Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

..inaelekea jpm haelewi dhana ya separation of powers ya hii mihimili mitatu.

..yes, serikali ndiyo yenye vyanzo vya fedha. Lakini serikali haiwezi kutumia fedha hizo bila bajeti kupitishwa na BUNGE.

..Vilevile bunge linatunga sheria. Lakini mhimili wa MAHAKAMA ndiyo unaotafsiri sheria hizo na kutoa haki kwa wananchi.

..matatizo mengine yanatokea kwa kutokuelewa taratibu za kikatiba na kisheria. Kwa hili tunapaswa kumuombea.

Cc Pasco, Nguruvi3
Nakubaliana nawe 100%. Dhana ya separation of power haielewi kabisa

Sheria anazotumia Rais zimetungwa na Bunge, na zinatafsiriwa na Mahakama ili zitumike na serikali. Huu ni mfano wa utatu huo. Dhana kwamba mhimili wa serikali ndio mkubwa ni mpya kabisa na inaondoa maana ya separation of powers kabisa

Separation of powers haina maana mwenye 'mpini' katika eneo moja ndiye mkubwa

Kwa kweli hili nimesikitika
 
Hajajibu hilo swali. Hajaeleza nini maana ya separation of power. Au anataka kusema hata pamoja na kuwepo kwa separation of power bado rais anakuwa na mamlaka makubwa kuliko vyombo vingine?
Hana mamlaka hayo yeye amejitwalia tu,hayo ni matumizi mabaya ya madaraka yaliyopitiliza.-period.
 
TETESI: SAMMY AWANI NA PASCAL MAYALLA MARUFUKU IKULU.

Pascal kwanza nikupongeze kwa kujenga swali lako vizuri sana
Majibu ya Rais kuhusu swali lako yanazua utata mwingine mkubwa. Kuna nyakati serikali inasema mihimili mitatu haiingiliani kiutendaji. Rais anasema mhimili wa serikali ni mkubwa Zaidi
Hili ni tatizo kubwa sana, hakuna mhimili mkubwa katika hiyo mitatu kwa wenzetu walioanzisha system hiyo. Rais anaposema mhimili wake ni mkubwa, tayari ameshakiuka 'separation of power'
Hakujibu swali na alipojaribu aliharibu Zaidi.


Sammy na wewe nikupongeze kwa kujenga swali lako vizuri sana..
Sammy awani " watu wengi wanahisi anakandamiza demokrasia ya nchi"
Majibu ya Rais kuhusu swali lako yanazua utata mwingine mkubwa.

Kwa maswali hayo nazani kuitwa tena ikulu msahau..

Maswali magumu, majibu mepesi.


Hapa kazi tu
Bado huamini kwamba Rais anapokuwa mkuu wa dola ni mkubwa kuliko wengine? Nadhani tunahitaji elimu kujua tofauti ya Head of Government na Head of State. Kwa hiyo unataka kumlinganisha Rais na Jaji Mkuu? Hawalingani mzeee
 
Hili swali wamekuwa wakiulizwa mara kwa mara na msomi Tundu Lisu. Na amekuwa kiichambua sana katika katika eneo hii kuonyesha ni kwa namna gani wanafanya abuse of power. Kwa nini hajawahi kujitokeza hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoa ufafanuzi ili kuhalilisha kwamba anachokifanya Rais kiko sahihi?
Ni mpaka pale tu mwanasheria mkuu kupitia wizara ya sheria atakapo peleka muswada bungeni kumpa raisi mamlaka hayo vinginevyo ataendelea kukaa kimya na kubariki uvunjifu wa sheria.
 
kwa jinsi alivyo jibu ni dhahiri kwamba Mh. rais anatumia madhaifu ya katiba yetu inayompa mamlaka makubwa kufanya chochote wakati wowote so kwa nn hataki katiba mpya tena ya warioba!?
Akikubali Katrina mpya maana yake anajibana yeye kitu ambacho yeye na chama chake ccm hawataki kusikia kabisa , na kama tunataka katiba mpya lazima sisi kama taifa tumwage mboga zao na ugali kwanza ili wakubaliane na matakwa ya dai la katiba mpya. Lasivyo tutaishia kupiga Keller na kubakia na taifa lisilo na dira bora. Amueni kumwaga mboga zao na ugali ili nao waonje njaa tunayopitia inayotokana na maamlaka ya katiba waliyo nayo. Amueni moja tuuu nalo ni kuitaa katiba hii istumike katika uchaguzi mwaka 2020 , watupe tume huru ya uchaguzi.
 
KUMBE RAISI ANALIDHIBITI HATA BUNGE, SASA LINAISIMAMIAJE SERIKALI WAKATI LIKO CHINI YA RAISI.
Hujui kwamba Bunge linaweza kutunga sheria na Rais akakataa kuisaini? Hujui kwamba kwa mujibu wa Katiba Rais anaweza kutoa msamaha wa hukumu yoyote iliyotolewa na mahakama?
 
Walipa Kodi Wenye Nchi na Wenye Katiba Inayotaka Iheshimiwe. Bunge Linaipangia Serikali Jinsi ya Kuzitumia, Magufuli anadhani Yeye Ndiye anayetoa Fedha Kwa Kuwa Hata Bdgeti haiheshimu, anachukua Pesa za Mikopo ya Wanafunzi na Madawa anaenda Kunulia Ndege kwa Ushamba tu, halafu Kesho anawaambia wanafunzi wasimpush! Kisha wanaanza Kuwaambia Wengine hawajafikia Kiwango cha Kupewa Mikopo Kwani hawasomi Sayansi ya Mafuta ya Korosho!
UMEANDIKA KWA JAZIBA PAMOJA NA YOTE ULIYOSEMA BADO NI MTAWALA (EXECUTIVE) NDIYE ANAYEPELEKA HICHO BUNGE ILICHOPANGA NA HATA BUNDE ILICHOPANGA KINATOKANA NA MUSWADA WA BAJETI INAYOPENDEKEZWA NA WATAWALA. USHAURI WANGU ACHA UANAHARAKATI HII MIHIMILI MITATU HAIKO SAWA HATA KIDOGO.
 
Huyu jamaa kauliza swali la msingi sana, na kwa kiongozi mwenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo angelijibu kwa ufasaha, nakiri kuwa nimekuwa na kichwa kigumu kuamini kama tutakua na maendeleo katika awamu hii, mkuu hapendwi kuudhiwa ila anashindwa namna ya kufanya watu wasimuudhi, kingine kinachonifanya nisiwe na imani sana na serikali ya awamu hii, ni namna inavyoonesha chuki za wazi kwa upande unaowapinga, wanatumia nguvu ya madaraka badala ya hoja.
 
Hivi mkuu BAK, kama DU kashindwa kujibu maswali ya mtu kama Paskal anayeuliza kwa nidhamu na ka woga kidogo ataweza kweli kukabiliana na waandishi makini kama wa CNN au BBC ambao huwa hawana woga wala unafiki kama alivyokuwa anajibishana nao Ben? Naanza kujisikia aibu kabla hajaenda
Swali la Pascal halikuwa na mashiko ndio maana Rais naye kalijibu kwa swali. Rais ndiye anazindua Bunge, Rais anasaini miswada kuwa Sheria, Rais anateua majaji, Rais anaweza kufuta hukumu ya mahakama yoyote.
 
Hongera P Mayalla na jamiiforums kwa ujumla kuwa na Tankthinkers wazuri isipokuwa wachache wa buku sabaza za Lumumba
 
Vizur sana mayalla japo kakujibu vijanjajanja umekuna penyewe
 
Wauliza maswali wengi wao walikuwa kkkundi cha wahuni wachache walioandaliwa kuuliza maswali ya kusinzia
 
Back
Top Bottom