Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Nakubaliana nawe 100%. Dhana ya separation of power haielewi kabisa

Sheria anazotumia Rais zimetungwa na Bunge, na zinatafsiriwa na Mahakama ili zitumike na serikali. Huu ni mfano wa utatu huo. Dhana kwamba mhimili wa serikali ndio mkubwa ni mpya kabisa na inaondoa maana ya separation of powers kabisa

Separation of powers haina maana mwenye 'mpini' katika eneo moja ndiye mkubwa

Kwa kweli hili nimesikitika
 
Hajajibu hilo swali. Hajaeleza nini maana ya separation of power. Au anataka kusema hata pamoja na kuwepo kwa separation of power bado rais anakuwa na mamlaka makubwa kuliko vyombo vingine?
Hana mamlaka hayo yeye amejitwalia tu,hayo ni matumizi mabaya ya madaraka yaliyopitiliza.-period.
 
Bado huamini kwamba Rais anapokuwa mkuu wa dola ni mkubwa kuliko wengine? Nadhani tunahitaji elimu kujua tofauti ya Head of Government na Head of State. Kwa hiyo unataka kumlinganisha Rais na Jaji Mkuu? Hawalingani mzeee
 
Ni mpaka pale tu mwanasheria mkuu kupitia wizara ya sheria atakapo peleka muswada bungeni kumpa raisi mamlaka hayo vinginevyo ataendelea kukaa kimya na kubariki uvunjifu wa sheria.
 
kwa jinsi alivyo jibu ni dhahiri kwamba Mh. rais anatumia madhaifu ya katiba yetu inayompa mamlaka makubwa kufanya chochote wakati wowote so kwa nn hataki katiba mpya tena ya warioba!?
Akikubali Katrina mpya maana yake anajibana yeye kitu ambacho yeye na chama chake ccm hawataki kusikia kabisa , na kama tunataka katiba mpya lazima sisi kama taifa tumwage mboga zao na ugali kwanza ili wakubaliane na matakwa ya dai la katiba mpya. Lasivyo tutaishia kupiga Keller na kubakia na taifa lisilo na dira bora. Amueni kumwaga mboga zao na ugali ili nao waonje njaa tunayopitia inayotokana na maamlaka ya katiba waliyo nayo. Amueni moja tuuu nalo ni kuitaa katiba hii istumike katika uchaguzi mwaka 2020 , watupe tume huru ya uchaguzi.
 
KUMBE RAISI ANALIDHIBITI HATA BUNGE, SASA LINAISIMAMIAJE SERIKALI WAKATI LIKO CHINI YA RAISI.
Hujui kwamba Bunge linaweza kutunga sheria na Rais akakataa kuisaini? Hujui kwamba kwa mujibu wa Katiba Rais anaweza kutoa msamaha wa hukumu yoyote iliyotolewa na mahakama?
 
Mimi nilifikiri kauliza swali la maendeleo ya nchi, kumbe safari za nje za wabunge.inatusaidia nini sisi???
Halafu ameuliza kama si mwanasheria. Rais anateua majaji, Rais anasaini miswada ya bunge kuwa sheria.
 
UMEANDIKA KWA JAZIBA PAMOJA NA YOTE ULIYOSEMA BADO NI MTAWALA (EXECUTIVE) NDIYE ANAYEPELEKA HICHO BUNGE ILICHOPANGA NA HATA BUNDE ILICHOPANGA KINATOKANA NA MUSWADA WA BAJETI INAYOPENDEKEZWA NA WATAWALA. USHAURI WANGU ACHA UANAHARAKATI HII MIHIMILI MITATU HAIKO SAWA HATA KIDOGO.
 
Huyu jamaa kauliza swali la msingi sana, na kwa kiongozi mwenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo angelijibu kwa ufasaha, nakiri kuwa nimekuwa na kichwa kigumu kuamini kama tutakua na maendeleo katika awamu hii, mkuu hapendwi kuudhiwa ila anashindwa namna ya kufanya watu wasimuudhi, kingine kinachonifanya nisiwe na imani sana na serikali ya awamu hii, ni namna inavyoonesha chuki za wazi kwa upande unaowapinga, wanatumia nguvu ya madaraka badala ya hoja.
 
Swali la Pascal halikuwa na mashiko ndio maana Rais naye kalijibu kwa swali. Rais ndiye anazindua Bunge, Rais anasaini miswada kuwa Sheria, Rais anateua majaji, Rais anaweza kufuta hukumu ya mahakama yoyote.
 
Hongera P Mayalla na jamiiforums kwa ujumla kuwa na Tankthinkers wazuri isipokuwa wachache wa buku sabaza za Lumumba
 
Vizur sana mayalla japo kakujibu vijanjajanja umekuna penyewe
 
Wauliza maswali wengi wao walikuwa kkkundi cha wahuni wachache walioandaliwa kuuliza maswali ya kusinzia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…