GE2025 Hongereni CHADEMA kwa kuukataa huu uhuni wa Tume ya Uchaguzi. Sasa mambo ni hadharani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
9,205
Reaction score
22,219
Tunaambiwa eti "Watanzania Milioni 37.6 wamejiandikisha kupiga kura".
Sidhani kama huyu ndugu alitakiwa aoneshe data base ya watu halisi milioni 37.6 waliojiandikisha maana ni uongo

Kuna mambo matatu!

1. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka
2022, idadi ya raia wa Tanzania ni milioni ambayo inakadiriwa kufikia milioni 62. Kwa mujibu wa sensa hiyohiyo, Asilimia 42.7 ya watu walikuwa na umri wa miaka chini ya 14 Sio 18), sawa na watu milioni 26.5. Kwahiyo waliobaki ni (62-26.5) = 35.5
Hiyo milioni 35.5 ni kuanzia miaka 15 na kuendelea. Tuseme raia wameongezeka, wale waliokuwa na umri kuanzia 15, sasa wana 18 na wanaweza kujiandikisha wakafikia idadi ya juu zaidi ya milioni 35.5.
Hiyo ni sawa na kusema 'karibu raia wote wenye miaka 18 na zaidi wamejiandikisha'. Je! Hilo linawezekana kwa Tanzania?
Hata hivyo, kuna mambo mengine ya kujiuliza kama ufanisi wa kuandikisha na pili muamko wa raia kujiandikisha.

2. Ufanisi wa kuandikisha.
Ni ukweli usio wa wazi ufanisi wa kuandikisha wapiga kura ni mdogo. Wengi waliojiandikisha ni mashahidi kwamba kwenye vituo vyao watu wengi waliondoka bila kuandikishwa kutokana na muda kuwa mchache na kushindwa kusubiri. Wapo waliosubiri siku ya mwisho na bado hawakutokea.

3. Muamko wa kujiandikisha.
Kuna idadi kubwa ya watu hawakujiandikisha kwa sababu mbalimbali. Wapo ambao hawakupata hata taarifa. Wapo wagonjwa. Wapo wasafiri. Wapo wengi ambao hawana mpango wa kupiga kura kama mimi.
Kusema, wapiga kura 'karibu wote' wamejiandikisha ni taarifa ya kutilia mashaka sana.

Nadhani kama taifa, kuna ugonjwa tunaugua. Ugonjwa wa kujidanganya huku tukijua tunajidanganya na hatupo tayari kupona.

Shetani limeshika hatamu!
Shetani halishibi damu!
IMG-20250726-WA0108.jpg

Nawasilisha.
Dr. Chris Cyrilo.
 
View attachment 3419917

Nawasilisha.
Dr. Chris Cyrilo.
Halafu ni Dr ujue
 
Kuna ndugu yangu alienda kuchukua kadi mpya za kidigital za ccm, aliambiwa aende na kitambulisho cha kupiga kura, sasa cha kujiuliza kwanini kiwe kitambulisho cha kupiga kura?

Hapo wameshahesabu kura kitambo, ndio maana huyo mama anajua atapita tu
 
Utakuta mtoa mada tu alijiandikisha kupiga kura yani hii nchi inawanafki sana.
Usipokuwa makini utajaa kwenye mfumo kichwa kichwa
 
Tunaambiwa eti "Watanzania Milioni 37.6 wamejiandikisha kupiga kura".
Sidhani kama huyu ndugu alitakiwa aoneshe data base ya watu halisi milioni 37.6 waliojiandikisha maana ni uongo

Kuna mambo matatu!

1. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka
2022, idadi ya raia wa Tanzania ni milioni ambayo inakadiriwa kufikia milioni 62. Kwa mujibu wa sensa hiyohiyo, Asilimia 42.7 ya watu walikuwa na umri wa miaka chini ya 14 Sio 18), sawa na watu milioni 26.5. Kwahiyo waliobaki ni (62-26.5) = 35.5
Hiyo milioni 35.5 ni kuanzia miaka 15 na kuendelea. Tuseme raia wameongezeka, wale waliokuwa na umri kuanzia 15, sasa wana 18 na wanaweza kujiandikisha wakafikia idadi ya juu zaidi ya milioni 35.5.
Hiyo ni sawa na kusema 'karibu raia wote wenye miaka 18 na zaidi wamejiandikisha'. Je! Hilo linawezekana kwa Tanzania?
Hata hivyo, kuna mambo mengine ya kujiuliza kama ufanisi wa kuandikisha na pili muamko wa raia kujiandikisha.

2. Ufanisi wa kuandikisha.
Ni ukweli usio wa wazi ufanisi wa kuandikisha wapiga kura ni mdogo. Wengi waliojiandikisha ni mashahidi kwamba kwenye vituo vyao watu wengi waliondoka bila kuandikishwa kutokana na muda kuwa mchache na kushindwa kusubiri. Wapo waliosubiri siku ya mwisho na bado hawakutokea.

3. Muamko wa kujiandikisha.
Kuna idadi kubwa ya watu hawakujiandikisha kwa sababu mbalimbali. Wapo ambao hawakupata hata taarifa. Wapo wagonjwa. Wapo wasafiri. Wapo wengi ambao hawana mpango wa kupiga kura kama mimi.
Kusema, wapiga kura 'karibu wote' wamejiandikisha ni taarifa ya kutilia mashaka sana.

Nadhani kama taifa, kuna ugonjwa tunaugua. Ugonjwa wa kujidanganya huku tukijua tunajidanganya na hatupo tayari kupona.

Shetani limeshika hatamu!
Shetani halishibi damu!
View attachment 3419917

Nawasilisha.
Dr. Chris Cyrilo.
Chadema inaufahamu huu upumbavu, Yaani zaidi ya nusu ya Watanzania wamejiandikisha!

Wadanganyeni wajinga wenzenu
 
Mbona ni rahisi tu.

Hilo daftari liwekwe wazi watu walikague kujuwa watu waliojiandikisha.
Kwani hapo kuna siri gani?

Je, hakuna njia yoyote ya kulazimisha uhakiki wa usahihi wa daftari hili?
Hakuna uwezekano wa kupeleka kesi mahakamani; hata kama mahakama nako kunaweza kuwa na matatizo yake, lakini mchakato huo unaweza kutoa mwanga zaidi juu ya hujuma hizi?
 
Hivi Kuna haja ya kupiga kura hiyo October, Mimi naona ni Bora Mh.Samiah angeendelea kuongoza bila kuitisha upigaji kura wenye sitofahamu nyingi 🤔
Ungeonekana kuwa mtu wa maana zaidi kama ungemshawishi rafiki yako huyo Samia asijihangaishe kugombea. Watu hawamtaki; kasoro labda wewe Pekee unaye mhimiza aendelee!
 
Watakuwa wanajumlisha wote waliojiandikisha kuanzia walipoanza miaka kama 20 iliyopita. Wapo na waliofariki
 
Wanatuona sisi wananchi ni wapumbavu kama walivyo wao sasa tutaona ambao watajitokeza kupiga kura.
Kwenye kaya yangu itakuwa marufuku kwa mtu yeyote kwenda kupiga kura siku hiyo
Mkuu, 'evangelicat', nasikitika kukueleza kuwa hiyo njia utakayotumia haitoshi kumzuia Samia kujitangaza mshindi.
Maana ya hayo manamba makubwa tuliyo tangaziwa leo, ni kuwa sisi tutakaobaki nyumbani bila kuiga kura hesabu yetu bado itakuwa ni ndogo kulinganisha na kura atakazokuwa ametengenezewa na kujazwa kwenye masanduku ya kura.

Kutokwenda kupiga kura ni sehemu moja ya kwanza, inayohitaji kufuatiwa na njia nyingine za kuzuia uchaguzi kikamilifu. Hata hizo kura za kutengenezewa nazo zisiweo kabisa.
 
Mbona ni rahisi tu.

Hilo daftari liwekwe wazi watu walikague kujuwa watu waliojiandikisha.
Kwani hapo kuna siri gani?
Waweke mara ngapi?
Ukitaka kuangalia watu wapya waliojiandishq picha zao na majina vilibandikwa kwenye kuta za ofisi zote za watendaji mitaa na vijiji

Na viongozi wa vyama mawakala waliruhudiwi kuhakiki hilo zoezi kuhakikisha watu wanajiandikisha hilo eneo ni wakazi wa eneo husika
Chadema hamkwenda mlivyo wapumbavu

sasa hivi ona sasa unaulizia daftari.Wakati watu wanapojiandikisha mlitakiwa kuwepo

Tabu yenu Chadema hamfuatilii mambo ya serikali mitaani mko tu na ujinga wenu
 
Ungeonekana kuwa mtu wa maana zaidi kama ungemshawishi rafiki yako huyo Samia asijihangaishe kugombea. Watu hawamtaki; kasoro labda wewe Pekee unaye mhimiza aendelee!
Hakuna haja ya uchaguzi manake imeshasetiwa kwamba lazima ashinde 🤔
 
Back
Top Bottom