Hongera sana TISS kwa kazi nzuri sana awamu ya tano

TISS effectiveness is INVERSELY proportional to the security measure of a common civilian but DIRECTLY proportional to the protectionism stature of a totalitarian state.

mnaojua hesabu kidogo mmenielewa!
Mimi sio hesabu tu Hata Hicho Kingereza sijakielewa
Matatizo ya kukumbia umande dah
 
Hapana. Hao ni Walinzi Maalamu wa Rais wanaitwa PSG kutoka Usalama!

Kumbe Mkuu! Akhsante kwa ufafanuzi wako ' Kuntu ' kabisa. Kwahiyo kumbe PSU na PSG ni vitengo viwili tofauti vya Ulinzi wa Viongozi? Nitashukuru mno kama utanijibia pia na hili Mkuu wangu kwani unaonekana ' umebobea ' sana katika haya masuala hivyo unaweza ukawa msaada mkubwa hasa Kwangu Mimi.
 
Mkuu acha ushamba Hakuna TISS anaebeba bunduki
wale walio vamia clouds ....n tiss je walikuwa na bunduki ama

hawa walio mpa ulinzi magu juzi ni tiss je walibeba nini?

bora uwe mshamba unaye elewa kuliko mjanja usiye jua kitu
 
Mie sio mhalifu nikajiunge ili iweje,kafa wa 1,2,3,4,5,6 hadi 30+ unasema kuna juhud,unazijua juhudi wewe?Halaf sasa si mara ya 1 hii
Wewe hujitambui mkuu,unafikiri vita ya kupigana na wahalifu inachukua siku moja?! Unakumbuka Marekani na ujanja wake kwa kuunganisha nguvu na washirika wae walitumia muda gani kumfuta Osama? unachoshangaa nini sasa,au unataka mpaka wakunyatie wewe na familia yako ndio ujue watu wako kazini? watu wangekuwa wamelala unafikiri hata ungekuwa na kiburi cha kukaa mtandaoni leo kuropoka ropoka vitu usivyovijua? Tulia wewe! watu wanarisk maisha yao kwa faida yako na familia yako halafu unaleta kidomodomo!!
 
Sasa Osama alikuwa anaishi Marekani?[emoji57]
 
mmmm TISS,mie nilifikiri kujadili system ni TABOO,kumbe wanajadiliwa kama M16,FBI.MOSSAD,ok ...,ila seriously now ule mradi wa umeme pale selous please ripoti ya kuhusu mazingira izingatiwe na impact yake kwa wanyama,ndege na viumbe vingine vinavyoishi kwenye lile pori,tusije piga kelele wakati tembo,nyati,samba n,k,watakapoanza kuingia kwenye makazi ya binadamu ,pale MLOKA wanaelewa hili na athari zake wameziona,sio sisi tulio kwenye comfort zones zetu hapa Magomeni.
 
Ni matumaini yangu hujawahi kuandika maneno yoyote ya kashfa dhidi ya serikali tangu umejiunga JF la sivyo suburi siku Maxence Melo atakapokubali matakwa ya serikali pale mahakamani ndipo utakapojua TISS ni wa kusifiwa au kuogopwa. Unaposikia wabunge wanalalamika watu kupotea ktk mazingira yasioeleweka unafikiri ni kazi ya nani? Wale walinzi wa mheshimiwa labda tuwaite Secret Service, TISS aka Usalama wa Taifa tupo nao mitaani, ndani ya daladala na hata maofisini kiasi ambacho wengine tunafahamiana nao, labda kama unajisifia mwenyewe!!!
 
Hongera zao, maana naona hata Bei ya sukari na unga imeshuka, ajira nje nje
 
Kuumbe! Huyu ndo Al watan
Yaani mwana wa nyumba.
 
Bro uwezo wako wa kufikiri ni mkubwa sana,nimependa jinsi ulivyohusisha visa vya marais mbalimbali compared na kwetu,kweli si rahisi kumcontrol mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…