Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Naomba nichukue nafasi hii nikiwa kama mdau wa michezo na shabiki mkubwa wa timu ya Yanga (Timu ya Wananchi), kuupongeza uongozi wa timu, chini ya Mwenyekiti Mshindo Msolla, Wadhamini wa timu, benchi la ufundi, na wadau wote kwa ujumla! Kwa kufanya usajili mzuri.
Nimekiona hiki kikosi mahali fulani! Baada ya kukikagua kwa muda mrefu, nimejiridhisha ni kikosi bora! Na nina imani kubwa kitafanya vizuri kwenye ligi yetu ya ndani, na pia kwenye mashindano ya kimataifa.
Magolikipa;
Djgui Diarra, na Eric Johora.
Walinzi;
Djuma Shaban, Kibwana Shomari, David Bryson, Adeyun Saleh, Yassin Mustapha, Abdallah Shaibu, Dickson Job, Bakary Mwamnyeto, Yanick Bangala.
Viungo;
Khalid Aucho, Mukoko Tonombe, Deus Kaseke, Feisal Salum, Zawadi Mauya, Saido Ntibazonkiza, Farid Mussa, Balama Mapinduzi, Jesus Moloko, Ditram Nchimbi, Dickson Ambundo.
Wasambuliaji;
Fiston Mayele, Heritiel Makambo, Yacouba Sogne, Yusuph Athumani!
Binafsi nilitamani sana kumuona pia mlinda mlango Metacha Mnata akiwemo, badala ya huyo golikipa Mrundi! Lakini ndiyo hivyo tena.
Kwa usajili huu, unaona kabisa viongozi wa Yanga wamekubali kubadilika. Hawajasajili kishabiki, au kwa kukurupuka kama ilivyokuwa kwa misimu miwili iliyopita. Badala yake wamesajili watu wa kazi!!
Hakika naamini kati ya Yanga na Azam, mmojawao kati yao atachukua ubingwa wa ligi kuu! Huku Yanga ikiwa na nafasi kubwa zaidi! Hakika Yanga ya msimu ujao ni 🔥🔥