Mh. Rais kajibu vizuri sana swali la Pasco ile asijue sheria hawezi kufahamu kwamba swali limejibiwa. Mh Rais alianza kujibu swali kwa kuuliza swali, mfumo amvao hutumiwa na wanafalsa kuwafanya waliouliza maswali kupata majibu yao kwa kujibu swali walilouliza.
Mh Rais alimuuliza mbona hukuuliza kwa nini nilikwenda kuhutubia bungeni??
Kama yuko smarti bila shaka atapata jibu kupitia ibara ya 62 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tz ambapo inasomeka hivi[emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116]
Ibara ya 62.
Ibara ndogo ya (1),
Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge.
Ibara ndogo ya (2),
Bunge litakuwa na wajumbe wa aina zote zilizotajwa katika ibara ya 66 ya Katiba hii ambao wote wataitwa Wabunge.
Ibara ndogo ya (3),
Iwapo jambo lolote lahitaji kuamuliwa au kutekelezwa na sehemu zote mbili za Bunge kwa mujibu wa masharti ya Katika hii au masharti ya sheria nyingine yoyote, basi jambo hilo halitahesabiwa kuwa limeamuliwa au limetekelezwa ipasavyo ila mpaka liwe limeamuliwa au limetekelezwa na Wabunge na vile vile na Rais, kwa mujibu wa madaraka yao kuhusu jambo hilo.
Katiba ya Tanzania - Android Apps on Google Play