Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndo hivo mkuu, nilkua nimeshachoma sindano 2 alafu sion nafuu nikazidiwa zaid , tukashtuka hebu twende hospital nyingineSasa si wanaweza kukuua hawa, bahati nzuri uliwahi kuhama ungebaki hali ingezidi kuwa mbaya
Huo uspecialist wako labda uwe katika hospital yako binafsi ndio unaweza kuonana bure na wagonjwa,lakini ukiwa umeajiriwa hauwezi kuonana na wagonjwa bure tu unalipwa mil 3 halafu uonane na wagonjwa bure tu?Kwani specialist nini bwana, mimi ni specialist lakini hata bure unaweza kuniona..............unakuwa specialist ili uwahudumie watu kwa maarifa ya kiwango cha juu siyo ulipwe pesa nyingi. Haya mambo ndo yanafanya watu wanashindwa kuhimili gharama za matibabu hospitali wanakimbilia kwenye miti shamba. Kwa case ya huyu mleta mada yeye tayari ameshalipia kumwona daktari na vipimo nk. iweje apigwe tena cha juu kwenye dawa? acheni ku complicate mambo utafirkiri nyinyi hamtaugua wala kufa......
Inategemea na mambo mengi mkuu,mimi nimewahi kupeleka mgonjwa Bugando,ukiwa wodi ya VIP kipimo cha ultrasound ni kama laki moja hivi lakini mtaani ni elfu 10 mpaka elfu 15...ni sawa na uende hotel alafu juisi ya Embe ya azam ya boksi uuziwe 15 wakati mtaani ni 4000.Kwa hiyi ndio dawa yenye retail price ya 7000/= mtu auziwe 37000/= hakuna uwiano kabisa
Lakini hapo umesema ni VIP.Inategemea na mambo mengi mkuu,mimi nimewahi kupeleka mgonjwa Bugando,ukiwa wodi ya VIP kipimo cha ultrasound ni kama laki moja hivi lakini mtaani ni elfu 10 mpaka elfu 15...ni sawa na uende hotel alafu juisi ya Embe ya azam ya boksi uuziwe 15 wakati mtaani ni 4000.
kwa hiyo matibabu imekuwa biashara na siyo huduma......Huo uspecialist wako labda uwe katika hospital yako binafsi ndio unaweza kuonana bure na wagonjwa,lakini ukiwa umeajiriwa hauwezi kuonana na wagonjwa bure tu unalipwa mil 3 halafu uonane na wagonjwa bure tu?
Private Hospital zote consultation fee ya kuonana na specialist ,super specialist sio chini ya elfu 50 hutaki kutoa pesa nenda ukaonane bure na Clinical officers
Ndio maana nimesema inategemea mambo mengi,inategemea sana uwekezaji wake upoje,hizo pesa alizowekeza inabidi zirudi.Kuna mambo mengine unaweza kuta ni ya nyuma ya pazia,mfano aina ya wataalam alio nao,anayeweka clinical officers hawezi charge sawa na anayeweka MD,watu wa maabara kaweka wa level gani? Nurses ni wa level gani? Zile darubini za maabara zipo za laki nane, milioni 2 na kuendelea.... kwahiyo uwekezaji ndio unafanya gharama zipo juu.Lakini hapo umesema ni VIP.
Kiukweli hospitali nyingi binafsi has mjini Daslam ni za kinyonyaji sana especially upande wa Madawa.
Kuna hospital inaitwa Mt. Consolata huko Ikonda Makete kule gharama za matibabu ni ndogo kero ni gharama za nauli kuifikiaGharama za uendeshaji wa kituo cha afya ni kubwa sana,kodi ya jengo,kodi za biashara,mishahara ya wafanyakazi,bili za maji na umeme.Siwezi sema umepigwa hela kubwa sababu sijui running cost ya hiko kituo.
Mimi sijakataa kabisa kwenye investment ndio mana pia tukienda baadhi ya hospital tunaambiwa bei ya kumuona C.O , MD, au specialist.Ndio maana nimesema inategemea mambo mengi,inategemea sana uwekezaji wake upoje,hizo pesa alizowekeza inabidi zirudi.Kuna mambo mengine unaweza kuta ni ya nyuma ya pazia,mfano aina ya wataalam alio nao,anayeweka clinical officers hawezi charge sawa na anayeweka MD,watu wa maabara kaweka wa level gani? Nurses ni wa level gani? Zile darubini za maabara zipo za laki nane, milioni 2 na kuendelea.... kwahiyo uwekezaji ndio unafanya gharama zipo juu.
Yan imagine kondoo moja inataka ikuchome sindano dawa hujui..Halafu wanavyodengua sasa utafikiri wanakuhudumia bure
Bora kwenda kwa mitishamba tu
Pia wana tabia ya kukurundikia madawa yani mtoto Ana homa tu nilirundikiwa mada mapaka basi .... nyumbanikwangu kumegeuka pharmacy ndogoPole sana Mkuu.
Vituo vya Afya vimegeuka chanzo cha kujipatia Utajiri Wa haraka.
Wengi huwa hawakubali kukuandikia Dawa ukanunue Pharmacy.
Kitengule hospitali ya wafu ile, hawana madaktari ambao ni prwoffesional hata kama ni proffesional bhasi hawana weledi wa kutosha kidogo wanaiulie binamu yangu hapo halafu gharama ziko juu sana.Jana nimeenda hospital moja hapa Tegeta kibaoni, na imeshajijua maana ipo peke yake pele kibaoni. Waanapiga bei kubwa sana wateja wao, kujiandikisha tu pale ni 7,500/= na sijui ni yanini maana hata file hupewi mambo yote yapo kwenye system za computer. Baada ya hapo anakwambia inachofuata ukamuone daktari, kumuona daktari ni 15,000/=. Dokata anakupa vipimo ukafanye, achana na gharama za vipimo hizi sibishani nazo.
Noma ilikuja baada ya vipimo vyote tukaandikiwa sindano 3 na dawa za kutuliza maumivu. Tuliambiwa gharama za sindano moja ni 37,000/= Hapo ndio kengele ikalia kichwani na kujua hapa kuna shida. Nikaomba niandikiwe ni sindano gani ili nichome mbele kwa mbele, hapo dokta akaanza kukataa anasema harusiwi kutoa hicho kitu inaweza kumletea shida kikazi, ilileta ubishi mkubwa sana kwakuwa mimi nimeshalipa kukuona na kila kitu kitoka kwako nimeshalipia na gharama za vipimo hapa niandikie hizo dawa mi niondoke, ndio kwa mbinde nikapewa majina ya hizo dawa.
Nikaenda pharmacy ipo opposite tu na hiyo hospital hizo dawa hapo wanauza 7,000/= tu na lile bomba la sindano ni 500/= Nikamlipa nesi 3000 nikachomwa sindano yaani 10,000/= nikawa nimepata tiba ambayo ilibidi nilipe 37,000/=
HOSPITALI MUWE NA HURUMA NA WATEJA WENU, MTU AKIUMWA ISIWE NAFASI YA KUMPIGA, SIO POA KABISA
Sasa mkuu kuna gharama za uendeshaji lakini fikiria kuna sdl,tra,mishaara,Kodi ya jengo,osha,zima moto,nssf,umeme,maji nk...kwa hiyo matibabu imekuwa biashara na siyo huduma......
Bima ya afya unaambiwa dawa hakuna kanunue kwenye madukaNdipo umuhimu wa bima ya afya huonekana
Kuwa serious basi , mimi nahudhuri klinik ya mtoto muhimbili. Gharama ni nafuu kuliko privateSasa mkuu kuna gharama za uendeshaji lakini fikiria kuna sdl,tra,mishaara,Kodi ya jengo,osha,zima moto,nssf,umeme,maji nk...
Amoxicillin caps inayouzwa pharmacy ni tofauti na amoxicillin inayouzwa hospital'amoxcillin ya hospital lazima itakuwa bei kubwa ili kufidia gharama za uendeshaji...sasa ukitaka dawa za pharmacy na hospital zifanane bei hapo lazima hospital itashindwa kujiendesha.
Hapo muhimbili tu matibabu ni gharama kubwa kuliko private
Usichokijua ni kwamba watanzania wenye bima ya afya ni 14% tu.Ndipo umuhimu wa bima ya afya huonekana