LD,
Chini ni makala ya pili iliyoandikwa mwezi mmoja uliopita kabla ya Mkataba huu kuwekwa hadharani....ilizungumzia Ripoti ya World Bank... tena, kwa kiunagaubaga na bila mpangilio maalum ninayonukuu....
Bandari ya Dar es Salaam imepanda kwa nafasi 49 katika orodha ya hivi karibuni ya Benki ya Dunia katika bandari zenye ufanisi zaidi duniani.
Kupanda huko kinaweka Bandari ya Dar es Salaam mbele ya Bandari ya Mombasa...
Sekta ya bandari nchini imefurahia kipindi cha ukuaji thabiti katika suala la maendeleo ya miundombinu na upatikanaji wa vifaa na teknolojia za kisasa kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta hiyo ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania.
Uwekezaji umefanyika, maboresho yalifanyika DPW wanafanya nini hapa?
Kumekuwa na maboresho makubwa katika miundombinu ya bandari, ununuzi na matumizi ya vifaa na teknolojia za kisasa za kushughulikia mizigo, usalama na usalama, huku hatua kubwa zikichukuliwa katika kuzitangaza bandari za nchi kwa lengo kuu la kuzidisha kiasi cha mizigo inayopitia bandari za Tanzania.
Ujenzi mpya wa RoRo Berth umeongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam kushughulikia vyombo vikubwa kwa ufanisi, na kuboresha muda wa kugeuka kwa meli zinazopitia.
Mwezi mmoja baadae tunaambiwa kulikuwa hakuna ufanisi, na utendaji mbovu!
Narudia niliyobandika, CCM imerudi kutaka kurudia yale ya Marehemu Ben Mkapa. Niseme, Uchaguzi huu ujao haununuliki. Mengine, ongeza na za kwako..
Uwekezaji ufanyike, Ubinafsishaji ufanyike, ila uwe unaoenda kumkuza na kumheshimu Mtanzania/Mwafrika. Kwa hili wameleta sababu lukuki na zingine za kumkebehi, kumkejeli, na kumdharau Mwafrika wanatoa sababu za Kumdhalilisha Mwafrika, pamoja na kuwa kuna "political correctness" suala hili ni la Kibaguzi, selfishness na la kisiasa zaidi kuliko kiuchumi, ingawaje uchumi umetumika hapa kama malipo ya baadae. Ipo siku,, narudi, mtu, watu, au Taasisi zitakazo kujitokeza na kuweka uani kilicho nyuma ya hili. Mungu anisaidie.
Huko walipoenda walienda kutafuta usalama wa Kura tu 2025, songombingo yake wametumia mali ya, na Rasilimali za Mtanzania kufikia azma yao. Wataumbuka.