Tetesi: Hospitali ya Ipamba wagonjwa na wauguzi hupotea tu

Nimesoma Tosamaganga miaka sita yaani kutoka kidato Cha kwanza mpaka Cha sita sijawahi sikia hilo. Na tulikuwa tunauguzana yaani classmate wako akiumwa tunapeana zamu alafu full kuzurula USIKU magengeni, ila sijawahi sikia ama kuona hili usemalo. [emoji23][emoji23][emoji23]
Mtoa mada toa fact za ushahidi ulioonekana ili tuamini.
 
dah aise..
hii ulisimuliwa, inasemekana au uliwahi kwenda mpka pale, na ukanusurika kupotea au unaogopa kupotea?

na hao waliokusimulia wapo na walinusurika kupotea?🐒

vp wajenzi wa hiyo hospitali nao walipotea, akina nani hupeleka vifaa tiba eneo hilo na je waliwahi kupotea 🐒

unadhani ni tangu lini matukio kama hayo yanatokea eneo hilo 🐒

unadhani ni zaidi ya watu wangap wanaweza kua wamehusika kati kasumba hiyo 🐒

na jee, unadhani ni ushirikina au uchawi 🐒

unaweza kuelezea handaki kwa ufupi 🐒
 
Hizi ni Hekaya za Abunuwasi.
 
Hizi ni Hekaya za Abunuwasi.
Nakazia hoja. Mara nyingi masimulizi kama hayo huwa yanalengo kuu la kuwaogopesha/kuwatisha watu ili wale wanaopeleka wagonjwa wao pale wawe na nidhamu ya utulivu kuzingatia kilichowapeleka hapo yan kumwuguza mgonjwa wao na sio tena kujitumbukiza kwenye kuzurura nje usiku. Je , unatoka nje kwenda kufanya nini ilhali vyoo vipo humo ndani na umekuja hapo kwa kazi moja tu ya kumuuguza mgonjwa wako? Tulia na acha kusumbua watu wengine na wagonjwa pia bila kusahau na Wahudumu wa matibabu Dokta na Manesi.
 
Hizi story zako hata haziaminiki 😂😂 yan mtu apoteze mama mkwe, mke na mtoto kirahisi tu, tena mtu mwenye gari ? Si angewajazia polisi huko,

Tafuta story nyingine 😂😂😂😂 hizi ndo zile hakuna anaeweza nyanyua fimbo ya Nyerere 😂😂😂
 


Story za Abunuwasi, na ni dharau kwa serikali kuongea haya mambo ambayo najua serikali tungeshughulika nayo.
 
Story za Abunuwasi, na ni dharau kwa serikali kuongea haya mambo ambayo najua serikali tungeshughulika nayo.
Yap! Na mtoa mada asipokuwa mwangalifu wakati mwingine anaweza kutakiwa atoe ushahidi au athibitishe hilo kwani Hospitali ni Taasisi nyeti - Sio vizuri na haikubaliki kuizushia mambo na kuipaka matope ilhali inashughulikia mustakabali wa Afya za watu kwa nia njema kabisa.
 
Stori za vijiweni.

Kwamba mtu mzima anapotezwa ili viungo vyake vitumike kutibu wagonjwa?
 
JamiiCheck watusaidie kwa hili
 
Bullshit ...
 
Kama wagonjwa na wahudumu upoteaa tu wewe unabakia hapo kufanya nn au kwenda kutibia kwa lipi Kama hbr za kupoteaa kwa watu una,zijuwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…