Mkuu ni kweli Waziri ameamua kwa dhati kabisa kuwaona wakulima wanapata sahihi kutokana na kazi zao. Aidha nadhani Waziri angeangalia pia suala la vipimo (kilo) katika soko wakati wa mauzoya mazao yao. Leo vile vipimo rasmi (mizani) havitumiki kabisa huko vijijini, hawa watu wanao itwa wanunuzi (madalalI)wa mazao ya wakulima wanatumia vipimo (ndoo ndogo/kubwa, mabeseni, magunia ya plastiki n.k) katika manunuzi, vitu ambavyo sio vipimo halali. Tunaomba Mh Waziri uliangalie hili, maana vipimo hivi Kilo 1 ya hawa madalali ni sawa na kilo 1. 5 hadi kilo 2. Lumbesa (kujaza mazao kwenye gunia na kuongeza kilemba juu) mara nyingi hufikia kilo 130 hadi 150 na mkulima anaaminishwa ni kilo 100, kwa kweli wakulima wananyonywa. Tunakuomba Mh. Tutatulie na hili, japo kuwa kwa sasa jambo hili ni kama donda ndugu.