Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Kwa ujumla ni namna tu ya kujionyesha kuwa Pascal anajiamini lakini wakati mwingine ni ukosefu wa kufikiri kwa kina.Rais ndiye kiongozi wa nchi anayetambulikana na wote.Mwenye mamlaka.Hiyo mihimili mingine ipo kweli lakini kwenye karatasi.Sisi wananchi tunamjua Rais ,mambo ya bunge na mahakama ni baadaye.Rais ana uwezo,ana mamlaka hata ya kunyonga.Anaweza vilevile kuacha kutia saini ya kunyongwa kwa aliyehukumiwa na mahakama ya juu. Kumuuliza rais uwezo kaupata wapi ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu na ukosefu wa adabu vilevile.
Lakini Rais si mfalme na wala si Waziri Mkuu ambae ndie kiongozi wa serikali kikatiba
 
Jambo lingine kalisema katika utangulizi kuonyesha hajikombi wala hana njaa (kama jina lake lilivyotafsiriwa, ingawa majina hayatafsiriwi kwani yeye la kati tukimwita Wanzuki au kangara atafurahi?) Ni pale aliposema waandishi binafsi wapate mialiko ya ziara za nje na wanaweza kujilipia.
Hiyo ni kuonyesha hana njaa na hategemei fadhila.
Hata msosi wao wakimnyima waweza kuta msukuma huyu kwenye mkoba wake kajibebea viazi vyake vya kuchemsha yaani manumbu (joke)
 
Nampongeza sana sana pascal mayala ndiye pekee aliyejua kilochompeleka pale
Wengine naona hawakuwa wamejiandaa kwa chochote.
 
mayala kauliza swali lenye akili sana...
kuna pambaff mmoja aliuliza eti mheshimiwa wakati unapokuwa nje ya ofisi unapendelea nini..?
akajibiwa ulitaka nikupende wewe.., ha ha..
 
Pasco, yule wa BBC, Tido na Bakari wa Mwananchi waliuliza maswali bila uoga.

Ryoba mpaka aibu. Sijui kwa vile anafanya kazi TBC?
 
Back
Top Bottom