Mkuu nimejibu kwamba sera nzuri ya serikali ni ile inayoangalia maslahi ya watu wengi katika nchi, Leo wakulima ni zaidi ya asilimia sitini ya watanzania achilia mbali wale wafanyakazi wanaotegemea kilimo pia kama njia nyingine ya kuongeza kipato chao
Pili suala la kuagiza nje hiyo ni sera nyingine ya mambo ya nje
kwa serikali ya taifa lolote lazima lilinde wazalishaji wake wa ndani kwanza kabla kuagiza bidhaa nje maana wazalishaji wa ndani ndio wanaoshikilia uchumi kuliko wachuuzi wa wanaogiza bidhaa nje ,
Swali je walaji wangapi wenye uwezo wa kuagiza nje kama sio kutegemea wachuuzi wachache wa kimataifa waongeze import kwa taifa
Hii ni sera ya kimapinduzi itawafanya vijana wengi wakinbilie kwenye kilimo kwa sababu wana uhakika wa soko
hivyo kilimo kuajiri mamillion ya vijana
Kuna pull and push attractive factor
serikali zilizopita zilitumia push attractive factor, mgambo na kuwafokea vijana waende kwenye kilimo kisicho na uhakika wa soko,
But akili kubwa imetumia pull attractive factor ya kutengeneza mazingira ya soko zuri hivyo vijana wengi watakimbilia fursa wenyewe ya kilimo
Unachokosea ni kufikiri kilimo kimeajiri watanzania wengi kwa sababu kina faida.
Kilimo kimeajiri watanzania wengi kwa sababu hakuna jinsi.
Matokeo yake watu inabidi tu walime Ili wajikimu. Unakuwa na agrarian economy.
Hakuna nchi tajiri duniani ambayo ina wakulima 60% hata ikiwa na wakulima 10% hiyo nchi lazima itakuwa masikini.
Tunataka kila mwaka tuambiwe ni jinsi gani productions costs za kilimo zimepungua.
Pia tujue mashamba makubwa mangapi yameanzishwa. Mashamba at least size ya ASAS.
Ukishusha gharama za uzalishaji utavutia wawekezaji wakubwa, kuwekeza kwenye mashamba makubwa. Hii itashusha Bei au itaongeza kipato cha mwananchi kwa sababu kilimo kutakuwa kama sehemu ya viwanda.
Mashamba makubwa ni viwanda.
Haya Mambo ya kuacha biashara ya kilimo iwe holela haitatufikisha popote.
Kilimo Ili kiimarike inabidi kifanywe na watu wachache. Siyo umvute kila mtu aanze kujilimia mihogo.
Watu wanahitaji nyama, samaki, maziwa, legumes etc... Vitu hivi Bei yake ni holela siku zote na vikipanda Bei zaidi tutazidi kudumaa, maana hata wakulima wengi hununua vitu hivi. Ndiyo maana tupo 10% ya nchi zinazoongoza kwa kudumaa duniani. People can't afford better nutrition kwa sababu ni Bei ghali.