Hotuba kwa Wazee wa Dar: Rais Samia kuteua Viongozi bila kujali itikadi za Vyama

Hotuba kwa Wazee wa Dar: Rais Samia kuteua Viongozi bila kujali itikadi za Vyama

Mama nakuona kweli umedhamiria kuliunganisha taifa na kuleta maendeleo ya kweli. Nimesikiliza hotuba yako kwa wazee wa Dar es salaam nimeipenda mno, nakushauri kama itakupendeza muite Tundu Lissu na umteue awe mwanasheria mkuu wa serikali. Pia mimi niteue niwe CAG.
CAG Asad arudishwe

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
 
Bwashee umekuwa Sigara kali
Huyo MATAGA hana pa kujishikiza! Ni mnafki mkubwa aliyekua anatetea upumbavu wa kusema maendeleo haya chama..

Huku toa kauli akiwaambia hatowapelekea watu maji kama wasipoichagua CCM


Sasa hivi anaenda na upepo wa fursa kwenye utawala mpya
 
Rais Samia amesema kuanza sasa ataanza kuteua wachapakazi bila kujali itikadi ya kisiasa katika Serikali yake.

Amewataka watanzania kujiandaa kisaikolojia kupokea mabadiliko yatakayoleta Umoja wa Kitaifa.

Huko mbele katika kupanga safu za kujenga uchumi sitochagua, Mtanzania yeyote mwenye weledi na umahiri anayeweza kuleta manufaa kwa Taifa nitamuingiza afanye kazi, sitochagua huyu katoka Chama kipi yule katoka Chama gani lengo letu ni kujenga umoja wa Watanzania


Mkuu haya ndiyo maendeleo yasiyokuwa na chama ambayo hatimaye leo kibwagizo hicho umelazimika kuzisahau.

Mataga na ndugu zao wa chama fulani watakuwa wamenuna kweri kweri!
 
Sasa hapa unapinga au unakubali?

Maana tukisema tumuunge mkono mama yetu kwa nia yake ya kutaka kuwapa kazi wapinzani unakuja na vijimaneno vya hovyo
Safari lazima mhame nchi
 
Akikuteua lazima utekereze ilani ya chama,sioni jipya hapo hata akina Anna Ngwila, Magufuri aliwapa vyeo kutoka upinzani lakini wakatekereza ilani ya ccm.upinzani wa Tanzania tatizo sio ccm bali alikuwa Magufuri😄😄😄😁Samia kaja kuumaliza upinzani kabisa,maana atachukuliwa mwenye ndomo anapewa kipande cha myama😄😄😄😁
Asante sana mama hii ndiyo aina ya viongozi tulikuwa tunawasubiri.

Tanzania tulisha zoeshwa huchaguliwi hadi ujikombe, urambe viatu vya mteuzi uukane ukabila wako ndio upate teuzi.

Sipati picha leo hii wale mataga, chawa, sukuma gang watalala wapi masikini.
 
Bado matakwa yetu Watanzania ya kutaka Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi yako pale pale. Hii danganya toto haisitishi matakwa hayo. Zitto ameula Mkuu wa Mkoa wa Kigoma. 😜😜
Ni ajabu sana kuona watu wanvyoweza kuchotwa akili kirahisi rahisi.

Hapa ndipo unapoweza kuwatambua mamluki waliojazana huko kwenye vyama, na wafia vyama wenyewe.

Heko mkuu BAK.
 
Nenda kwenye kaburi la Jiwe then jipige kifuani ukilia ukisema"Kayafa ulitulisha ujinga na upumbavu"
Nadhani umesahau huyo Jiwe ndo aliwateuwa wapinzani. Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro, aliteuliwa kutoka ACT Wazalendo bila kuhama chama. Na alimuahidi Tundu Lissu pia kumpa madaraka. So kikubwa mama yetu anaendeleza.
 
Wewe hapa tupo tz! Na hao sukuma gang tunasubiri waje wawapelekee bavicha moto hiyo 2025 kwenye uchaguzi mkuu ndio warudi kwao.

Kikubwa kwa sasa kina lema wajiandae kula teuzi
Mtaumia sana kisaikolojia kudadadeeeeekiiii
 
Ukisikia maendeleo hayana chama, hii ndo maana yake. Haiwezekani eti mtu hadi awe mwana ccm ndo afikiriwe kupata fursa huko serikalini.
 
Tujenge umoja wa kitaifa[emoji1666][emoji1666][emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223][emoji2223]
 
Back
Top Bottom