HOTUBA YA LISSU MAREKANI
π. ππ£ πͺπΌπΏπΉπ±
Mkataba wa DP World na TPA (HGA) umevusha sheria ya mwaka 2017 ulinzi wa maliasili inakataa kuingia mkataba kabla ya kupelekwa bunge
Mikataba yote ya rasilimali kesi zake ni lazima vifanyike kwenye maahakama za ndani ya nchi tu kama kuna mgogoro, Mtakaba wowote ulishapelekwa Bunge unakuwa public kwa kila mwananchi
Mkataba unapopelekwa bungeni inakuwa public document
Walijaribu kuondoa masharti haya kupitia mswada kuondoa hii sheria ya 2017 lakini wakashindwa , sababu walitaka kuendana na mkataba DP World, kuendelea na HGA ni kuvunja katiba
Mimi sina Imani na wanachosema mpaka nione mkataba wenyewe , wauweke hadhari, serikali yetu imejaa waongo , kuna wizi umefanyika serikali kwa miaka mingi, tena unafanyika IKULU, imekuwa nyumba ya waranguzi ukinza Bandari, Tegeta escrow, EPA yote hii imefanya na maraisi IKULU
Kabudi hakukosea alipomuita rais mungu, kwa katiba yetu ni mungu mtu, Ndio maana unaona Bandari leo inauzwa na Samia kwa mwaarabu
π. ππ¨ππ¨π¦U πππ₯ππππ§π π‘π ππ¨ππ’π¦π’πππͺA CHADEMA
Tunahitaji umoja makundi yote bila kubezana
Lazima tujitofautisha na na kauli zinazofanana na CCM, ukikosolewa unasema umetukanwa, unakuwa na chawa wa kushambulia, CHADEMA lazima tukosolewe, Kwa sasa tumakuwa chama kikubwa kuna vitabia vya ovyo vimeanza jengeka kwa baadhi ya watu, hatukuwa na hizi tabia huko nyuma
Ukiona mtu anashambulia kundi lolote linalofanya harakati kutafuta haki nchini, huyo mtu anafanyakazi ya CCM, anafanyakazi ya Shetani
Ni bahati mbaya kwamba kuna kauli zinatolewa kudogosha Diaspora ambao wametupigania sana CHADEMA na wamepigana haki nchini, tunawachukulia DIASPORA kwa maslahi bila kungalia umuhimu wa mchango wao lakini faida ya kazi zao wanazofanya
Lakini Diaspora mnapokua na jambo uratibu ufanyike vizuri na taarifa vifikie pande mnazotaka kushirikiana nazo kwa wakati.
C . DIASPORA
vi. Uraia pacha ni muhimu, kwa sasa kuna idadi kubwa ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi, zamani walikuwa watoto wa viongozi tu, lakini sasa kuna Watanzania kutoka matabaka yote. CCM wameona kuna watu wengi wanaliogopa ili kundi sasa ni kubwa.
D. UONGOZI WA CCM NI OVYO
Hivi tunaweza jilinganisha kipi na majirani kama Kenya, ni kitu gani tumefanya vizuri kuliko wakenya? Niambieni kimoja tu tunachofanya vizuri , Kuna wanaosema kwamba hatuna ukabila Tanzania, sasa nenda chuo kikuu DARE ES SALAAM,ukaone ni kina nani wanakuwa maprofesa pale, Kisha rudi niambie hatuna ukabila
Makonda (Katiba Mwenezi CCM), Kingai (DCI) na Wambura (IGP) ni mharifu, Wamefanya mambo ya kikatili sana, Makonda ameshiriki sana kuumiza watu na kutengeneza kesi za uongo, Yeye Kingai na Wambura kesi zangu zote walikuwa wanahusika nazo, Nilikuwa nakamatwa popote Tanzania na kupelekwa kwa Kingai ambaye alinipeleka kwa Wambura, Hivi teuzi za watu wa ovyo zimeanza kitambo, Samia amekuwa akiteua watu wenye tuhuma za uharifu, kurudi kwa Makonda tujipange kutakuwa na ukatili mkubwa sana. Tunatakiwa kujiandaa sana, kutakuwa na mambo mabaya, kutakuwa na giza siku za mbeleni
Kuna wakati CCM ilikuja na VISION 2025 kuna nini wamefanya? wameandika mambo mengi ya uongo pale ndani, sasa wamekuja na VISION 2050 pia wamejaza uongo mtupu, wamekuwa watu wakuandika mauongo kila siku
E. MARIDHIANO HAKUNA CHOCHOTE TUMEPATA , CCM IMEKATAA KILA KITU
Baada ya mwaka mzima wa mazungumzo tuliwaandikia CCM masuala tuliyozungumza na walikuwa wameyakubali baadhi, lakini tulipowataka kundika wakakwepa kwepo, baadaye walijibu na kukataa mambo yote hata yale mwanzo walionekana kukubali , Lakini kwenye maandidshi wamekataa kila kitu
Kama wanataka maridhiano kwa nini wanakataa kuweka kwenye maandishi
Ni kweli tumekuwa wepesi kumshangilia Samia, Mimi nilimshangilia kiasi na nikawekwa kwenye mabango ya mama, ila nikaweka tweet tuwe na tahadhali katika kumshangilia huyu Rais, kuna wakati nampiga makombora, si ni muhimu kuwa makini
Ni kweli kuna hali ya kupigania kidogo maridhiano, ila kwa kweli maridhiano hakuna kitu, Kuna watu wanasema sijui wafungwa wameachiwa, mikutano ya vyama vya siasa imeruhusiwa, Mwenyekiti ameachiwa na mengine mengi, ila kweli ni kwamba, Masuala ya Wafungwa kuachiwa, mwenyekiti na kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa na wale Covid 19 ni masharti tuliweka kabla ya maridhiano kuanza, Mwenyekiti ameachiwa kabla ya maridhiano, nilipoona na Rais Mara ya kwanza nilimpa hayo masharti kwa haji ya maridhiano.Kama kuna mtu anadai hayo ni matundo ya maridhiano niko tayari aje kunielimisha kivipi masharti ya kuingia kwenye maridhino iwe matunda ya maridhiano.
Kwa kifupi MARIDHIANO tumeliwa, ni ngumu tu kusema lakini ni wazi tumeliwa, hata hayo yanayosemwa ni matunda ya maridhiano sio kweli, yalikuwa ni masharti ya maridhiano , Maridhiano ulikuwa ujanja ujanja tu wa kupoteza muda, tunatakiwa kuwa makini sana na serikali ya CCM ni waongo
F. KATIBA MPYA
Watanzania tunatakiwa kujiandaa kwa mambo magumu, maana katiba mpya itasaidia kufungua mambo mengi
Katiba yetu ya sasa ni ya CCM ni katiba ya chama kimoja, Katiba Itapatikana kwa njia moja tu, Lazima kutumia nguvu ya umma, Hakuna njia nyingine, Tunatakiwa kwenda nchi nzima kushinikiza Nguvu ya umma pekee ndio itatupatia katiba sio vingivyo
Marekani Kulikuwa na wanaharakati wengi na makundi mengi yalipigania misingi waliyonayo sasa, na walipambana kwa miaka 200 kupata mifumo bora. Lazima tupambane sana, Marekani iliingia mpaka kwenye vita ya ndani kujikomboa, sio kazi rahisi kufanya ukombozi wa taifa lolote like
Mpaka leo hakuna matokeo ya urais jimbo kwa jimbo, matokeo yote yapo, ila ya Samia na Magufuli 2020 hakuna , na sheria inakata haya mambo
Tunakwendaje kwenye uchaguzi kwa mazingira haya, Tunakwenda je kwenye uchaguzi na Rais ambaye anauza maliasili zetu, anapora ardhi ya watanzania kila kona ? tunawezaje kwenda kwenye uchaguzi na mtu wa aina hii ?
Je tusipoenda kwenye uachaguzi nini kitatokea, je wataacha? Mimi nafikiri tulishasema hatuendi, hatujabadilisha msimamo, lakini tunatakiwa kujua tukienda kuna kikaangio cha uchaguzi, au turuke tuangukie kwenye moto pia, sio suala dogo, hatujatoa msimamo rasmi toka tumesema hatuendi, ila tutatoa msimamo mpya
Bila #katibaMpya tutakuwa na uchaguzi mbaya sana