Hayo yameelezwa na Mh Rais wakati akijibu swali la mwandishi wa habari wa kujitegemea ndugu Mayalla , alipo muuliza mh Rais kuwa alipata wapi mamlaka ya kuzuia mikutano ya kisiasa kutoa maoni yao , na kudhibiti bunge ambapo bunge likitaka kusafirisha wabunge kwenda nje ya nchi waende wakaombe kibali kwa mheshimiwa Rais , haya mamlaka umeyatoa wapi ? kwakua uliapa kuilinda katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Majibu ya Rais "kwanza naomba ndugu mayalla unapo jiuliza kuhusu mihili hii pia jiulize kuwa nani anatafuta pesa na nani anayetoa pesa kwenye mihili hii mingine ya bunge na mahakama kama ukifahamu haya unaweza kufahamu kuwa ni mhimili gani ambao unaweza kuwa unamamlaka kwenye mihili mingine , kwa mfano nilipoenda bungeni kuhutubu niliwahutubia wabunge wabane matumizi mbele yao, na vilevile nilienda kwenye sherehe za mahakama wakaniambia kuwa hawatoi hukumu mapema kwa sababu hawana fedha niliamua muda huo huo kuwapatia fedha mhakimu na wao hawakuenda mahala popote kulalamika kuhusiana na hilo...