Kwa ujumla ni namna tu ya kujionyesha kuwa Pascal anajiamini lakini wakati mwingine ni ukosefu wa kufikiri kwa kina.Rais ndiye kiongozi wa nchi anayetambulikana na wote.Mwenye mamlaka.Hiyo mihimili mingine ipo kweli lakini kwenye karatasi.Sisi wananchi tunamjua Rais ,mambo ya bunge na mahakama ni baadaye.Rais ana uwezo,ana mamlaka hata ya kunyonga.Anaweza vilevile kuacha kutia saini ya kunyongwa kwa aliyehukumiwa na mahakama ya juu. Kumuuliza rais uwezo kaupata wapi ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu na ukosefu wa adabu vilevile.