Hongereni sana Law School of Tanzania kwa kulinda ubora wa fani ya sheria hapa Nchini

Tatizo ni digrii nyingi ni magumashi ndio maana law school hawatoboi.

Sasa mtu anamaliza digrii hajui hata kuandaa nyaraka za kufungua kesi mahakamani unafikiri atatoboa pale law school kweli?.

Amini nakwambia kuna watu wengi wanamaliza digrii ya sheria na hawajui hata kuandika barua ya kuomba kazi achilia mbali barua ya kujieleza

Law school panahitaji mtu awe na uwezo wa kuchambua mambo kwa haraka, awe na uwezo wakuandaa nyaraka za mahakamani, awe na uwezo wa kutafsuri sheria.na kujua atumie vipi zaidi ya yote awe na uwezo wakuelewa maelezo ya swali alilopewa
 
Amini nakwambia kuna watu wengi wanamaliza digrii ya sheria na hawajui hata kuandika barua ya kuomba kazi achilia mbali barua ya kujieleza
Mkuu una ngazi ipi ya elimu ya sheria Astashaha, Shahada au Shahada ya Uzamivu?

Km kitu hukijui ni bora ukae kimya kuliko kujitia ujuaji mwingi

Somo la Communication skills ndilo linalofundishwa karibu semester zote na ndilo lina hio topic ya kuandika barua ya maombi ya kazi

Sasa unasemaje hawajui kuandika barua hapo unawatupia lawama wanafunzi, walimu au serikali?

Tafakari kwanza kabla haujashika kalamu yako na kuandika ujinga wako
 
Mwaka huu katika darasa la watu 600 wamefaulu 26 tu.
Wanaofaulu pale Law school ukisoma fact sheet yao ni chini ya 10% kila mwaka, tatizo linaweza kuwa sehemu zote mbili shule na wanafunzi.

Kiuhalisia sio vizuri kumaliza digrii ya sheria na kuunganisha law school, labda kama mtu ameshakaa kwenye.firm wakati anasoma digrii yake.

Ni vizuri na inashauriwa baada ya kumaliza digrii mtu akae angalau miezi 6 hadi mwaka 1 kwenye law firm ajifunze kwa vitendo ndio aende law school, kama ilivyokuwa lazima kwa zamani ufanye intern miaka miwili ndio ukafanye mtihani wa Bar

Tatizo digrii zote za sheria ni porojo tu (theory) ambayo hautaitumia kabisa pale law school na hata ukiitumia haifiki 25% ya ulichokivuna, law schoolni kama vile unaanza kusoma upya na unasoma mambo mapya.

Usishangae mtu ana GPA ya 4+ au hata ana PhD na law school ame disco hio ipo na inawezekana kabisa.

So ukitaka kumshauri mtu mwambie akae kwenye law firm kwanza ajifunze kisha aende sasa LST kupambania kombe
 
Wanasheria wanapataje digrii huko vyuoni hadi washindwe kufaulu kwenye uwakili kwa kiwango cha kutisha vile ? Tunapenda weledi lakini si vizuri kutumia kinachoitwa weledi kukomoa wengine
 
Aje kusema Braza Shonga anakomoa vijana [emoji23][emoji23]
 
Kwa hiyo, kumbe tuna wanasheria na mawakili. Asante kwa Elimu hii. Nadhani, utafafanua zaidi. Mimi na "uanasheria wangu wa msituni", nilijua ukishahitimu sheria teyari ni Wakili.
Mtu yoyote mwenye degree ya sheria ni mwanasheria lakini siyo kila mwanasheria ni wakili
 
Huyu ni chawa wa Magu tangu mwanzo
 
Rafiki ipo hivi, kila wakili ni mwanasheria ila sio kila mwanasheria ni wakili.

Wapo wanasheria ofisi za serikali na hata binafsi amabo sio mawakili, hawa huwa wanafanya kazi chini ya usimamizi wa wakili (kama yupo) kuna muda wanafanya kazi wenyewe ila huwa kuna changamoto.

Sasa tofauti ya wazi kati yao ni kuwa wakili yeye anamamlaka.yakuwakilisha au kutetea mtu Mahakamani, ila mwanasheria asiye wakili hana hayo mamlaka.

Pia wakili anayo Mamlaka ya kuapisha watu sababu yeye ni Kamishba wa viapo, ila mwanasheria asiye wakili hana hayo mamlaka sababu sio kamishna wa viapo.

Jambo lingine wakili anaweza kuandaa nyaraka mbali mbali sababu yeye ni Mwandishi wa umma, lakini mwanashetia asiyekuwa wakili hana mamlaka ya kuandaa nyaraka za kisheria. Hili la kuandaa nyaraka limekuwa changamoto sababu hadi stationary watu wanaandaa nyaraka za kisheria hao ndio huitwa Vishoka.

Kwenye swala la kwanini anaitwa wanasheria Mkuu wa serikali, hii inabeba dhana kamili ya kuwa fani ni sheria na wahusika ni wanasheria awe ni wakili asiweni wakili bado ukiwaba shahada ya sheria wewe ni mwanasheria.

Lakini pia kuna Wakili Mkuu wa serikali huyu yupo chini ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali, huyu huwa ana shughulika na kesi zote za madai dhidi ya serikali.

Kisha yupo Muendesha Mashtaka Mkuu wa serikali, huyu anashughulika na kufungua na kuendesha kesi zote za jinai nchini.

Zipo ofisi nyingine nyingi chini ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ambazo kimsingi zina mawakili na wanasheria.

Naamini utapata mwanga
 
Huyo ni Paralegal sio Lawyer

Lawyer lazima awe amepitia law school akafaulu bar exams na akapatiwa Muhuri wa Mwanasheria

Ushaelewa sasa?
Hapana, paralegal ni mtu mwenye cheti cha sheria au mwenye shahada nyingine ambaye atapewa mafunzo rasmi ya sheria. Ukisoma Sheria ya msaada wa kisheria imetoa maana ya nani ni Mwanasheria, nani ni Wakili na nani ni Msaidizi wa kisheria.

Kasome kifungu cha 2 au cha 3 kinachotoa tafsiri/maana ya maneno.
 
Kwa hiyo uwakili ni zaidi ya uanasheria!?
Mtu yeyote aliyehitimu shahada ya kwanza ya sheria ni mwanasheria ila wakili ni yule mhitimu wa sheria aliyepita shule kuu ya sheria.

Wakili anaingia mahakamani kumwakilisha mteja lakini mwanasheria asiye wakili haruhusiwi.

Kiufupi kila wakili ni mwanasheria lakini sio kila mwanasheria ni wakili.
 
Asante sana Mkuu. Umejibu maswali yangu yote. Sina dukuduku lingine kuhusu jambo hili kwa maelezo yako haya. Kwa Mara nyingine. Shukrani sana Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…