More updates: Msiba upo Kijiji Cha Ulonga karibu na Tengeru, familia ilipata bill ya milion 38+ baada ya ndugu yao kufariki
Wakalipa 20M wakakataliwa kuchukua mwili hata baada ya kupeleka nyaraka za nyumba Kama dhamana
Walikuwa wanatumia bima ya NHIF wakiamini inacover kila kitu hivyo awakujua Kama wanadaiwa, walipokwenda kuchukua mwili wakiwa tayari wameshakamilisha tartibu za mazishi ikiwemo kuchimba kaburi ndipo walipojulishwa kwama kitengo Cha uhasibu wanadai mgonjwa wao hakutibiwa kw gharama za bima na hivyo gharama wanazotakiwa kulipa Ni milioni 38.
Kwa taarifa hizi za ndanu ya familia inabidi tujue bima ya NHIF inatibu vitu gani?
Mgonjwa anadaiwa kukaa hospitalin hapo kwa miezi miwili muda mwingi akitumia oxygen means gharama kubwa zilikuwa za oxygen na hospital inadai bima ailipii oxygen.
Lakini pia inaelezwa hii siyo familia ya Kwanza, watu wengi wanaotibiwa kwenye hospital hiyo uishia kuuza Mali kutokana na gharama. Mnaofahamu hospital hii tusaidieni kujua inavifaa gani vizito hivyo?
Tumeshuhudia wagonjwa wakipelekwa Hadi India kwa gaharama za milioni ishiri na utibiwa na kurudi.
Hii milioni 38 kwa mgonjwa ambaye yupo kwenye uangalizi tu inatokana na huduma gani zaidi ya matibabu?
Tunaomba tupate elimu ili tujue namna ya kukabiliana na changamoto Kama hizi, unalazwa hospital miezi miwili unalipa milion 40+? Hii hospital ina hadhi gani kubwa kwa gharama hizi?