Tetesi: Hospitali ya Ipamba wagonjwa na wauguzi hupotea tu

Sijui kwa Nini Nyerere hospitali ya machizi aliweka Dodoma na hapo hapo pakawa na bunge na ikulu
 
Waaaapi; Huku kilabuni tunajinywea Ulanzi na esp. hapa Kitelewasi tunakula nyapula hatunaga hizo stori zisizo na mbele wala nyuma.
Nyie wa kitelewasi mpo ok, namzungumzia huyu jamaa wa kilabu cha sambuliti pale mlandege
kanywa komoni analeta story za ajabu
 
Hii ni imani potofu kama zile za wanyonya damu. Mambo ya kizamani sana haya. Mkiambiwa muweke majina ya waliowahi kupotea, ndugu zao na anuani za makazi yao mnawajua?
 
Mbona kama inafanana na Ile movie ya Leonard di Caprio ,A cure for wellness?
 
Mimi nimesoma hapo Tosa miaka hiyoo kitambo sijasikia hii kitu.

Zitto Kabwe na wengine wengi wamesoma hapo sijawasikia wakilalamikia hizi habari.
Labda ni matukio ya miaka ya karibuni.
Mimi nimefundisha Tosa na nimeuguza wagonjwa wengi pale na tuna connection ya waliofanya kazi Ipamba Tanesco lakini hatujawahi kupata taarifa hii
 
Hizo habari ni za kweli, lakini huwa ni kama za siri sana kwani hata ikitokea huwa hakuna kwa kulalamika kutokana na mazingira ambayo watu huwa wanapotea.
Wapo wenyeji wenye uwezo wa kuthibitisha uwepo wa matukio hayo hasa wale wa mazingira ya vijiji vya jirani (Njiapanda, Kitwiru, Tanangozi, Mlolo, Ng'eza, Nyabula, Ikuvilo, Tagamenda na vingine)
Watu hupotea kimya kimya mithiri ya kutekwa vile.
 
Sijui kwa Nini Nyerere hospitali ya machizi aliweka Dodoma na hapo hapo pakawa na bunge na ikulu
Nyerere hakuiweka hospitali Dodoma.

Hiyo Hospital imejengwa na waingereza mwaka 1927 ikaanza kazi kupokea wagonjwa wenye matatizo ya akili kutoka sehemu mbalimbali za Tannganyika.
 
Nimesoma Tosamaganga 2009-2011 sijawahi sikia ilo swala
Hizi habari hazipo mashuleni, bali zipo mtaani hasa kwa watu wazima. Mata nyingi mtu anapoenda kuuguza mgonjwa wake kule hupewa tahadhari na wanaofahamu.
Wanafunzi wanavokuwa shuleni ni wachache sana ambao hupata habari za uraiani hususani wanafunzi wa shule za bweni kama Tosamaganga
 
hadithi njoo uongo njoo utamu kolea
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…