Ok,iko hv.huku tupo wasukuma mikoa mitano yote ni ya kwetu,na nitajaribu kwa kifupi kuchambua kulingana na maeneo yetu.
1.ikumbukwe tunaishi Tabora,Shinyanga,Simiyu,Mwanza,Geita na pembezoni mwote mwa ziwa victoria
2.Wasukuma wa Tabora ni wakarimu japo wana kanamna ka kupenda kidogo ushirikina lakini ni wavumilivu ktk mapenzi,wao wana destuli ya uvivu kidogo wa kuchapa kazi lakini si wavivu kiasi cha kuwasema vibaya,wapole na hawana mawaa na mtu awaye yote
3.Wasukuma wa Shinyanga,ni wachapa kazi na wakarimu,na kwa namna fulani hv ni wakorofi kidogo na hawapendi kuonewa.
4.Wasukuma wa Simiyu,hawa ni wakorofi na ni wakarimu pia,ni wachapa kazi kweli kweli hawana uvivu,wanatafuta mali hata kama wewe mwanaume umelala ndani au umetelekeza familia usitegemee watoto watakufa na njaa.
5.Wasukuma wa Mwanza ni the same na Geita,hawa hata wewe uwe wa makabila mengine nenda kaoe,ni wakarimu kupitiliza na wapole sana,hawa mume anaweza kuoa mke wa pili lakini yeye akaishia kulia machozi kwa siku moja then anatulia na kusamehe na mambo yanaendelea,na hawa ndiyo wenye shepu nzuri na ni Blackbeauty kweli kweli tofauti na wa Simiyu na Shy ambao wao ni weupe,wanaitwa wanyantuzu.hakuna desturi ya ukeketaji,na wasukuma wote siyo wachoyo hasa wa chakula.wao humkirimu mgeni yeyote ajaye nyumbani mwao au maeneo yao.
6.TAHADHARI.kama utakuja wewe mtu wa makabila mengine ukaoa mke wa SIMIYU mnyantuzu,elewa una mwanajeshi iwapo utamletea za kuleta,hao ndo wana sifa hata ya kukutoa roho ukiwa umepata pesa na ukajidai kumchanganyia habari zako.hii ni kwa ufupi
N.B ni wakarimu na wachapa kazi all Sukuma.ASANTE