Tunaambiwa eti "Watanzania Milioni 37.6 wamejiandikisha kupiga kura".
Sidhani kama huyu ndugu alitakiwa aoneshe data base ya watu halisi milioni 37.6 waliojiandikisha maana ni uongo
Kuna mambo matatu!
1.
Kwa mujibu wa sensa ya mwaka
2022, idadi ya raia wa Tanzania ni milioni ambayo inakadiriwa kufikia milioni 62. Kwa mujibu wa sensa hiyohiyo, Asilimia 42.7 ya watu walikuwa na umri wa miaka chini ya 14 Sio 18), sawa na watu milioni 26.5. Kwahiyo waliobaki ni (62-26.5) = 35.5
Hiyo milioni 35.5 ni kuanzia miaka 15 na kuendelea. Tuseme raia wameongezeka, wale waliokuwa na umri kuanzia 15, sasa wana 18 na wanaweza kujiandikisha wakafikia idadi ya juu zaidi ya milioni 35.5.
Hiyo ni sawa na kusema 'karibu raia wote wenye miaka 18 na zaidi wamejiandikisha'. Je! Hilo linawezekana kwa Tanzania?
Hata hivyo, kuna mambo mengine ya kujiuliza kama ufanisi wa kuandikisha na pili muamko wa raia kujiandikisha.
2. Ufanisi wa kuandikisha.
Ni ukweli usio wa wazi ufanisi wa kuandikisha wapiga kura ni mdogo. Wengi waliojiandikisha ni mashahidi kwamba kwenye vituo vyao watu wengi waliondoka bila kuandikishwa kutokana na muda kuwa mchache na kushindwa kusubiri. Wapo waliosubiri siku ya mwisho na bado hawakutokea.
3
. Muamko wa kujiandikisha.
Kuna idadi kubwa ya watu hawakujiandikisha kwa sababu mbalimbali. Wapo ambao hawakupata hata taarifa. Wapo wagonjwa. Wapo wasafiri. Wapo wengi ambao hawana mpango wa kupiga kura kama mimi.
Kusema, wapiga kura 'karibu wote' wamejiandikisha ni taarifa ya kutilia mashaka sana.
Nadhani kama taifa, kuna ugonjwa tunaugua. Ugonjwa wa kujidanganya huku tukijua tunajidanganya na hatupo tayari kupona.
Shetani limeshika hatamu!
Shetani halishibi damu!
View attachment 3419917
Nawasilisha.
Dr. Chris Cyrilo.