404 Pages
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,703
- 2,963
Huyo ni Paralegal sio LawyerMwanasheria wa Serikali asiye na muhuri
Lawyer lazima awe amepitia law school akafaulu bar exams na akapatiwa Muhuri wa Mwanasheria
Ushaelewa sasa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo ni Paralegal sio LawyerMwanasheria wa Serikali asiye na muhuri
Tatizo ni digrii nyingi ni magumashi ndio maana law school hawatoboi.Mleta mada nini kimekufanya uje na huu uzi, sio umeona malalamiko yamezidi ndio maana? Naamini utakuwa umesoma gazeti la Mwananchi la leo, wengi mno wanafeli.
Sioni sababu kwanini wanafunzi wengi wafeli kiasi hicho, ni either walimu ni incompetent, au kama ni competent, basi wanawafelisha makusudi hao wanafunzi, na kama muda wa masomo ni mfupi wauongeze, lakini sio huu utapeli wanaoufanya wa kula bure ada za wanafunzi.
Sijawahi kuona shule inayosifiwa kwa kufelisha wanafunzi wengi hapa duniani zaidi ya hiyo Law School, sifa yao kuu imekuwa ni kufelisha, na ajabu wajinga mnawapongeza.
Mkuu una ngazi ipi ya elimu ya sheria Astashaha, Shahada au Shahada ya Uzamivu?Amini nakwambia kuna watu wengi wanamaliza digrii ya sheria na hawajui hata kuandika barua ya kuomba kazi achilia mbali barua ya kujieleza
Wanaofaulu pale Law school ukisoma fact sheet yao ni chini ya 10% kila mwaka, tatizo linaweza kuwa sehemu zote mbili shule na wanafunzi.Mwaka huu katika darasa la watu 600 wamefaulu 26 tu.
Wanasheria wanapataje digrii huko vyuoni hadi washindwe kufaulu kwenye uwakili kwa kiwango cha kutisha vile ? Tunapenda weledi lakini si vizuri kutumia kinachoitwa weledi kukomoa wengineKwa moyo wa dhati nipende kuwashukuru watendaji wote wa Law School of Tanzania (shule ya sheria ) kwa kuzingatia weledi katika kufundisha na hatimaye kutoa wanasheria ambao watatumika serikalini pamoja na sekta binafsi.
Napenda nikiri wazi kabisa kwamba shule hii ni moja wapo ya taasisi chache za Serikali zinazozingatia weledi.
Watendaji wake hawafungwi na jina la mwanafunzi wala uwezo wake kiuchumi.
Wanazingatia kujiweka mbali na ukaribu na wanafunzi utaopelekea kutoa upendeleo katika usahihishaji.
Wanazingatia mno ubora wa mwanafunzi katika kutoa kile alicho nacho kichwani kwake.
Nawaomba wasiache hata mara moja ubora huu kwani kwa kufanya hivyo wataliangamiza Taifa kwa kutoa wanasheria wasiokuwa na uwezo hivyo kuharibu taaluma ya sheria.
Mungu aendelee kuwatia nguvu kwa kusimamia taaluma zenu kwa manufaa ya Taifa.
Aje kusema Braza Shonga anakomoa vijana [emoji23][emoji23]Watu kama nyie ndio mnaofeli halafu mnasingizia chuo.
Law school inatoa wanasheria wenye sifa ya kuwa mawakili.
Haitoi mawakili.
Anayetoa uwakili ni Jaji Mkuu.
Ukifaulu Law School, bado hauwi wakili moja kwa moja , lazima utume maombi kwa jaji mkuu ambaye atakuita kukufanyia interview baada ya muda wa mapingamizi kupita.
Unaweza ukafaulu law school na usiapishwe kuwa wakili kama jaji mkuu atakubaliana na mapingamizi yaliyetwa juu yako.
Hivyo Law School haitoi mawakili bali wanasheria wenye sifa ya kuwa mawakili.
Angalia hayo matokeo halafu tafakari , kumbuka kwamba Watahiniwa wote ni graduatesMnatuchanganya, mwingine ameandika siasa chafu za law shool.
Masaa 17 baadae unakuja wewe na counter thread ya kuwaambia hongereni. Sisi tusioyajua ya ndani, tushike lipi?
Mtu yoyote mwenye degree ya sheria ni mwanasheria lakini siyo kila mwanasheria ni wakiliKwa hiyo, kumbe tuna wanasheria na mawakili. Asante kwa Elimu hii. Nadhani, utafafanua zaidi. Mimi na "uanasheria wangu wa msituni", nilijua ukishahitimu sheria teyari ni Wakili.
Huyu ni chawa wa Magu tangu mwanzoUliyeleta mada hii una tabia ya kusifu na kuabudu serikali ya kijani. A.K.A chawa wa kijani. Tunakujua.
No surprise, hujaweza kukemea vitendo viovu hapo LST kama rushwa na upendeleo. Vipo sana tu.
Umejikita kusifia blindly bila ku reason kama msomi. Kweli ukiwa lumumba fc akili unaiacha mlangoni.
Wanakomoa watuAngalia hayo matokeo halafu tafakari , kumbuka kwamba Watahiniwa wote ni graduates
Rafiki ipo hivi, kila wakili ni mwanasheria ila sio kila mwanasheria ni wakili.Asante sana Mkuu Kwa ufafanuzi. Ubarikiwe. Sasa najaribu kuwaza kuwa Kuna uwezekano wa kumpata Mwanasheria wa Serikali asiye na muhuri? Maana naona hapa muhuri mpaka uende kwenye hiyo shule. Pia mwenye muhuri yaonekana ni mzito kuliko asiye na Muhuri. Sasa kama ni mzito kwa nini kwenye Cheo cha Mwanasheria Mkuu wa serikali kisitumike Cheo Hiki kikuu? Yaani Wakili Mkuu wa serikali (nadhani kiki Cheo kipo) ndiye afanye kazi za Mwanasheria Mkuu wa serikali. Natanguliza Shukrani kwa majibu.
Hapana, paralegal ni mtu mwenye cheti cha sheria au mwenye shahada nyingine ambaye atapewa mafunzo rasmi ya sheria. Ukisoma Sheria ya msaada wa kisheria imetoa maana ya nani ni Mwanasheria, nani ni Wakili na nani ni Msaidizi wa kisheria.Huyo ni Paralegal sio Lawyer
Lawyer lazima awe amepitia law school akafaulu bar exams na akapatiwa Muhuri wa Mwanasheria
Ushaelewa sasa?
Mtu yeyote aliyehitimu shahada ya kwanza ya sheria ni mwanasheria ila wakili ni yule mhitimu wa sheria aliyepita shule kuu ya sheria.Kwa hiyo uwakili ni zaidi ya uanasheria!?
hapana tusilichukulie jambo hilo kwa wepesi namna hiyo.haiwezekani nusu ya darasa wakafeli.nadhani kuna jambo chini ya kapeti.wajuvi watujuze ni nn kinaendelea hapo shule ya sheria?Huyo KADISCO vibaya ndio maana kuandika hivyo
Ndo nami nasangaa. Iweje uwe wakili bila kujifunza sheria?
Mwanafunzi akifuzu hapo anakua mwanasheria au anakua wakili?Law school wanatoa Postgraduate diploma in legal practice
Asante sana Mkuu. Umejibu maswali yangu yote. Sina dukuduku lingine kuhusu jambo hili kwa maelezo yako haya. Kwa Mara nyingine. Shukrani sana Mkuu.Rafiki ipo hivi, kila wakili ni mwanasheria ila sio kila mwanasheria ni wakili.
Wapo wanasheria ofisi za serikali na hata binafsi amabo sio mawakili, hawa huwa wanafanya kazi chini ya usimamizi wa wakili (kama yupo) kuna muda wanafanya kazi wenyewe ila huwa kuna changamoto.
Sasa tofauti ya wazi kati yao ni kuwa wakili yeye anamamlaka.yakuwakilisha au kutetea mtu Mahakamani, ila mwanasheria asiye wakili hana hayo mamlaka.
Pia wakili anayo Mamlaka ya kuapisha watu sababu yeye ni Kamishba wa viapo, ila mwanasheria asiye wakili hana hayo mamlaka sababu sio kamishna wa viapo.
Jambo lingine wakili anaweza kuandaa nyaraka mbali mbali sababu yeye ni Mwandishi wa umma, lakini mwanashetia asiyekuwa wakili hana mamlaka ya kuandaa nyaraka za kisheria. Hili la kuandaa nyaraka limekuwa changamoto sababu hadi stationary watu wanaandaa nyaraka za kisheria hao ndio huitwa Vishoka.
Kwenye swala la kwanini anaitwa wanasheria Mkuu wa serikali, hii inabeba dhana kamili ya kuwa fani ni sheria na wahusika ni wanasheria awe ni wakili asiweni wakili bado ukiwaba shahada ya sheria wewe ni mwanasheria.
Lakini pia kuna Wakili Mkuu wa serikali huyu yupo chini ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali, huyu huwa ana shughulika na kesi zote za madai dhidi ya serikali.
Kisha yupo Muendesha Mashtaka Mkuu wa serikali, huyu anashughulika na kufungua na kuendesha kesi zote za jinai nchini.
Zipo ofisi nyingine nyingi chini ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ambazo kimsingi zina mawakili na wanasheria.
Naamini utapata mwanga
akifuzu hapo anaenda kuapishwa na Jaji Mkuu ili awe wakili.Mwanafunzi akifuzu hapo anakua mwanasheria au anakua wakili?