Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 4,120
- 3,468
Niende moja kwa moja kwenye mada.
Nimeshuhudia mimi mwenyewe. Nilikuwa na mgonjwa aliyehitaji huduma ya dharura katika hospitali moja ya Wilaya ya Ilala. Tena tumemkimbiza usiku wa saa sita. Tulipofika tu akaanza kupimwa na kutokana na hali aliyokuwa nayo alihitaji kufanyiwa upasuaji usiku uleule.
Kwa kuwa mgonjwa hana Bima tulitakiwa kulipa cash. Cash hatukuwa na kiasi cha kutosha tukaambiwa BILA CASH KULIPWA HAMUWEZI KUPATA HUDUMA. Kuna msamaria mmoja kati ya wale waliopeleka wagonjwa akatueleza twende hospitali fulani.
Tulipofika hospitali ile tukaambiwa mgonjwa wenu tutamfanyia upasuaji na malipo mtayalipa baada ya huduma. Ikawa hivyo. Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuwaumba hawa watu wenye Roho Nzuri na tunawatakia maisha marefu.
Lakini hawa wenye kupenda pesa badala ya kuhurumia wanyonge walipa kodi. Mungu awake thawabu zao. Wasikae na hela maisha yao yote. Amina.