Mayalla, ndio Mwandishi Pekee aliyemuuliza Rais? Mimi nimeona tofauti kabisa, Mayalla ameshindwa hata kuyapanga maswali yake kipaumbele kiasi cha kuto mwanya muulizwa maswali pakutokea na hivyo kukwepa hata kujibu swali lake kikamilifu.

Kwa mtazamo wangu mimi,mwandishi wa BBC ndie aliuliza swali mwafaka kwa maudhui ya mkutano huo na kwa Tido kuchomokea swali la mkato,kali na kwenye kidoto ambalo wazi limeonekana kuwa mwiba na hata kuweza kumtoa kwa muda kwenye mstari.

Inapotokea mdahaliwa akauteka mdahalo,inaonyesha wazi udhaifu na ukame wa waandishi wenye weledi Tanzania.

Sijui umeandaliwa vipi lakini nilitamani kuwaona waandishi wabobezi kama akina Ali Saleh(Azam Director&former BBC Manager),Deodatus Balile,Jabir Issa n.k.

Kukosekana kwa waandishi wa aina hiyo,imekuwa wengi wao walikwenda kuitikia mwaliko wa chakula cha mchana kusheherekea mwaka mmoja tokea Mdahiliwa kuingia Ikulu.
 
Bora hao waandishi/watangazaji uchwara wote wangeondolewa na kuachwa Pasco tu ambaye angeuliza maswali ambayo Watanzania wengi tungependa kuyasikia yakiulizwa. Hongera Pasco omba 90 minutes za uso kwa uso nyie wawili tu lakini wakishaona humu JF tunakusifia sana watakuingiza kwenye kundi la adui yao.
 
Sijaona swali alilojibu inavyotakiwa,kila swali anapindisha maelezo sidhani kama kuna mwandishi aliyeridhika kwa majibu yake,mfano alipoulizwa dawa za watoto hospitalini mbona wanakufa kwa nimonia akaanza kujibu billions za kwenye bajeti ya wizara ya afya tena kwa kujigamba zimeongezeka,so kumbe hela zipo kwanini sasa dawa hakuna mahospitalini?!


Yule wa bbc kamuuliza kwanini anadhoofisha demokrasia akajibu tofauti,kama haelewi alichofanya juu ya uhuru wa habari,kuzuia mikutano ya kisiasa,ilibidi nizime tu tv.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…