Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Sawa mkuu mpaka 2020 (m2020 ). Tumekulewa _ kwa nini unahalalisha lakini separation of powers ina maana tofauti na hii tafsiri yako na mkulu.
 
Rejea swali la Mayala!
Mayalla aliuliza kwamba Rais kapata wapi mamlaka ya kuwaambia Majaji na Wabunge kuomba kibali kabla ya kusafiri. Huo siyo uingiliaji wa mihimili mingine. Ndio maana Rais akauliza mbona hawakuhoji siku aliyoipa Mahakama hela za kuendesha kesi na pia mbona hawakuuliza siku ambayo Rais alihutubia Bunge na kueleza sera zake za kubana matumizi.

Hivi Jaji Mkuu anaweza kwenda kulihutubia Bunge kwa mujibu wa Sheria? Hivi Bunge lina ruhusa ya kubatilisha hukumu ya mahakama?
 
Kwakweli kauliza swali zuri japo halijajibiwa hata kidogo, eti mwenye chungu, mara fedha za bunge.....

Mara ohoo mayalla maana yake njaa yaani swali lilikuwa gumu kweli kweli kiasi sura ilianza kubadilika.Nampongeza sana Pasco Mayalla ingawa namhofia uenda asipewe tena mwaliko wa kweli kula bata Ikulu kwa ukosefu wa nidhamu uliotukuka.Nasema yale maswali yalilenga kumjaribu na kumdrive Mheshimiwa ambaye mwisho wa alisisitiza yeye ndio Rais sijui nani kamwambia yeye si Rais.
 
Kweli kwa swali gumu kama lile la Jana lazima alambishwe wapi Slow Slow na zile kelele zake
 
Wajameni tuache kutoa mapovu. Pascal Mayala haelewi utendaji serikalini ukoje ndio maana aliuliza ili aeleweshwe. Kuuliza si ujinga pamoja na.kwamba yeye niwanasheria. Hajawahi kuwa mtumishi wa umma na hivyo haelewi namna gani serikali na mihimili mingine inafanya kazi. Sidhani kama ni busara kumsifia kauliza swali la maana wakati swali lile lilikua wazi tu. Ni suala la kueleweshwa tu.
 
kauliza swali zuri na bila uoga kwa sababu ana uhuru wa kifedha pia yupo huru kikazi(mwandishihuru) ,sasa imefahamu kwamba ili journalist awe huru ni lazima afanye kazi yake independently, mkuu Pasco au Pascal Mayalla hongera,naamini ni mtu mmoja ila kama nimechanganya samahani
 
Kwa lipi hasa? Mbona mm sioni jipya?
 
ni mtu mmoja hujachanganya
 
binafsi napenda kuwa huru kwa kazi zangu binafsi,ajira ya kupewa na ambayo muda wowote naweza aibishwa na kutenguliwa hapana,pia na naamini kwa mtu wa aina yangu hawezi kubali ajira za kupewa kama unazozitaja
 
Next time na wewe nenda kamuulize Maswali yasiyokua na majibu ili akuzibe mdomo! Haya ya jana hebu tuyaacheni maana wao wamejichimbia shimo ambalo litakuja kuwa kaburi lao siku si nyingi, makofi yale waliyopiga kwa vicheko siku si nyingi yatabadirika kuwa mapigo ya Mapambio
 
Mkuu Kimbunga, utakuwa ama hufuatilii au umeamua tu kujenga hoja kwa kusimamia kile alichojibu rais. Si kweli kwamba watu hawakuhoji au kuuliza mheshimiwa Rais alipoipa hela mahakama. Kulikuwa na mjadala mkali sana uliojielekeza katika hofu ya Rais kuingilia uendeshaji wa kesi. Suala la kubana matumizi halia tatizo, na wananchi wanaunga mkono, wanachohoji wananchi, na bila shaka Mayala alisaidia wananchi kuhoji kiko wazi. Maswali yako ya mwisho sioni mantiki yake katika hoja ya msingi!
 
Asee uyuu jamaa ni shujaa japo swalii haljajibiwa kama inavyotakiwa ila hongera kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…