Unachokosea ni kufikiri kilimo kimeajiri watanzania wengi kwa sababu kina faida.
Kilimo kimeajiri watanzania wengi kwa sababu hakuna jinsi.
Matokeo yake watu inabidi tu walime Ili wajikimu. Unakuwa na agrarian economy.
Hakuna nchi tajiri duniani ambayo ina wakulima 60% hata ikiwa na wakulima 10% hiyo nchi lazima itakuwa masikini.
Tunataka kila mwaka tuambiwe ni jinsi gani productions costs za kilimo zimepungua.
Pia tujue mashamba makubwa mangapi yameanzishwa. Mashamba at least size ya ASAS.
Ukishusha gharama za uzalishaji utavutia wawekezaji wakubwa, kuwekeza kwenye mashamba makubwa. Hii itashusha Bei au itaongeza kipato cha mwananchi kwa sababu kilimo kutakuwa kama sehemu ya viwanda.
Mashamba makubwa ni viwanda.
Haya Mambo ya kuacha biashara ya kilimo iwe holela haitatufikisha popote.
Kilimo Ili kiimarike inabidi kifanywe na watu wachache. Siyo umvute kila mtu aanze kujilimia mihogo.
Watu wanahitaji nyama, samaki, maziwa, legumes etc... Vitu hivi Bei yake ni holela siku zote na vikipanda Bei zaidi tutazidi kudumaa, maana hata wakulima wengi hununua vitu hivi. Ndiyo maana tupo 10% ya nchi zinazoongoza kwa kudumaa duniani. People can't afford better nutrition kwa sababu ni Bei ghali.