Hongera Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kwa kutetea soko la wakulima, wanaokupinga ni wanafiki

Huna akili
 
Unazungumzia 'Free market" na humo humo bado unaweka "ruzuku"?

Mkuu, hakuna soko huria la aina hiyo..
Na nikujidanganya na hizi nadharia zisizo na maana, kwamba kuna soko huria halafu katika jamii hiyo hiyo kuna makundi yanayofaidika kwa aina moja au nyingine kwa msaada wa ziada zaidi ya wengine.

Hizi ni nyimbo tunazoimbishwa tu toka vitabuni nasi tunaimba kama ma'robot' bila kuweka akili juu yake kuhusu uhalisia wake upoje.
 
Naungana na Bashe, kufunga mipaka ni kupunguza hali ya kulima, Acha watu wauze popote, Ili kesho wengi waingie kwenye kilimo KWA sababu jirani zao wamelima wamepata.
Tunataka tuone magari ya plate number za Kenya yakizurura hadi mashambani vijijini yakimwaga noti kwa wakulima kama zamani.
Kabla ya Magu gari za friji za Kenya unazikuta zimepaki shambani bagamoyo zinapakia tikiti, nanasi, matango nk mkulima unalambwa cash. Ndio unaoziona hizi nyumba za mabati zilizochipuka kama uyoga vijijini, hali ingeendelea kisingekuwepo kwa nyumba za nyasi vijijini.
 
Mkuu 'Gift', kwa kawaida sina muda wa kupoteza kusoma magazeti kama haya unayoweka hapa. Hizi nadharia ni nadharia tu na common sense au intuition basi.
 
Sie wajinga tunaolima ndio tunanufaikaje Sasa wewe unatakaje labda? Naona mnajificha kwenye kichaka Cha walanguzi,lugha za wale failures
Toka kwenye ukulima, nenda kawe 'mlanguzi', bado huelewi?
Anayefaidika ni huyo anayenunua mazao yako siyo wewe mkulima.
 
Sera za hovyo ndio zimeua kilimo na kusababisha machinga na bodaboda kuzagaa mijini. Sababu kilimo hakilipi kama pesa ipo shambani nani awe bodaboda na machinga.
 
Hapa bado unaiingiza serikali kwenye biashara, ambayo Bashe anataka serikali isijiingize kabisa..

Kwa maana hiyo, acha wanaoingiza bidhaa toka nje nao wawe huru kuingiza chochote wakati wowote.
 
Alichofanya ni kama kubeba maji kwenye ndoo yenye matobo akitegemea itajaa...Akifungua mipaka huku watanzania ambao ndiyo walaji ndiyo wanaotengeneza cash economy watapata wapi power ya kununua mazao ya mkulima? Huoni kawatengenezea quater wale wa nje na hivyo watakuja kuichukua na kwenda ku enjoy kwao huku wakiiacha nchi hoi?

Uki calculate welfare effects hiyo quater ime enda nje na both consumer na producer wamekuwa impacted negatively...Hesabu za uchumi siyo absolute kama mathematics au calculus lazima ujue conditionalities na physical nature ya transactions unayo deal nayo kuanzia levels mbalimbali...
 
Hakuna nchi kichaa ya kufanya hivyo. Nchi zote kwanza zinalinda wakulima wao kwa kuhakikisha wanapata bei nzuri za ndani na hata kuexport. Jambo la pili wanazuia na kubana import ya mazoa ambayo yanaweza kuzalishwa na wakulima wao. Kuingiza mazao kutoka nje ni pale imepatwa na uhaba au haiwei kuzalisha bidhaa hiyo. Biashara huria si ya kwenda kichwakichwa.
 
Hakunaga soko huria la namna hiyo. Serikali zote zinamanipulate hili soko huria kwa faida ya nchi zao. Kanuni ya kwanza ni kuhakikisha unafanya export kubwa kuliko import. Serikali inaweza hata ruhusu mahindi kutoka USA, sukari kutoka Brazil na mchele kutoka SEA, lakini ni akili hiyo kwa uchumi wa nchi?
 
Naona wewe na Bashe hamuelewani.
Bashe yupo kwenye wizara ambayo wanunuzi toka nchi jirani wanakwenda shambani kwa mkulima na kununua mazao yangali shambani, na yeye Bashe hajui hilo kuwa linatokea nchini mwake.
Malori toka nje yanaingia ndani yanachukua mizigo Bashe hana habari, anasikia tu wakulima wameuza mazao yao wanakotaka wao!
 
Bashe ni mjanja sana mnamsifia anawatetea wakulima ni kweli lakini na yeye anajitetea humohumo, ana hundreds oh hectors huko Ikungi sijui anataka kulima zao gani, kama siyo alizeti basi korosho kwahiyo lazima ajiandalie mazingira mapema
 
Sasa hilo linashida gani? Serikali inachotakiwa ni kuhakikisha imenunua chakula cha kutosha kwa bei ya soko kufidia wakati wa njaa. Hii waliifanya wachina baada ya kupigwa na njaa na umasikini wakati wa Mao. baada ya Mao wakaja na Household responsibility. Unaiuzia serikali kiasi kadhaa cha mazao yako na mengine yote ni uu yako na jukumu lako kuyafanya utakavyo. Ukiuza , ukilisha wanyama ni wewe.
 
Kama ingekuwa hivi ingekuwa sahihi kwamba anaend akununua kwa mkulima na mkulima akishauza mazao yao yapo sehemu, yakiwa yameisha huko kwao serikali inaya rudisha sokoni na ndiyo hivyo nchi inakuwa haijapoteza, kinyume na hapo watu wa nje wananunua ama walanguzi (ambao ni wachache kwahiyo wanafanya monopsony kwakua hakuna masoko ya uhakika zaidi yao) na kwa bei ya chini kwa mkilima kisha wakisha ya toa mikononi mwa wakulima wanayarudisha kwa bei ya juu sokoni (Monopoly) kama ingekuwa ni wao tu boader imefungwa angalau tungekuwa na watanzania ambao watawekeza humu je ipo guaranteed? Kuna sera zipi za kuhakikisha hao wanunuzi walanguzi hawataenda kuwekeza nje ya nchi? Mbaya zaidi wanafungua mipaka na hivyo mazao yetu ambayo hayajawa processed yanaondoka na kwenda kuwa value added kisha yanarudishwa kwa walaji ambao unawakamua kodi kwa bei ya juu....Fungueni macho na masikio, uchumi haujengwi na mtu mmoja na wala si model moja unayoijua ndiyo infanya kazi, uchumi ni art na inahitaji magination and creativity ili kiweza kuujenga ndiyo sababu lazima saa nyingine utumie subjectivity na saa nyingine uwe objective....Tofaut na science zenye frames ambazo zipo absolute
 
Sera mbovu ndizo zilizalisha madalali wanyonyaji. Mkulima hana options za pa kuuza hivyo anampa dalali kwa bei ya hasara. Leo hii kama wafanyabiashara wa nje wanafuata mizigo mashambani huyo dalali hatakuwa na nguvu. Cha muhimu ni sera hii kuwa endelevu tu. inatatua hata hiyo shida ya dalali mnyonyaji.
 
Ndiyo ujiulize hilo swali Sasa.
Ukiwapa wakulima soko huria, basi wape consumers soko huria. Kuwapa consumers soko huria ni kuruhusu imports.

Otherwise, restrict wakulima na restrict consumers. Sasa hivi consumers wapo restricted, hiyo haisaidii taifa, wote tutakula chakula kidogo au kisicho bora.
Punguza production cost na uchochee uwekezaji wa mashamba makubwa.

United States Farm bill iliweka hela kwa wakulima(subsidy) na pia ikatoa food stamps kwa consumers ili waweze kununua vyakula.
You don't just allow food exports, utajimaliza.
 
Mkuu ni kweli Waziri ameamua kwa dhati kabisa kuwaona wakulima wanapata sahihi kutokana na kazi zao. Aidha nadhani Waziri angeangalia pia suala la vipimo (kilo) katika soko wakati wa mauzoya mazao yao. Leo vile vipimo rasmi (mizani) havitumiki kabisa huko vijijini, hawa watu wanao itwa wanunuzi (madalalI)wa mazao ya wakulima wanatumia vipimo (ndoo ndogo/kubwa, mabeseni, magunia ya plastiki n.k) katika manunuzi, vitu ambavyo sio vipimo halali. Tunaomba Mh Waziri uliangalie hili, maana vipimo hivi Kilo 1 ya hawa madalali ni sawa na kilo 1. 5 hadi kilo 2. Lumbesa (kujaza mazao kwenye gunia na kuongeza kilemba juu) mara nyingi hufikia kilo 130 hadi 150 na mkulima anaaminishwa ni kilo 100, kwa kweli wakulima wananyonywa. Tunakuomba Mh. Tutatulie na hili, japo kuwa kwa sasa jambo hili ni kama donda ndugu.
 
Soko huria siyo huria kama unayodhani. Nchi inalinda kwanza wazalishaji wake wa ndani na kuhakikisha ina export zaidi. Si rahisi kupunguza production cost sababu serikali italazimika kutumia pesa nyingi kwenye subsidizing. Njia nzuri ni kuhakikisha soko na bei nzuri. Hili halitavutia tu wawekezaji wakubwa kwenye kilimo, litafanya hata wale wadogo kuwa wakulima wakubwa.

Hao US kila siku wanawezesha wakulima wao kwenda kuuza mahindi na mazoa mengine ya kilimo Mexico huku wakifanya hila matunda ya Mexico(Maparachichi ya Mexico) yasifurike US ili kulinda wakulima wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…