Hoteli ya Sugu: Wafanyakazi wa Serikali wanavyoisaliti Serikali ya Magufuli

Hoteli ya Sugu: Wafanyakazi wa Serikali wanavyoisaliti Serikali ya Magufuli

Roho za kimasikini zikitawala , hata umuite muwekezaji gani hatokuja.
Tunafanyiana uzombie wenyewe kwa weyewe waTanzania, nani wa nje atatuamini.
Roho za kimasikini zikitawala , hata umuite muwekezaji gani hatokuja.
Tunafanyiana uzombie wenyewe kwa weyewe waTanzania, nani wa nje atatuamini.
Ndugu yangu unajua kuna kanuni moja. Kiongozi wa nchi kama rais akishajiwekea mazoea ya kufanya kazi yake bila kuheshimu katiba, sheria na taratibu za nchi tena wakati mwingine ili akomoe kikundi au mtu fulani tu basi anajenga precedence mbaya sana kwa waliyo chini yake. Si ajabu hapo hao walionuia kubomoa walikuwa wanadhani watamfurahisha aliyewateua kwani ndiyo style zake za kushughulikia mambo. Watu wa chini hawawezi kuheshimu sheria kama aliyetakiwa kuzitunza ndiyo wa kwanza kuzivunja.
 
Hio roho mbaya haiji hivi hivi huenda wanaiga mahali kwa kufuatisha mdundo wa ngoma
 
Ndugu yangu unajua kuna kanuni moja. Kiongozi wa nchi kama rais akishajiwekea mazoea ya kufanya kazi yake bila kuheshimu katiba, sheria na taratibu za nchi tena wakati mwingine ili akomoe kikundi au mtu fulani tu basi anajenga precedence mbaya sana kwa waliyo chini yake. Si ajabu hapo hao walionuia kubomoa walikuwa wanadhani watamfurahisha aliyewateua kwani ndiyo style zake za kushughulikia mambo. Watu wa chini hawawezi kuheshimu sheria kama aliyetakiwa kuzitunza ndiyo wa kwanza kuzivunja.
Lakini muda huu Rais JPM amekwisha onyesha kuwa viongozi wa Serikali wanapaswa kutumia akili katika suala la uwekezaji wa wananchi wake.
 
Tuwataje kwa majina waliomuandama Mengi.
Na je wao wametajirika?
Masiligi na marehemu mkapa na serikali yote ya awamu ya tatu. Cha kushangaza Mengi alikuwa CCM tena mwanachama mtiifu kisa ni mchaga tu. Yani mimatumbi ipo wazi mhindi awe amzidi utajiri mmatumbi mwenzake
 
Hao ndio wanaowaabudu weupe na kukandamiza weusi wenzake.Nakumbuka marehemu Mengi aliandamwa sana weusi wenzake hawakupenda awe tajiri!
Mtu mwenye cheo na dhamana lakini ana roho ya kimasikini, roho ya korosho, huwa wana shida kubwa sana.
Wanatumia kila sheria kukandamiza mfanyabiashara.

Tatizo hawajui kuwa kwa kufanya hivyo, wanakandamiza uchumi.
 
Wakati wa kampeni Lissu aliwaelimsha sana watu kuhusu yanayotendeka awamu hii kuhusu wafanyi biashara na TRA na maofisa wengine!
Mimi nadhani huu ulikuwa usanii moja ambao nia yake ilikuwa kuokoa jahazi na kuonyesha kuwa maneno ya Lissu hayakuwa kweli!!

Wakati mambo ya ajabu yametendeka hasa kwa wafanyi biashara hasa walio upinzani!
Shamba la Mbowe lililokuwa linajiri maelfu ya watu-je mkuu alichukua hatua gani kusahihisha hilo????
Billicanas- contracts kuvunjwa bila sababu yoyote kwa uonevu na kumwondoa mfanyi biashara anayelipa kodi kwa aibu kama walivyofanya
Mahoteli ya Mbowe-harassment ya mara kwa mara
Shamba la Sumawe-bila shaka litarudishwa sasa baada ya kurudi nyumbani!!! Hahaha!!!
Serikali iangalie sana tabia hizi za uonevu kwa maslahi ya wananchi wetu!!
Tunajionyesha kuwa watu wa dini sana lakini matendo yetu hayaendani na tunachohubiri!!!!
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Africa
Heri ya mwaka mpya 2021- Let us hope there will be change of heart now that we are all green!!! Hahaha!!!
 
Umesikia story ya Hai DC kichaa alivyoharibu miundo mbinu ya shamba kubwa la mwekezaji wa kizungu aliyekuwa ameajiri mamia ya watu???
Alimsimamisha huyo mwekezaji kwa miezi mingi bila sababu ya maana, wafanyakazi wakakosa kazi na miundo mbinu ikaharibika! Baadaye akamrudisha na mwekezaji alikataa akadai warudishe miundo mbinu yote kwanza kama ilivyokuwa!
Sijui kama hilo saga limeishaje!
Huyo DC kichaa ndiyo mtindo wake! Lakini kwa kuwa aliwezesha Mbowe akose kura huyu ni hero wa chama tawala badala ya kuitwa mhalifu!!!
Maendeleo hayana chama!!!
 
Hili sakata la kutaka kufunga Hoteli ya Sugu huko Mbeya limeleta hisia nyingi.

Lakini baya zaidi ni lile la the dark side ya watu fulani ndani ya Serikali.

Serikali inaendeshwa na watu.

Na watu hao maafisa ndiyo waliotaka watumie mgongo wa Serikali kubomoa Hoteli hiyo.

Kwa wafanyabiashara tunajua kuna watu-maafisa, wenye mamlaka na wana wivu, au kinyongo na maendeleo ya wananchi, hasa wafanya biashara.

Nimeambiwa huko Mbeya kuna viongozi wa ajabu sana. Pengine Magufuli atembelee Mbeya kujionea vioja cha maafisa au viongozi wake.

Miaka ya 2017 uwekezaji wa maparachichi ulitiwa misukosuko. Mwekezaji mzalendo wa ufugaji samaki kule Tukuyu-Kiwira badala ya Serikali kumtia moyo, kupitia DED wakamfungia mradi karibia miaka miwili bila sababu za msingi. Waliposikia Magufuli anatembelea Mkoa wa Mbeya, wakamfungulia mradi.

Hili ni kielelezo cha watu ndani ya Serikali wenye roho mbaya, na ni mbaya kwa wawekezaji.

Watu wa aina hii wako wengi na idara tofauti kuanzia ma DED, TRA, NEMC, hata baadhi wakuu wa Wilaya.

Hili sakata la Hoteli ya Sugu ni kielelezo tosha cha Watu wasioitakia mema serikali ya Awamu ya Tano.

Maafisa hawa wana msimamo wa kukomoa wafanyabiashara au wawekezaji.

Serikali kupitia Rais anasema hili, wakati baadhi ya maafisa wa Serikali wanatekeleza matakwa yao.

Rais Magufuli kwa kweli inabidi aelezwe tu kwamba kuna wafanyakazi/maofisa ndani ya Serikali yake wanamhujumu.
Ni Roho Mbaya tu za ma CCM dhidi ya CHADEMA
 
Ndio utaratibu unaanza na sugu mwambie ajipange si alisema jpm ni mtu mwoga sasa jpm anamsamehe na yeye anashukuru ila sisi kimyakimya tunadeal naye
JPM amezungukwa na wachawi wengi sana.ndio maana tunamlaumu rais mamb hayaendi kumbe kuna wahujumu wengi.Akili km hizi nchi hii itasongaje mbele.
 
Miswahili ni mijitu yenye roho mbaya sana. Yaani haitaki yenyewe ifanikiwe, inataka mkose wote, Basi tu wanafurahi sana wote mkiwa mafukara
Yaani mkuu nikipata kitu kama 10B hapa bongo napakimbia pa kipumbavu sana. Yaani waafrika tuna roho mbaya na nyeusi kama rangi zetu zilivyo.
Huo ni wivu na ni kweli ukikuta hata mkuu Wa wilaya anazidiwa na Hela na raia. Wanaumia sana wandhani kuwa kusoma ndo tiketi ya kuipata Hela.
Yaani jamani wanaumiaga sana kuzidiwa Hela na MTU ambaye hata hajui kusoma a ivyo wanamtengenezea zengwe ili wamtoe Hela tu.
 
Hili sakata la kutaka kufunga Hoteli ya Sugu huko Mbeya limeleta hisia nyingi.

Lakini baya zaidi ni lile la the dark side ya watu fulani ndani ya Serikali.

Serikali inaendeshwa na watu.

Na watu hao maafisa ndiyo waliotaka watumie mgongo wa Serikali kubomoa Hoteli hiyo.

Kwa wafanyabiashara tunajua kuna watu-maafisa, wenye mamlaka na wana wivu, au kinyongo na maendeleo ya wananchi, hasa wafanya biashara.

Nimeambiwa huko Mbeya kuna viongozi wa ajabu sana. Pengine Magufuli atembelee Mbeya kujionea vioja cha maafisa au viongozi wake.

Miaka ya 2017 uwekezaji wa maparachichi ulitiwa misukosuko. Mwekezaji mzalendo wa ufugaji samaki kule Tukuyu-Kiwira badala ya Serikali kumtia moyo, kupitia DED wakamfungia mradi karibia miaka miwili bila sababu za msingi. Waliposikia Magufuli anatembelea Mkoa wa Mbeya, wakamfungulia mradi.

Hili ni kielelezo cha watu ndani ya Serikali wenye roho mbaya, na ni mbaya kwa wawekezaji.

Watu wa aina hii wako wengi na idara tofauti kuanzia ma DED, TRA, NEMC, hata baadhi wakuu wa Wilaya.

Hili sakata la Hoteli ya Sugu ni kielelezo tosha cha Watu wasioitakia mema serikali ya Awamu ya Tano.

Maafisa hawa wana msimamo wa kukomoa wafanyabiashara au wawekezaji.

Serikali kupitia Rais anasema hili, wakati baadhi ya maafisa wa Serikali wanatekeleza matakwa yao.

Rais Magufuli kwa kweli inabidi aelezwe tu kwamba kuna wafanyakazi/maofisa ndani ya Serikali yake wanamhujumu.
Kujipendekeza kunawasumbua. Wanafikiri kuwafanyia ubaya wapinzani ni kumfurahisha bwana. Tuna viongozi wa ajabu sana.
 
A
Ndio utaratibu unaanza na sugu mwambie ajipange si alisema jpm ni mtu mwoga sasa jpm anamsamehe na yeye anashukuru ila sisi kimyakimya tunadeal naye
Acha roho mbaya kijana..kumbuka wewe ni marehemu mtarajiwa
 
Sugu aliwadharau sana watendaji sasa ajipande kwenye kodi maana hawatamuacha salama ajaiita rais huku analialia kushukuru rais og.

Aliifanya mbeya yake upepo umegeuka atulie sindano iingie
Acheni kutisha watu. Jinai haina kikomo nyambafu
 
Umesikia story ya Hai DC kichaa alivyoharibu miundo mbinu ya shamba kubwa la mwekezaji wa kizungu aliyekuwa ameajiri mamia ya watu???
Alimsimamisha huyo mwekezaji kwa miezi mingi bila sababu ya maana, wafanyakazi wakakosa kazi na miundo mbinu ikaharibika! Baadaye akamrudisha na mwekezaji alikataa akadai warudishe miundo mbinu yote kwanza kama ilivyokuwa!
Sijui kama hilo saga limeishaje!
Huyo DC kichaa ndiyo mtindo wake! Lakini kwa kuwa aliwezesha Mbowe akose kura huyu ni hero wa chama tawala badala ya kuitwa mhalifu!!!
Maendeleo hayana chama!!!
Kuna jamaa wa system aliteuliwa kuwa Balozi nchi fulani.

Kule ubalozini aliwaendesha rigwaride wafanyakazi utafikiri ni ofisi yake binafsi.
Wafanyakazi walipofikiwa na ndugu zao aliwazuia kabisa kutumia rest house ya ubalozi.
Balozi aliwaambia rest house ni kwa matumizi ya wageni wa Serikali tu.
Wafanyakazi wakalowa kabisa.
Katika pitapita zake huyo Balozi, alishambuliwa na vibaka na kuumizwa vibaya, baada ya muda ilibidi arudi bongo kwa mapumziko ya kustaafu.

Alipostaafu ilibidi arudi nchi ile ile kwa matibabu.

Akawakuta wafanyakazi wale wale ambao walimkatalia kata kata kutumia rest house ya Serikali.

Walimwambia ile sheria uliyoitunga kuwa rest house ni ya matumizi ya Serikali tu, haijatenguliwa, kwa hiyo mzee jitegemee mahotelini.
Jamaa ex Balozi alitahayari na kujiondokea.
Huyo ex Balozi alifariki muda baadaye.
Ubaya tunalipa hapa hapa duniani.
 
Huu nao ni ujinga mwingine unaoishushia JF heshima yake. Kauli ya rais ilikuwa very specific ni watu gani aliwalenga. Ingekuwa general kihivyo asingefanya vitendo kama vipe kumpa Bakhresa shamba la ekari elf 10 bure. Hizi ID za kificho zinatoa uhuru watu kupost ujinga.
Kwani Sasa hali ikoje kwa hao matajiri na wafanyabiashara kwa ujumla,wa chini na wa kati.Tuanzie hapo. Karibu.
 
Kwani Sasa hali ikoje kwa hao matajiri na wafanyabiashara kwa ujumla,wa chini na wa kati.Tuanzie hapo. Karibu.
Kujadili hali ya mfanyabiashara au wafanyabiashara fulani kunahitaji facts na siyo stori za kwenye vijiwe vya kahawa. Siwezi kujitia wendawazimu hapa kuanza kujadili watu nisio na taarifa za kutosha kuwahusu.

Kama nitataka kujijadili mwenyewe (maani nnaifahamu vema biashara yangu), basi ni kwamba sasa hivi nimerahisishiwa mazingira ya kazi. Sipati tena adha ya ushuru kila mara niendapo sokoni na bamia, mchicha, na chainizi ninazolima. Sasa hivi ni mwendo wa kitambulisho tu.

Pia REA imenisaidia kupata access ya umeme kwa ajili ya umwagiliaji wa bustani, kazi imebaki kwangu kununua incubator. Karibu uniungishe bamia mzazi. Ziko fresh like, ...
IMG_20210102_114248_056.jpg
IMG_20201210_202007_651.jpg
 
Back
Top Bottom