Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,660
- 3,501
Kwanza enzi hizo tulizoea jina moja tu la hoteli. Hili neno mgahawa lilikuja kama jipya/geni hivi na tukazoea taratibu kwahiyo hapa nitatumia neno mgahawa au hoteli kumaanisha kitu kimoja.
Sizungumzii makitu makubwa makubwa hapa nazungumzia vimigahawa vya kawaida vinavyopatikana uswahilini. Zamani tulizoea ukienda hotelini unaona ukutani MENU ya vyakula na bei zake hivyo kwa ajuaye kusoma kama ni mgeni wala hatapata tabu wala kuwapa taabu wahudumu kwa kuwauliza maswali mengi
Ajabu ya siku hizi ni kwamba wahudumu (hasa wanawake) wanaamini midomo yao kuliko maandishi, umefika mgahawani kimama kinajieleza mpaka kinaboa. Unakuta wateja kibao huku apike, huku aandalie wateja huku atafute chenji huku tena bado ajibu maswali ya wateja kuhusu vyakula alivyonavyo na bei zake. Matokeo yake nini sasa?
Ujue wabongo tulio wengi siyo mara zote tunakula tulichokipanga bali tunakula tulichokitamani. Wengine wana aibu kuuliza uliza maswali hawawezi au hawapendi kwahiyo unakuta umeagiza chakula fulani mara paap mwenzako mwingine kaagiza chakula kingine ambacho hukutarajia kabisa kama kipo. Unajikuta umeingia kwenye self conflict isiyo na maana
Halafu kumezuka mtindo mwingine tena mteja ukisema kwa mfano nipe supu utasikia ya ng'ombe au kuku, ukisema ya ng'ombe utasikia tena ya buku au buku mbili, ukisema ya kuku utasikia paja, shingo, bawa, kidali au paja ya juu nk mara chapati ngapi, ubwabwa wa sh ngapi..!? Maswali siyapendi haya! Kungekuwa na menu kwani tungesumbuana hivyo? Na of course mara nyingine haya makitu ndio yanaleta ugumu kuandika menyu maana orodha itakuwa ni kitini kizima
Miaka ya nyuma kule nyumbani ukisema supu ilikuwa ni tatu tu na hakuna maswali mengi (Kulikuwa kuna supu kama supu kisha kuna supu ya utumbo inayojumuisha mapupu na vitu vingine vya ndani kisha kulikuwa na supu ya kongoro, kuku enzi zile haikuwa ikipikwa supu- kuku ni mboga 🤣)
Tukirudi kwenye mada hebu andikeni menyu ya vyakula bana mturahisishie na mjirahisishie kazi. Binafsi nikifika hotelini huwa kama ni mgeni eneo hilo napata tabu sana maana kwanza sipendi maswali maswali lakini pia sijiandaagi kwamba naenda kula chakula fulani
#rudisheni menu migahawani#