Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
We mwarabu, kama unaumizwa na midafala ya wenye nchi yao, rudi kwenu.We Onyango toa UBUMBAFU .
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We mwarabu, kama unaumizwa na midafala ya wenye nchi yao, rudi kwenu.We Onyango toa UBUMBAFU .
Hakuna anayepinga uwekezaji wowote ule wa kutoka nje au ndani, wa kutoka kampuni ya Ulaya, Uarabuni, Asia au hata ndani ya Afrika, kama utaongeza ufanisi. Wanaoharibu kila kitu na hawa viongozi waliokosa hekima, ambao wanafikiri wanaweza kufanya maamuzi ya hovyo bila ya kuzingatia maslahi ya nchi, kwa sababu tu wao wamepewa rushwa nono.Mnaopinga huu ukodishaji njooni na solution! Ufanisi pale bandarini hakuna. Je SGR ikianza itakuwa ikipokea mizigo kwa speed hii hii? Mm nafurahia mijadala ya kuboresha vipengele vya mkataba. Kuhusu ufanisi nakubaliana na ukodishaji Ili tuendelee! Najiuliza sana, au tatizo ni mwarabu? Ivi tunaweza kuhoji uwezo wa kampuni ya Dubai kwenye hili?
Watu wamevitaja vipengere vyote vyenye utata kwenye mkataba. Kama kungekuwa na dhamira njema, tayari vipengere hivyo vingekuwa vimeanza kufanyiwa kazi kwa njia ya uwazi, lakini kigugumizi kwa upande wa Serikali na bunge, ni rushwa walizokula wakimwaminisha mwekezaji kuwa mkataba utakuwa vile vile, hakuna wa kupinga, wao ndio wenye maamuzi ya mwisho. Sasa watarudi vipi kuiambia DP, wakati walikwishalipwa kuhakikisha mkataba wa hovyo haubadilishwi?Wekeni clear huo unyonyaji basi ujadiliwe na makubaliano yafikiwe, unajua huu mjadala watu wengi ikiwemo maadui zetu wanataka mwisho wa siku tusiboreshe bandari yetu ibaki na speed ya 2G wakati tunahitaji 5G pale! Wafanyakazi wa bandarini hawataki mwekezaji kwa sababu wanajua akiingia uzembe kwisha
LD,Nani kayumba msimamo? Ndo matarajio yenu wakenya ili muendelee kufaidika na bandari zetu kukosa ufanisi sio?
Hongera kiongozi, ila nna swali katika watu waloandamana juzi we ulikuwepo na ilikuaje mwisho wake.Heko Watanzania kwa mwamko mnaoonesha wa kufuatilia masuala nyeti ya nchi yetu. Laiti tungekuwa hivi miaka 30 iliyopita tungekuwa mbali sana kimaendeleo..
Mnajua ukweli huu?: HAKUNA NCHI YA WAJINGA NA WAOGA ILIYOWAHI KUENDELEA! Ukiona ujinga na woga vinatoweka basi ujue maendeleo yapo karibu.
Hata kama serikali inaendelea kupoka uhuru na haki yetu ya kufanya maandamano mitaani, basi kwa sasa tufanye maandamano hayo online!
Nawaambia watanzania wenzangu maandamano haya yana nguvu na impact kubwa kuliko tunavyofikiri na tukiendelea hivi tutaona viongozi wetu wakijiuliza maswali mengi na kujirudi.
Mtu asibeze tunachofanya mitandaoni. Kama ilivyo kwenye maandamano mitaani kinachotakiwa katika maandamano ya mitandaoni ni UMOJA na MSHIKAMANO!
Utafiti unaonesha dozi inafika vizuri tu kwa njia hii. Tunaweza kuondokana na kero nyingi kwa njia hii na kuleta kuheshimiana kati yetu na viongozi wetu.
Tuoneshe umoja na mshikamano wetu bila kuchoka na tutaona matokeo yake.
Mungu ibariki Tanzania!