Nilisikiliza maamuzi ya ZEC juu ya pingamizi la mgombea wa ACT, Maalim Seif. ZEC iliona makosa ya ujazaji fomu lakini haikuona kama makosa hayo ni sababu ya kuharibu Uchaguzi. Kwa maana kwamba, kosa la ujazaji halikuwa na lengo la kunufaisha mgombea au kuufanya Uchaguzi usiwe wa haki n.k.
Tatizo liko kwa NEC, NEC imeonesha ubwege wa aina fulani na kuufanya mchakato mzima kuwa kama zoezi la watoto wadogo.
Ni aibu kwa chombo kama NEC kubariki mapingamizi yanayotokana na mgombea kutoweka nukta katika majina yake, kusahau kuweka sahihi, au kuweka sahihi kabla ya kuwasilisha fomu, nk. Mapingamizi mengi yaliyowekwa kuwazuia wagombea udiwani na ubunge kwa vyama vya upinzani yameonesha udhaifu mkubwa wa Tume.
Ni Tume isiyo na umahiri wa kisheria au inayofany kazi kujipendekeza na kupewa heko kwa idadi ya kuwazuia wagombea wa vyama vya upinzani.