Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Naomba Kuuliza et alvofanya uamuzi huo wa kubana matumizi amevunja katiba kama rais
 
Kujiamini ni kitu kizuri kwani ndiyo inayokiwa chachu ya Maendeleo hongera sana kwa maswali ya kijasiri brother.
 
Swali la Pascal halikuwa na mashiko ndio maana Rais naye kalijibu kwa swali. Rais ndiye anazindua Bunge, Rais anasaini miswada kuwa Sheria, Rais anateua majaji, Rais anaweza kufuta hukumu ya mahakama yoyote.
Ndugu yangu acha fikra zilizo lala wakati wewe ni muelewa. Kwa mitano hiyo, tunaona mawaziri na viongozi wengine wanaapa utii mbele ya Rais kwa vile ndio bosi wao. Sasa mbona na Rais anaapa utii mbele ya Jaji mkuu?
Ndio tunapokuja kwenye separation of power katika implementation ya majukumu ya uendeshaji.
Sii unajua kuwa hata bunge laweza kufukuza kazi Rais? Ni mambo tuu ambayo yapo katika katiba ili kuleta kuheshimiana
 
"Akifa Mbowe,Akifa Lissu,Wakifa wote mashujaa wa Nchi hii Wataibuka watu wasio Ogopa,Majasiri,watu wenye akili maalum ambao hawakutegemewa katika jamii, kama Akina PASCAL MAYALLA."~~Emanuel J John
8343462fd574040f569a74c59e39a989.jpg
 
Kujiamini ni kitu kizuri kwani ndiyo inayokiwa chachu ya Maendeleo hongera sana kwa maswali ya kijasiri brother.
Angeanza Pascal kuuliza nadhani wengi wangeuliza maswali ya maana wengine wametupotezea wakati
 
Kwa kweli kati ya maswali yote hili ndilo lilikuwa swali lenye mashiko kwelikweli. Ila majibu yake sasa...
 
Swali liliulizwa kisomi sana, na still alijaribu kuliwekea nyama nyama ili lisimtie ukakasi mkuu, lkn...
Na ndio maana hata morale ya kuuliza ilishuka wakabaki wana rudia rudia tu yale yale...
 
..mtiririko uko hivi:

1. Bunge linapitisha sheria.

2.mahakama inatafsiri sheria hiyo, au inatoa hukumu.

3.serikali inatekeleza hukumu hiyo.

..Raisi anapotoa msamaha haimaanishi kwamba amefuta hukumu.

..mimi sijawahi kusikia mtu amehukumiwa halafu Raisi akataa kutekeleza hukumu hiyo na kuamuru mhusika asitumikie adhabu. Huko ndiyo kufuta hukumu kwa mtizamo wangu.

..hata mamlaka aliyonayo Raisi ya kutoa msamaha kwa wafungwa amepewa na sheria iliyopitishwa na bunge. Hili siyo suala ambalo Raisi anajiamulia tu kwa utashi wake.

..pia umezungumzia Raisi kuteua mahakimu na majaji. Sasa nikuulize: Mbona Raisi huapishwa ktk nafasi hiyo na Jaji Mkuu?

..Tukijenga dhana kwamba Raisi hana mipaka ktk madaraka yake tunaweza kuiingiza nchi ktk matatizo.
Umenena vyama. Waanzilishi wa hii dhana na separation of powers amina Jeremy Bentham walitamani iwe hivyo yaani kila muhimili uwe kivyake bila kuingiiliana lakini wakagundua kwamba hakuna separation of powers isiyo na kuingiliana ndio wakaja na kitu inaitwa checks and balances. Rais anaweza kusamehe na anaweza kubadili hukumu. Mkuu wa Dola anakuwa na upper hand dhidi ya wakuu wengine wa mihimili. Hutaki basi sikulazimishi ila unaona mwenyewe nani ni namba 1 wa nchi.
 
Tatizo kifanya akili yako kutokua huru ni sbb ya kushindwa kumuelewa jpm.kuna vipengele vya katiba tulio wengi hatuvifaham mafuhum yake.naomba nipatiwe mfano wa hata nchi moja inayoongozwa na mahakama au bunge
Hadi mwana wa Adam arudi huwezi kupata jawabu ya hili swali lako.
 
Mimi mwenyewe nimeguswa sana na maswali ya mwandishi pascal mayala aliyomwuliza Raisi magufuli hakika pascal kaiva kikazi.
 
Maswali mangi ya msingi yalijibiwa kibabaishaji sana likiwemo hili.
 
Back
Top Bottom