Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli

lile swali lilikuwa very clever na mkubwa wa kazi akaishia kutoa spins tu kwa majibu aliyoandikiwa kutoka lumumba.
 
hongera pasco hakika hujatuangusha wanafamilia ya jf
Mkuu unaambiwa sio wa jf, huyu wetu ni nguchiro tu, hana uwezo wa kuuliza yale maswali, yeye ni mropokaji tu humu anaeitumikia lumumba
 
Majibu ya swali la Mayalla yanatoa viashiria vya uwepo wa "udikteta uchwara"
 
Nimemsikia Pasco Mayalla akiuliza swali kwamba Rais amepata wapi mamlaka ya kuwaambia Wabunge (legislature) na Mahakama (Judiciary) waombe ruhusa kwake watakapo kusafiri?

Hoja ya Pasco ni kwamba kuna separation of powers yaani Executive, Judiciary na Legislature ambazo zinatakiwa zifanye kazi bila kuingiliana. Hilo ni sawa ila Pasco kweli hafahamu kwamba Rais wa Jamhuri ni mkuu wa dola na chini ya dola ndio unapata executive arm, judiciary arm na legisleture?

Hajui kwamba Rais wa Jamhuri ni Head of Government na wakati huohuo ni Head of the State?
1.Kuwa head of state maana yake ni kuingilia mihimili mingine? 2. Unakubaliana na kinachofanyika kwa kuwa kinafanywa na head of state?
 
Mayalla kauliza swali la msingi sana ila rais amekosa jibu la maana
 
Kamuuliza kuwa kapata wapi mamlaka ya kuzuia safari za watumishi nje wakati kuna mihimili mitatu na yote inajiongoza yenyewe?

Pia kwanini mikusanyiko ya kisiasa inatambulika na katiba lakini yeye kaizuia wakati aliapa kutumikia nchi kwa mujibu wa katiba?

Kama wangekuwepo hata watano tuu wenye mwelekeo wa Pasco hakika angependa hayo masaa mawili yaishe aondoke, [COLOR=blue/]akini kwa vile waliokuwepo wengi ni makanjanja basi kawaambia waulize mpaka wachoke wenyewe[/COLOR].
[emoji3] [emoji3] [emoji85]
 
Tangu kumalizika kwa press ya Rais watu mbalimbali wamekuwa wakimsifia mwandishi mmoja ( Paschal Mayalala).

Najiuliza ni swali gani na lenye tija kwa wanyonge na maskini wa nchi hii alilouliza mpaka mnamuita hero?

Nawashangaa sana au ndo dalili za kufilisika hoja?

Mnamuonea wivu JPM anavyoinyoosha nchi?

USHAURI: Tulieni nchi irudi kwenye mstari then mambo mengine yatafuata

"NG'WANGALUKA MPAKA IKULU"
JPM OYEEEEEE!
WENYE WIVU WAJINYONGE.
 
Mayala anajielewa hayuko bias kama anavosifiwa sasa mawazo yake yaheshimiwe wakat mwingine akiandika usichokipenda
Najua yuko tayar kukoselewa pia
Hata rais kimyakimya kajua kuwa kaulizwa swali la maana.
Miaka 26 ktk fani c mchezo,ni umri wa vijana wengi humu ndan

Tunaomjua P toka enzi hizo za pikipiki kubwa(baja) na koti la ledha tunaheshim kaz yake

Hongera sana P
 
Mkuu unaambiwa sio wa jf, huyu wetu ni nguchiro tu, hana uwezo wa kuuliza yale maswali, yeye ni mropokaji tu humu anaeitumikia lumumba
daaa nikajua ndio yule aaaaarrrrgh
 
Sio kumsifu bali aliuliza swali kwa reference ya katiba na ni alijiandaa kwa swali.
 
Wanaomsifu Pasco ni werevu na wajuvi,wenye IQ kubwa ambao wanajua umuhimu wa kufuata na kutii katiba ya nchi.

Wewe mp...bvu huwezi ona wala kujua umuhimu wa masuali aliyouliza Pasco.
 
Watu siyo kwamba wanamchukia Mhe Rais isipokuwa tulitarajia watauliza maswali ambayo mtaani ndiyo kilio kikumbwa kama soko kwa mazao, bei ya mbegu kama za mahindi, promotion kwa watumishi, kazi ya vyama vya siasa n.k
 
ile press conference cjaona maana yake yani waandishi asilimia 99% wameuliza maswal mepesi na maswal magum yaliyoulizwa kama yale ya jamaa wa BBC na Pasco yamejibiwa kiujanjaujanja tu, mtu anatoa majibu ambayo yako out of the question, that conference was meaningless and a wastage of time.
And wastage of money kama vibahasha vya kaki vilikuwepo
 
Back
Top Bottom