Wakuu kama mnakumbuka mdau mbishi wa Katiba ya Warioba Bwn.Humphrey Polepole alipewa ukuu wa Wilaya.Hii ilitafsriwa kuwa ni kumziba mdogo bwana huyu kwa kutumia kipande cha keki.Bwana yule hakuna na uwezo wa kutema kile kipande utamu ukamzidia Leo hii ni DC wa Ubungo cheo ambacho alikipinga sana akiwa timu ya Warioba.
Sasa from Nowhere amekuja Mwana JF mwenzangu Pasco,amevuma sana Leo mitandaoni.Paskali amehoji mambo magumu sana na hayakupata majibu,si kwa bahati mbaya,bali hakukuwa na majibu.
Je,mbinu iliyotumika kumrambisha udambwi-dambwi H.Polepole au Dr. Ryoba utatumika kwa Msukuma Paskali?
Ombi:Kwa kuwa Paskali amewahi kutuambia humu kuwa yeye hana shida na cheo kwa kuwa ana kipato kinachomtosha,Je uyaendelea na msimamo wako. Je,unamshauri nini Polepole kwa yale majibu ya Rais Hakuna katiba mpya?