Tetesi: Hospitali ya Seliani Arusha inayomilikiwa na Kanisa yazuia mwili wa Marehemu wakidai walipwe fedha za matibabu cash

Tetesi: Hospitali ya Seliani Arusha inayomilikiwa na Kanisa yazuia mwili wa Marehemu wakidai walipwe fedha za matibabu cash

Matibabu ya Covid ni ya gharama kubwa Sana serekali ipo kimya kuna rafiki yangu Baba yake alilazwa walikuwa wanalipa 500,000 kwa kila mtungi wa oxygen.... Nikimsikia mtu anadai hamna Covid nasema huyo hajui anachosema maana gharama za matibabu sio rafiki kabisa.
 
Yaan ukitaka kujua hii nchi watu hawana akili Ni kwenye hyo bima ya taifa eti kifurushi like kikubwa n zaid ya 1m alafu wanakupa masharti ya watu watakaonufaika pili masharti ya kutibu ugonjwa Mara gonjwa hili lalipo kwenye bima Mara Dawa hii haipo kwenye bima kiufupi wizara ya afya imeshindwa kujipanga kwenye kusimamia afya za watanzania.

Kuna wale watumishi waserikali Hawa nawapa pole kwanza wanalazimishwa kuchangia sababu hawana sehemu wanaweza kataa kuchangia pili anaechangia ndio anaeamua mnufaika awe nani Sasa unakuta eti mnufaika wa pili kupitia mchangia bima eti sababu n umri zaid ya 18yrs eti sababu hasomi hawezi kunufaika kwanini? Haya anaechangia bima n mzee umri umeenda anakatwa hela ya bure Sasa kaamua kumuweka mjukuu wake anufaike eti bima hawataki!

Sasa hii n bima ya afya ya taifa au kituo cha kukusanya pesa kwa udanganyifu wa kutoa bima?

Mtanzania anajitibu kwa pesa zake mwenyewe nasio mfuko wa bima.
 
Ni kweli..na hiyo familia imeamua kuuza nyumba iliyopo kikatiti ili walipe gharama wanazodaiwa.....bado nyumba hiyo haijapata mteja
 
Updates: Confirmed, ni Mama mtu mzima zaidi ya miaka 60 ambaye kwa sera ya wizara ya afya alipaswa kutibiwa kwa bima lakini pamoja na bima anadaiwa zaidi ya milioni 30 kutokana na kuwekewa oxygen kwa zaidi ya miezi miwili aliyolazwa hospitalini hapo.

Kitengo Cha uhasibu, menejimenti ya hospital ambayo ina viongozi wa dini pia ndiyo inayofanya haya. Tatizo la kukataliwa dhamana ni mgongano wa kisheria uliopo kwamba deni si la familia Bali ni la Marehemu hivyo kuliamishia kwa familia itasumbua kulipa.

Uongozi wa serikali wamekaa kimya na baadhi wameungana na Hospitali hiyo kwamba kinachofanyika ni sahihi. Kwa Mimi nadhani tatizo hizo hili la matumizi ya gesi ni kubwa kutokana na COVId na wanaopata changamoto hizi ni wazee zaidi. Endapo serikali itaendelea kujitenga na gharama za matibabu ya covid familia nyingi zitaongia mgogoro na serikali pamoja na Hospitali.

Wizara ya Afya najua mnaelewa mkasa huu kwa sababu naambiwa familia hiyo imeripoti serikalini zaidi ya wiki na nusu Sasa na hakuna hatua.

Awali nilidhani Hospitali ndiyo ina makosa kumbe ni msimamo wa baadhi ya viongozi japo unapingana na tamko la serikali. Nani yupo sahihi? Msimamo wa serikali, msimamo wa hospital na ofisi za Wilaya serikali Wilaya?

Naendelea kuchimba ntaleta majina ya mhusika na eneo exactly msiba ulipo ili vyombo vya habari vifike kuanika ukweli
Covid-19 alazwe miezi miwili on oxygen!!?
 
Usipende kuongea usiyoyajua ilimradi tu yakutoke. Hiyo sio hospital ya kanisa, ni jengo ndio mali ya KKKT ila imepangishia wengine wakaweka hospital.
Nakubaliana kwamba hiyo hospital ipo zaidi kifedha watu hapo wanajali zaidi fedha kuliko utu.
Seliani n moja ya hospital zilizo chini ya umiliki wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania zingine n Hydom-Manyara, Nkoaranga-Arusha, Machame-Kilimanjaro, Kcmc-Kilimanjaro, zipo nyingine karatu, Mwanza bukoba na kwingineko.

Pia n moja ya hospital ambazo zinanufaika na ruzuku ya afya na msamaha wa vifaa Tiba achilia mbali misaada ambayo wajerumani na kwingineko wanawapa kwania ya ili waweze kutoa matibabu kwa kila mtu.

Bodi ya hospital imejaa wachungaji na maaskofu lakini ukienda pale kupata matibabu utakimbia.

Kwa watu wa Arusha wanakwambia ukienda kutibiwa Selian wanakushangaa wanasema umeenda hotel na hukwenda kupata matibabu pale.
 
Haya ndo makanisa yanajifanya ya mungu dini ni moja tu japo inapigwa vita sana
Hiyo dini moja tu inayopigwa vita sema hapa kama mwakilishi wake unadhani deni zaidi ya Tsh 30 millions ingeweza kulifidia vipi ili hiyo taasisi iendelee kuhudumia jamii kesho?

Hapo zimetumika dawa,mitungi ya gas etc na ukisema wasilipwe hiyo pesa kesho materials watanunua na nini?ukipeleka mgonjwa wako hajapata matibabu stahiki unasema huduma zao mbovu hujui kuachia achia vitu kama hivi ndo kunakozorotesha huduma?hilo deni familia wakae chini waombe atleast walipe nusu nusu itakayobaki taasisi iwajibike usirahisishe mambo huo siyo mchezo wa upatu kwamba kijumbe kafa.
 
Ni kweli..na hiyo familia imeamua kuuza nyumba iliyopo kikatiti ili walipe gharama wanazodaiwa.....bado nyumba hiyo haijapata mteja
Hali Ni mbaya, serikali inakopa trilion na moja ya kipaombele Cha hizo fedha Ni kununua gesi, je gesi zikinunuliwa gharama itapungua?

Hadi familia inauza nyumba waweze kumzika ndugu yao watoto wanaobaki watalala wapi?

Kiongozi wa serikali akiugua gharama za matibabu zote wanalipiwa na serikali lakini wao Wapo tayari mwananchi alale nje kulipa gharama za matibabu za mzazi aliyefariki. Hii haikubaliki huu ni unyama.

Kama unaweza kutoa location ya msiba na namba za simu za Kiongozi wa hiyo familia zitoe watu watu watatuma pesa kulipa hilo deni kuliko familia ilala nje baada tu ya mazishi. Weka mawasiliano hapa tuwachangie , tusipokubali kuungana kwenye matatizo tukategemea hawa wanaolipiwa kila kila kitu tutazidi kudidimia.

Namkubali Sana yule jamaa wa tweeter anayeahamasisha watu watoe michango kwa wagonjwa na watu wenye matatizo, anatambua wazi kwamba viongozi wapo tayari wakae na mabilioni kwenye akaunti lakini wananchi wanyanyasike.

Tupe location na namba ya simu ya wahusika tuokoe nyumba kuuzwa
 
More updates: Msiba upo Kijiji Cha Ulonga karibu na Tengeru, familia ilipata bill ya milion 38+ baada ya ndugu yao kufariki

Wakalipa 20M wakakataliwa kuchukua mwili hata baada ya kupeleka nyaraka za nyumba Kama dhamana

Walikuwa wanatumia bima ya NHIF wakiamini inacover kila kitu hivyo awakujua Kama wanadaiwa, walipokwenda kuchukua mwili wakiwa tayari wameshakamilisha tartibu za mazishi ikiwemo kuchimba kaburi ndipo walipojulishwa kwama kitengo Cha uhasibu wanadai mgonjwa wao hakutibiwa kw gharama za bima na hivyo gharama wanazotakiwa kulipa Ni milioni 38.

Kwa taarifa hizi za ndanu ya familia inabidi tujue bima ya NHIF inatibu vitu gani?

Mgonjwa anadaiwa kukaa hospitalin hapo kwa miezi miwili muda mwingi akitumia oxygen means gharama kubwa zilikuwa za oxygen na hospital inadai bima ailipii oxygen.

Lakini pia inaelezwa hii siyo familia ya Kwanza, watu wengi wanaotibiwa kwenye hospital hiyo uishia kuuza Mali kutokana na gharama. Mnaofahamu hospital hii tusaidieni kujua inavifaa gani vizito hivyo?

Tumeshuhudia wagonjwa wakipelekwa Hadi India kwa gaharama za milioni ishiri na utibiwa na kurudi.

Hii milioni 38 kwa mgonjwa ambaye yupo kwenye uangalizi tu inatokana na huduma gani zaidi ya matibabu?

Tunaomba tupate elimu ili tujue namna ya kukabiliana na changamoto Kama hizi, unalazwa hospital miezi miwili unalipa milion 40+? Hii hospital ina hadhi gani kubwa kwa gharama hizi?
 
Big up Ayo TV online kwa kufanyia kazi taarifa hizi nimeona Hospitali wanahojiwa wanakanusha na kibaya zaidi Daktari bila haya anasema hakuna mwanafamilia aliyejitokeza wakati wanafamilia wanasema wamekataliwa kuchukua mwili.......Ni Nani atafiwa na mzazi akamwacha mochwari wiki nzima?

Serikali ichukue hatua iwe fundisho kwa watu wenye tabia hii, lakini pia ofisi za serikali huko arusha walikuwa na taarifa mbona awakuchukua hatua?

Tumetimiza wajibu wetu wakuibua wengine timizeni wajibu wa kusimamia uadilifu kwenye taasisi zenu. Binadamu mcha Mungu awezi zuilia maiti mochwari, Hawa Ni wakatili
 
Nimepata Taarifa kutoka kwa familia moja ambao wameoa huko Mkoani Arusha zikisema walipata msiba wa Mkwe zaidi ya wiki Sasa lakini mazishi hayajafanyika kwa sababu Hospitali inadai haitotoa mwili hadi walipwe deni la matibabu. Taarifa zinadai wanafamilia wamepeleka zaidi ya nusu ya fedha na hati za nyumba lakini Hospitali imekataa kutoa mwili.

Hii inatokea siku chache baada ya Viongozi wa awamu ya sita kupiga marufuku utaratibu huu wakutoa adhabu kwa Marehemu au kulazimisha familia kulipa frdha ambazo kiukweli awana uwezo nazo.

Nazidi kufuatilia jina la wahusika na viongozi waliohusika kupingana na maelekezo ya Mhe. Rais na ntawaweka adharani hapa pale ntakapofanikiwa kupata Taarifa rasmi.

Aidha, ni wakati muafaka wizara ya Afya kufuatilia kadhia hii ambayo naambiwa imeripotiwa kwa mkuu wa Wilaya na Mganga mkuu na hakuna hatua walizochukua Hadi Sasa. Wizara mnapaswa kusimamia kwa vitendo maelekezo ya Mhe Rais ikiwezekana mkatoa mwongozo wa Nini hospital binafsi na hospital za serikali zifanye pale wanapobaini deni la mgonjwa linaongezeka kuliko kung'ang'ana na mwili wa Marehemu ambao kwa vyovyote vile hautaweza kulipa hizo gharama.

Lakini pia taasisi za dini angalieni utaratibu huu mnaotumia kwenye taasisi zenu
We ndo mala ya kwanza kuona maiti imezuliwa? Nenda muhimbili kaulizie. Vitaarifa vya kichonganishi sana eti inamilikiwa na kanisa.
 
More updates: Msiba upo Kijiji Cha Ulonga karibu na Tengeru, familia ilipata bill ya milion 38+ baada ya ndugu yao kufariki

Wakalipa 20M wakakataliwa kuchukua mwili hata baada ya kupeleka nyaraka za nyumba Kama dhamana

Walikuwa wanatumia bima ya NHIF wakiamini inacover kila kitu hivyo awakujua Kama wanadaiwa, walipokwenda kuchukua mwili wakiwa tayari wameshakamilisha tartibu za mazishi ikiwemo kuchimba kaburi ndipo walipojulishwa kwama kitengo Cha uhasibu wanadai mgonjwa wao hakutibiwa kw gharama za bima na hivyo gharama wanazotakiwa kulipa Ni milioni 38.

Kwa taarifa hizi za ndanu ya familia inabidi tujue bima ya NHIF inatibu vitu gani?

Mgonjwa anadaiwa kukaa hospitalin hapo kwa miezi miwili muda mwingi akitumia oxygen means gharama kubwa zilikuwa za oxygen na hospital inadai bima ailipii oxygen.

Lakini pia inaelezwa hii siyo familia ya Kwanza, watu wengi wanaotibiwa kwenye hospital hiyo uishia kuuza Mali kutokana na gharama. Mnaofahamu hospital hii tusaidieni kujua inavifaa gani vizito hivyo?

Tumeshuhudia wagonjwa wakipelekwa Hadi India kwa gaharama za milioni ishiri na utibiwa na kurudi.

Hii milioni 38 kwa mgonjwa ambaye yupo kwenye uangalizi tu inatokana na huduma gani zaidi ya matibabu?

Tunaomba tupate elimu ili tujue namna ya kukabiliana na changamoto Kama hizi, unalazwa hospital miezi miwili unalipa milion 40+? Hii hospital ina hadhi gani kubwa kwa gharama hizi?
Hiyo hosp ya Arusha kuna matukio 2 ya kuhusu BILI kubwa za oxygen baada ya mtu kufariki nimezisikia.
 
Hivi wanaporuhusu kuchukuliwa mwili wa marehemu bila kulipiwa gharama za matibabu Nani anabeba hizo gharama.....!

Kwa sababu haiwezekani waruhusu bure kabisa labda kufikia Mwaka mmoja Hospitali za binafsi zote zitakuwa historia kwamba zilikuwepo.

Serikali iendelee kutoa huduma lakini mashirika na watu binafsi wafanye biashara ya huduma kwa utaratibu mzuri.
 
Mlipe deni, hiyo ni biasharaa
Wananunua madawa, vifaa, wanalipia kodi, kulipa wafanyakazi.

No mercy under capitalism
 
Lakini pia taasisi za dini angalieni utaratibu huu mnaotumia kwenye taasisi zenu
Dawa ya deni ni kulipa. Hata kama ni taasisi ya kidini, madam inajiendesha kibiashara, ni lazima ikusanye mapato. Tusitake vya bure kwa kichaka cha hudua za taasisi ya kidini
 
Back
Top Bottom