Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Tido ni mzoefu alishaona kuwa JPM angepata shida sana kulijibu hilo swali la pili la Pasco na ndio maana akaingilia kati na kulipotezea!!
Hapo ndipo paliponikera mimi na pia nadhani na wenzangu wengi sana! Kama ni kutoa tuzo ya aliyeuliza maswali bora Pascal Mayalla angeibuka mshindi akifuatiwa na Sammy wa BBC
 
Pasco ni mtu makini sana, hana unafki wala woga na ndio maana ameamua kuwa private journalist. Pasco amemzidi viwango huyo Tiddo aliuliza maswali kama mwanafunzi wa journalism ngazi ya cheti.

Mkuu Pascal Mayalla wewe ni mfano wa kuigwa kwa wanahabari, hakika hata Nape atakukimbia siku akijua upo kwenye mkutano wake na wanahabari.
 
Leo tumewakilishwa vilivyo na members wawili pale magogoni.Aina ya maswali waliyouliza yanathibisha tofauti kubwa ya uwezo wa kufikiri na kutumia fursa.Wakati Pascal anaulizia matumizi ya katiba Jacton yeye anaulizia kula na kunywa kweli Jf ni mchanganyiko wa fikra.Bravo pasco kwa kuitambua Jf mbele ya Rais na kuitendea haki kimaudhui.Mods tafadhali msiunganishe huu uzi
 
Nimemsikia Pasco Mayalla akiuliza swali kwamba Rais amepata wapi mamlaka ya kuwaambia Wabunge (legislature) na Mahakama (Judiciary) waombe ruhusa kwake watakapo kusafiri?

Hoja ya Pasco ni kwamba kuna separation of powers yaani Executive, Judiciary na Legislature ambazo zinatakiwa zifanye kazi bila kuingiliana. Hilo ni sawa ila Pasco kweli hafahamu kwamba Rais wa Jamhuri ni mkuu wa dola na chini ya dola ndio unapata executive arm, judiciary arm na legisleture?

Hajui kwamba Rais wa Jamhuri ni Head of Government na wakati huohuo ni Head of the State?
Na wewe umeruka swali la pili la kifungu kinachozuia MIKUTANO YA KISIASA
 
Back
Top Bottom