Hongera watanzania: Hata kama wanatuzuia kuandamana mitaani, tuandamane mitandaoni. Maandamano haya ya kisasa yana nguvu kubwa!

Hongera watanzania: Hata kama wanatuzuia kuandamana mitaani, tuandamane mitandaoni. Maandamano haya ya kisasa yana nguvu kubwa!

Mnaopinga huu ukodishaji njooni na solution! Ufanisi pale bandarini hakuna. Je SGR ikianza itakuwa ikipokea mizigo kwa speed hii hii? Mm nafurahia mijadala ya kuboresha vipengele vya mkataba. Kuhusu ufanisi nakubaliana na ukodishaji Ili tuendelee! Najiuliza sana, au tatizo ni mwarabu? Ivi tunaweza kuhoji uwezo wa kampuni ya Dubai kwenye hili?
Hakuna anayepinga uwekezaji wowote ule wa kutoka nje au ndani, wa kutoka kampuni ya Ulaya, Uarabuni, Asia au hata ndani ya Afrika, kama utaongeza ufanisi. Wanaoharibu kila kitu na hawa viongozi waliokosa hekima, ambao wanafikiri wanaweza kufanya maamuzi ya hovyo bila ya kuzingatia maslahi ya nchi, kwa sababu tu wao wamepewa rushwa nono.

Tatizo kubwa siyo mwekezaji bali kukosekana watu waadilifu ndani ya Serikali na bunge.
 
Wekeni clear huo unyonyaji basi ujadiliwe na makubaliano yafikiwe, unajua huu mjadala watu wengi ikiwemo maadui zetu wanataka mwisho wa siku tusiboreshe bandari yetu ibaki na speed ya 2G wakati tunahitaji 5G pale! Wafanyakazi wa bandarini hawataki mwekezaji kwa sababu wanajua akiingia uzembe kwisha
Watu wamevitaja vipengere vyote vyenye utata kwenye mkataba. Kama kungekuwa na dhamira njema, tayari vipengere hivyo vingekuwa vimeanza kufanyiwa kazi kwa njia ya uwazi, lakini kigugumizi kwa upande wa Serikali na bunge, ni rushwa walizokula wakimwaminisha mwekezaji kuwa mkataba utakuwa vile vile, hakuna wa kupinga, wao ndio wenye maamuzi ya mwisho. Sasa watarudi vipi kuiambia DP, wakati walikwishalipwa kuhakikisha mkataba wa hovyo haubadilishwi?
 
Tatizo Serikali inajibu hoja kwa ujumla,sana ! Kwa Nini Wanasheria wa Serikali wasijitokeze kujibu hofu za Watanzania! Kuacha hoja zijibiwe na Wanasiasa kunaidhalilisha Serikali.
 
Nani kayumba msimamo? Ndo matarajio yenu wakenya ili muendelee kufaidika na bandari zetu kukosa ufanisi sio?
LD,
Kuna makala zilizoandikwa kabla hatujayasikia haya ya DPW, na makala zote zilikuwa zikiyapamba Ufanisi, Utendaji, Uekezaji uliokuwepo,Unaotokea na uliowekwa katika BANDARI yetu Salama.

Abdallah Msuya aliandika haya tarehe 23 machi 2023, nitanukuu kiunagaubaga,

Tanzania: Uwekezaji wa kimkakati bandarini unachochea ukuaji wa uchumi
Mafanikio ya Tanzania yanaongea kwa sauti na kupaka rangi mustakabali mzuri wa nchi hasa katika sekta ya bandari ambayo inachangia asilimia 40 ya pato la taifa (GDP).
TPA kwa msaada wa serikali katika kipindi cha miaka miwili iliyopita imefanikiwa kubadilisha shughuli za bandari na kuongeza ufanisi.

Kumekuwa na maboresho makubwa katika miundombinu ya bandari, ununuzi na matumizi ya vifaa na teknolojia za kisasa za kushughulikia mizigo, usalama na usalama, huku hatua kubwa zikichukuliwa katika kuzitangaza bandari za nchi kwa lengo kuu la kuzidisha kiasi cha mizigo inayopitia bandari za Tanzania.

Source:Allafrica.Com



Swali:Ufanisi gani Mwingine?
Tumetupa Trillioni za Shilingi katika bandari zetu na mafanikio yalishaanza kujitokeza, kimsingi hatukupaswa kuwa tumekopa na kuwekeza iwapo walishajua DPW wanakuja na fedha zao kufanya hivyo!

Swali:Mikopo ilikuwa ya nini
 
LD,
Chini ni makala ya pili iliyoandikwa mwezi mmoja uliopita kabla ya Mkataba huu kuwekwa hadharani....ilizungumzia Ripoti ya World Bank... tena, kwa kiunagaubaga na bila mpangilio maalum ninayonukuu....

Bandari ya Dar es Salaam imepanda kwa nafasi 49 katika orodha ya hivi karibuni ya Benki ya Dunia katika bandari zenye ufanisi zaidi duniani.
Kupanda huko kinaweka Bandari ya Dar es Salaam mbele ya Bandari ya Mombasa...
Sekta ya bandari nchini imefurahia kipindi cha ukuaji thabiti katika suala la maendeleo ya miundombinu na upatikanaji wa vifaa na teknolojia za kisasa kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta hiyo ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania.

Uwekezaji umefanyika, maboresho yalifanyika DPW wanafanya nini hapa?

Kumekuwa na maboresho makubwa katika miundombinu ya bandari, ununuzi na matumizi ya vifaa na teknolojia za kisasa za kushughulikia mizigo, usalama na usalama, huku hatua kubwa zikichukuliwa katika kuzitangaza bandari za nchi kwa lengo kuu la kuzidisha kiasi cha mizigo inayopitia bandari za Tanzania.

Ujenzi mpya wa RoRo Berth umeongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam kushughulikia vyombo vikubwa kwa ufanisi, na kuboresha muda wa kugeuka kwa meli zinazopitia.



Mwezi mmoja baadae tunaambiwa kulikuwa hakuna ufanisi, na utendaji mbovu!

Narudia niliyobandika, CCM imerudi kutaka kurudia yale ya Marehemu Ben Mkapa. Niseme, Uchaguzi huu ujao haununuliki. Mengine, ongeza na za kwako..

Uwekezaji ufanyike, Ubinafsishaji ufanyike, ila uwe unaoenda kumkuza na kumheshimu Mtanzania/Mwafrika. Kwa hili wameleta sababu lukuki na zingine za kumkebehi, kumkejeli, na kumdharau Mwafrika wanatoa sababu za Kumdhalilisha Mwafrika, pamoja na kuwa kuna "political correctness" suala hili ni la Kibaguzi, selfishness na la kisiasa zaidi kuliko kiuchumi, ingawaje uchumi umetumika hapa kama malipo ya baadae. Ipo siku,, narudi, mtu, watu, au Taasisi zitakazo kujitokeza na kuweka uani kilicho nyuma ya hili. Mungu anisaidie.

Huko walipoenda walienda kutafuta usalama wa Kura tu 2025, songombingo yake wametumia mali ya, na Rasilimali za Mtanzania kufikia azma yao. Wataumbuka.
 
Bi mkubwa kashasoma alama za nyakati, hili jumba mbovu awe makini.
 
Heko Watanzania kwa mwamko mnaoonesha wa kufuatilia masuala nyeti ya nchi yetu. Laiti tungekuwa hivi miaka 30 iliyopita tungekuwa mbali sana kimaendeleo..

Mnajua ukweli huu?: HAKUNA NCHI YA WAJINGA NA WAOGA ILIYOWAHI KUENDELEA! Ukiona ujinga na woga vinatoweka basi ujue maendeleo yapo karibu.

Hata kama serikali inaendelea kupoka uhuru na haki yetu ya kufanya maandamano mitaani, basi kwa sasa tufanye maandamano hayo online!

Nawaambia watanzania wenzangu maandamano haya yana nguvu na impact kubwa kuliko tunavyofikiri na tukiendelea hivi tutaona viongozi wetu wakijiuliza maswali mengi na kujirudi.

Mtu asibeze tunachofanya mitandaoni. Kama ilivyo kwenye maandamano mitaani kinachotakiwa katika maandamano ya mitandaoni ni UMOJA na MSHIKAMANO!

Utafiti unaonesha dozi inafika vizuri tu kwa njia hii. Tunaweza kuondokana na kero nyingi kwa njia hii na kuleta kuheshimiana kati yetu na viongozi wetu.

Tuoneshe umoja na mshikamano wetu bila kuchoka na tutaona matokeo yake.

Mungu ibariki Tanzania!
Hongera kiongozi, ila nna swali katika watu waloandamana juzi we ulikuwepo na ilikuaje mwisho wake.
 
Back
Top Bottom